Polisi, kwanini ni nyie tu?

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,091
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na shutuma nyingi zinazoelekezwa kwa jeshi la polisi ambazo nyingine zimekuwa zinalitia matope sana jeshi la polisi lenyewe hasa kwenye ile context ya kulinda usalama wa raia na mali zao lakini pia dhana ya polisi jamii kwa ujumla wake. Katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja tayari jeshi la polisi limejikuta kwenye sintofahamu zaidi ya tatu ambazo aote zinanifanya nitie mashaka utendaji na uadilifu wao.

Kwa mfano katika kipindi hiki jeshi hili limekutana na mambo yafuatayo;
  1. Kutekwa na kupigwa kwa Dr. Ulimboka ambapo limeshutumiwa moja kwa moja kwa mmoja wa maafisa wake kuhusishwa na tukio hilo
  2. Mwendelezo wake ni taarifa za kukanganya juu ya kukamatwa kwa mtu anayeshukiwa kuhusika na tukio lenyewe (taarifa zinakanganya na kupishana na za Gwajima) huku ikionekana taarifa ya polisi ni ya kuungaunga
  3. Mauaji yaliyotokea juzi huko Ndago kwenye mkutano wa CHADEMA ambapo polisi inasemekana walishindwa kuchukua hatua hata pale walipotakiwa kufanya hivyo na sasa wanawashutumu CHADEMA kwa kuhusika na tukio la mauaji.

Sasa kwa mtazamo wangu hii sio hali nzuri kutokea kwa jeshi lenye jukumu la kulinda raia na mali zao, ambalo halitakiwi kufanya kazi kwa kutoangalia itikadi za vyama au kutosema uongo. Najua kwamba kwa mujibu wa mfumo tulionao ambao unesapotiwa na katiba yetu, ni vigumu sana jeshi la polisi kufanya kazi against watawala kwasababu kwa mfano, Mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa maeneo yao (ambao ni makada wa chama tawala) ambao kimsingi ndio wanaotoa directives kwa viongozi wa majeshi (wakiwemo polisi) juu ya nini kifanyike kwenye maeneo yao. Kwa hali hii hutegemei polisi watende kinyume nao (Ukumbuke jeshini ni kufuata amri na huna ruhusa ya kuhiji amri ya mkuu)

Lakini ushauri wangu tu, zama tulizonazo zinaleta changamoto kubwa kwa jeshi la polisi, na kama litaendelea kujiweka mbali na wananchi kwa misingi hii litapoteza hadhi ya kulinda usalama wa mali na wao wenyewe, na kwa kuwa wao ndio wenye nguvu zaidi kwasababu ndio wenye nchi wanaweza kuhoji uhalali wa jeshi hilo kuwepo, na kama hawataona uhalali wake wataamua kutokuwa nalo na mi sitaki tufike huko so nawaomba tu jeshi la polisi wajitathmini kama wanaenda kwenye njia sahihi....
 
Labda kuna mengine pia wanasingiziwa kwani wao ndio walinzi wa amani hawawezi kuchomoka kama amani inapovurugika....

jukumu lao = amani = ghasia= huwezi kutenganisha mambo hayo.
 
Back
Top Bottom