Polisi Moshi yazuia jeneza la mwili wa Ndesamburo kupitishwa barabarani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Moshi limezuia utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa kuutembeza katika barabara za viunga vya manispaa hiyo, mwili aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, marehemu Philemon Ndesamburo .

Majibu ya barua yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Polisi Moshi, yamezuia mwili huo kupitishwa katika barabara za kati kati ya mji kwa kile walichoeleza kuwa leo Juni 5 na siku ya kazi na kuna shughuli za mbalimbali zinazoendelea.

Sababu ya pili iliyotolewa na ofisi hiyo ni kwamba wakiupitisha mwili huo barabarani watasababisha msongamano mkubwa ambao utakuwa chanzo cha usumbufu kwa watumiaji wengi wa barabarani.

“Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya inatoa maelekezo kuwa mwili wa Ndesamburo ukitolewa KCMC, upitishwe barabara ya YMCA kupitia Lucy Lameck Road hadi uwanja wa michezo wa Majengo ambapo kumepangwa kufanyika kwa shughuli zote za kutoa heshima za mwisho.

Jana mmoja wa wanakamati ya mazishi ya Ndesamburo, Anthony Komu aliliambia Mwananchi kuwa mwili wa Ndesamburo utachukuliwa KCMC saa 4 asubuhi na kupitishwa katika barabara kuu za mji wa Moshi ili kuwawezesha ambao hawatapata nafasi ya kufika Majengo, kuuaga mwili huo.
 
Waache mambo ya kitoto, Msafara wa Rais,Waziri unapopita katikati ya Mji na kusababisha msongamano huwa kunakuwa hakuna kazi za kufanya?

Sababu zingine ni za kijinga sana,waache watu wampumzishe mzee salama ana heshima kubwa sana Moshi kuliko mtu yoyote wa serikali
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Moshi limezuia utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa kuutembeza katika barabara za viunga vya manispaa hiyo, mwili aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, marehemu Philemon Ndesamburo .

Majibu ya barua yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Polisi Moshi, yamezuia mwili huo kupitishwa katika barabara za kati kati ya mji kwa kile walichoeleza kuwa leo Juni 5 na siku ya kazi na kuna shughuli za mbalimbali zinazoendelea.

Sababu ya pili iliyotolewa na ofisi hiyo ni kwamba wakiupitisha mwili huo barabarani watasababisha msongamano mkubwa ambao utakuwa chanzo cha usumbufu kwa watumiaji wengi wa barabarani.

“Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya inatoa maelekezo kuwa mwili wa Ndesamburo ukitolewa KCMC, upitishwe barabara ya YMCA kupitia Lucy Lameck Road hadi uwanja wa michezo wa Majengo ambapo kumepangwa kufanyika kwa shughuli zote za kutoa heshima za mwisho.

Jana mmoja wa wanakamati ya mazishi ya Ndesamburo, Anthony Komu aliliambia Mwananchi kuwa mwili wa Ndesamburo utachukuliwa KCMC saa 4 asubuhi na kupitishwa katika barabara kuu za mji wa Moshi ili kuwawezesha ambao hawatapata nafasi ya kufika Majengo, kuuaga mwili huo.
 
Mbona Serikali inakataa kukubaliana na taratibu za kamati ya mazishi ilihali hawajavunja sheria? na pia si waliomba vibali vya kufanya hivyo na ulinzi wa jeshi la polisi?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Si vibaya kwa wakaazi wa Manispaa ya MOSHI wakaacha shughuli zao kama kweli wana mapenzi ya dhati wakaenda kuuaga mwili wa marehemu.

Hii mambo ya kubishana na Serikali haisaidii,kikubwa ni wananchi wa MOSHI kuonesha kweli wameguswa na msiba wafunge maduka,ofisi na kila kitu chao ili wajumuike kwenye msiba.

Sidhani kama wanashindwa kupita mitaani na kipaza sauti kuwahimiza watu kufanya hivyo.
 
Mpaka wanaowafanya wasiwe na aibu watakapotoka madarakani ndiyo na wao watakuwa na utu na aibu. Sasa kama ni siku ya kazi kuna mtu analazimishwa kuacha kazi afuatilie mwili wa Marehemu Ndesamburo unapopitishwa barabarani?
 
Back
Top Bottom