STUNTER
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 13,075
- 17,237
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na
Kupambana na Madawa ya Kulevya, ACP Mihayo
Msikhela amedai wamejipanga kufanya msako
dhidi ya wasanii wanatumia mihadarati hadharani.
Akiongea na gazeti la Mtanzania, Kamishna huyo
alisema wasanii ambao ndio kioo cha jamii, sasa
wamekuwa wa kwanza katika kusambaza ujumbe
wa matumizi hayo. “Mimi binafsi simfahamu Chid Benz kama ni mtu
maarufu aliyekuwa akifahamika kwa kiasi hicho,
lakini baada ya kumuona kwenye mitandao ya
kijamii ndipo nikaanza kumfuatilia,” alisema
Kamishna Msikhela. Alisema endapo wakipata taarifa ya kwamba
wanatumia hadharani na kuwakamata, basi
watachukuliwa hatua kama wahalifu wengine. “Hawa wasanii tunawasaka nao watuhumiwe
kama wahalifu wengine na wakichukuliwa hatua
itakuwa fundisho kubwa kwa vijana ambao
walikuwa na nia ya kujiingiza katika mtandao
huo,’’ alisema. Alisema ni vema kwa vijana wasiwafuate watu
maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine
wanaushawishi mkubwa kiasi katika matumizi ya
dawa hizo. Kamishna Msikhela alisema wimbi kubwa la vijana
wenye umri kati ya miaka 15 na 30 ndilo ambalo
linajiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya
jambo ambalo ni hatari kwa Taifa. “Vijana hawa ndio ambao wangekuwa tegemeo,
vijana wa umri huo ndio ambao wangekuja kuwa
viongozi wa baadaye, yaani kwa umri huo ndiyo
wanaandaliwa kuwa madereva, mawaziri,
wakulima, lakini leo wanakuwa mateja, ni jambo la
hatari sana,’’ alisema. Kamishna Msikhela alisema Jeshi la Polisi kwa sasa
liko katika mkakati maalumu wa kuhakikisha elimu
katika jamii inatolewa ili wananchi waweze
kuelimika. Alisema ulimaji wa bangi mashambani ni mkubwa
kuliko mirungi, lakini aliongeza kuwa kama mateja
mitaani wanapungua basi hata uingizaji wa dawa
hizo kwa sasa nao umepungua.