PostGE2025 Polisi: Mpaka mchana wa leo Desemba 10,2025 hali ya usalama nchini ni shwari

PostGE2025 Polisi: Mpaka mchana wa leo Desemba 10,2025 hali ya usalama nchini ni shwari

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Tungependa tena kuendelea kutoa taarifa ya mwendelezo wa hali ya usalama hapa nchini kuanzia saa 12 asubuhi ya leo ya tarehe 10.12.2025 hadi mchana huu.

Hali ya usalama ni shwari na shughuli za kiuchumi na kijamii zinaendelea kama kawaida nchi nzima baada ya mapumziko ya jana tarehe 9.12.2025 ya sherehe za sikukuu ya Uhuru wa Taifa letu.

Jeshi la Polisi kwa ushirikiano na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama vitaendelea kushirikiana na nyinyi wananchi kuhakikisha amani na usalama unaendelea kuimarika hapa nchini ili hata wale wachache wenye hofu waweze kutoka waendelee na shughuli zao za kila siku za kujitafutia riziki na kupata huduma za kijamii wanazo hitaji.

Aidha, tuna washukuru na kuwapongeza wananchi wote kwa nafasi zao kwa namna wanavyoendelea kuwakataa na kuwapuuza wale wanaohamasisha na kuchochea vurugu na ukiukwaji wa Sheria za nchi kupitia mitandao ya kijamii na njia zingine.
1765361555425.png


1765361579970.png
 
Back
Top Bottom