Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
POLISI KUWAPIGA Waandishi wa Habari NI ISHARA YA ANGUKO LA DOLA.
Kunapotokea vita yoyote waandishi hushiriki vita kwa kuvaa mavazi maalum kwa ajili ya kutoa habari ya matukio yanayoendelea, na majeshi hayatakiwi kuwapiga risasi wala mabomu maana wanajulikana, na wapiganaji wanatakiwa kuwaheshimu. Hii inaonesha ni jinsi gani utaratibu wa kuwaheshimu Wanahabari ulivyotengenezwa kimataifa.
Inapotokea Nchi kupitia Jeshi lake la Polisi wanahabari wanapigwa mabomu au risasi kisa wamekuja kuchukua habari, ni laana kubwa maana bila wanahabari hatuwezi kujua chochote kuhusu uwajibikaji wa jeshi la Polisi, hatuwezi kujua wenye makosa wanaonewa au wanatendewa haki.
Wanahabari sio wachochezi bali kuwapiga wanahabari na kuwafedhehesha ndio kuchochea uchochezi yakinifu, wanahabari wakati mwingine wanasimama kama watetezi wa wanyonge na walala hoi kama Mimi Deogratius Kisandu.
Najua fika ya Mwangosi na ya Geita sio jeshi la kulaumiwa bali dola ndio inatakiwa kulaumiwa kwa kutokuweka miundombinu thabiti kwa ulinzi wa Wanahabari. Nacho jua Mimi Polisi hawezi toa kipigo kwa mwanahabari kama hajaagizwa maana kiutaratibu Polisi wanajua nyenzo ya uwepo wa wanahabari katika majukumu yao.
Tatizo letu, tunafikiri waandishi wa magazeti Fulani hao ndio halali kisa hayo magazeti yana milikiwa na chama Fulani au kigogo Fulani. Mwanahabari anaendelea kuwa mwanahabari hata kama ni wakujitegemea.
Nashauri, Wizara husika kufanya maboresho katika kuokoa uhai wa wanahabari katika mikutano ya aina yoyote ile. Kutengeneza urafiki shirikishi baina ya Jeshi la Polisi na Wanahabari.
Nawatakia Asubuhi njema.
Deogratius Nalimi Kisandu.