sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,745
- 1,171
Matukio ya kamata kamata viongozi wa upinzani hayana tija, yakiendelea iko siku yataleta machafuko.
Kumekuwa na matumizi mabaya ya nguvu kuwakamata viongozi wa upinzani, hali inayo pingana na kaulimbiu ya jeshi hilo tii sheria bila shuruti.
Jeshi lisiposimama imara na kurudi kwenye maadili ya kuto kukitumikia chama fulani, hali itakuwa tete.
Kuna haja gani ya kutumia nguvu kuwakamata viongozi wa vyama vya upinzani, ikiwa matukio hayo mengi yalisha leta athari kwa jamii iliyo kuwepo kwenye mikutano yao.
Haya matumizi ya nguvu huenda yanafanywa kimkakati ili kuzua tafrani isiyo kuwa na tija.
Kwa hali hii wananchi wataliamini vipi jeshi lao la police!
Mbona upendeleo umetamalaki katika kutoa haki, mara ngapi CCM wanafanya mikutano yao tena yenye kejeli kwa wananchi, lakini jeshi lipo kimya.
Viongozi hawa wa CCM wana tofauti gani na viongozi wa upinzani ikiwa kila mkutano wa viongozi wa upinzani lazima usababishiwe ***** ***** na jeshi hili!
Kwanini IGP ana linyamazia jeshi analo liongoza kufanya mambo ya hovyo yanayo weza kusababisha machafuko!
Kama maneno ya viongozi yana chochea watu kuichukia serikali nani aliye peleka malalamiko hayo polisi!
Hivi ni kweli jeshi hili halina njia mbadala ya kuwahitaji viongozi hao kuripoti kituoni kwa mahojiani mpaka watumie violence!!
Hii nchi ni yetu sote, kila mmoja ana haki ya kulindwa utu wake bila kutwezwa utu wake wala kudhalilishwa kwa mujibu wa katiba.
Kwa matukio haya ni zaidi ya uhalifu, kwa kuwa yanasababisha hali ya usalama kwa viongozi hawa kuwa duni.
Pia yana dhalilisha utu na heshima ya viongozi kwa matakwa ya watawala kudhoofisha nguvu ya upinzani.
Jeshi lijitazame upya, jeshi likichafuka nchi imechafuka, uvumilivu nao hautakuwa na kikomo.
Kwa matukio yanayoendelea, machafuko yote yatakayotokea jeshi la police linawajibika, kwa kuwa limekubali kuwa green guard ya chama.
Pia jeshi liache utamaduni wa kuwapangia wapinzani nini cha kusema, vinginevyo wajisajili kuwa chama cha siasa ili wanapokerwa na hoja za wapinzani wazijibu wakiwa jukwaani.
Mwisho, Mwalimu alisema hoja haijibiwi kwa rungu.
Waambieni mamlaka ya juu wajibu wenu nini, kutumika kwa niaba ya upendeleo wa upande mmoja kutaangamiza uvumilivu wa Watanzania, badilikeni!!