Polisi inavyotumiwa na CCM kusambaratisha upinzani

zaleo

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
1,902
764
Kutoka Yahoo friends
Nimeikuta ikizunguka, labda umeiona, ni kwa faida ya wale ambao hawakuiona.

Polisi wanavyotumiwa na CCM kuusambaratisha upinzani!!!ukweli huu hapa

na Mwandishi wetu

IMEBAINIKA kuwa mwenendo wa mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika mikutano na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni mkakati wa makusudi uliosukwa na watawala ili kukivuruga chama hicho, na kuwatisha wananchi kwamba ni chama cha fujo.

Hii si mara ya kwanza kwa watawala kufanya njama hizi dhidi ya wapinzani. Mara ya mwisho, waliofanyiwa hivyo ni Chama cha Wananchi (CUF), kilipokuwa chama kikuu cha upinzani.

Njama hizo zilikiangusha chama hicho, hadi kikajisalimisha kwa kufunga ndoa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, huku kikipoteza mvuto Tanzania Bara.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameliambia gazeti hili kuwa, CHADEMA inapaswa kuwa macho na njama hizi, kwani CCM imegundua kwamba inazidi kudhoofika na CHADEMA kinazidi kuimarika katika jamii; hivyo walio madarakani wanafanya kila njama kuua wapinzani ili wabaki madarakani.

Siku chache zilizopita, polisi walimuua kijana Ally Zona wakati wakitawanya waandamanaji wa CHADEMA mjini Morogoro. Jumapili iliyopita wameua mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, Daud Mwangosi, mkoani Iringa na kuleta sokomoko la kitaifa, ambalo limelichafua mno Jeshi la Polisi na Tanzania mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Utetezi wa polisi na jitihada zake kuwasingizia CHADEMA, waandishi na wananchi wengine kuwa ndio walifanya mauaji hayo, umegonga mwamba kwa sababu katika matukio yote haya, wapo mashahidi waliokuwapo pale pale.

Matukio haya yanatokea wakati ambapo vita ya kisiasa baina ya chama kilichoko madarakani na CHADEMA ikizidi kuongezeka kutokana na uungwaji mkono mkubwa unaopata chama hicho cha upinzani kwa sasa kuliko historia ya wakati mwingine wowote.

Kasi ya kukua kwa CHADEMA katika miaka ya karibuni inatishia madaraka ya watawala ambao wamekuwa madarakani kwa miaka ipatayo 50, na ambao chama chao, CCM, kimepoteza mvuto kwa umma, na hakiaminiki kutokana na kuzongwa na tuhuma nyingi za ufisadi, na kukumbatia makundi hasimu yanayotafuta madaraka na masilahi mengine, huku yakiendelea kudhoofisha uongozi wa CCM uliokwisha nyong’onyea.

Wakati CHADEMA kikipambana kukumbatia mapenzi ya umma unaokiunga mkono, huku kikifungua misingi na matawi vijijini, CCM inahaha kukidhibiti kwa propaganda na nguvu za polisi.

Kwa muda mrefu, CCM imejaribu kukipaka CHADEMA matope ya ukanda, ukabila na udini, kama ilivyofanya kwa CUF miaka ya nyuma; lakini baada ya kuona mbinu hizo zimeshindikana, sasa imeamua kutumia jeshi kutisha viongozi wake na wananchi kwa visingizo mbalimbali.

Hata hivyo, CHADEMA kinasema kimejiandaa vema kukabililiana na propaganda zote na vitisho vya watawala; na kwamba kimejifunza kwa makosa waliyofanya wengine katika NCCR-Mageuzi na CUF.

Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, anazo tafsiri tatu za matukio ya mauaji yanayofanywa na polisi katika mikutano ya CHADEMA.

Anasema: “Hawana majibu na matatizo ya wananchi, hawana majibu na tatizo la maji, elimu, matibabu ya uhakika na kero kadha wa kadha zinazowakabili wananchi. Kwa sababu hawana jibu, wanatumia nguvu. Sasa hawatumii vitisho tu, wanatumia nguvu.

“Hii ni taswira ya ‘system’ (mfumo) inayojua inaondoka. System imara haitumii nguvu, inatumia vitisho, kama kupeleka watu mahakamani. Sasa huko tumekwishapita, tumeingia katika hatua ya kuuawa.”

Tafsiri ya pili ya Lissu, ambayo ina uhusiano na ile ya kwanza, ni kwamba kwa vile watawala wanaona wako hatarini kuondoka, wanatafuta namna ya kuwachafua CHADEMA kwa wananchi ili wawaogope.

“Ikishindikana kutuchafua kwa propaganda wanaua. Wanaua watu kwenye mikutano na hadharani. Maana yake ni nini? Ni kwamba wanatuma ujumbe kwa jamii kwamba ukienda kwenye maandamano ya CHADEMA utakufa. Tafsiri yake ni kwamba watu waogope,” anasema Lissu.

Tafsiri yake ya tatu ni kwamba, watawala wanatengeneza mazingira ya kisiasa ili CHADEMA kionekane chama cha vurugu, ili utafutwe msingi wa kukifutia usajili.

“Ukishafanya mauaji kwenye mkutano unajenga mazingira ya kusema hiki chama hakina sifa, unamtengenezea mazingira msajili wa vyama vya siasa akiondoe…ukikiondoa CHADEMA maana yake umeondoa mgogoro na bungeni…utawaondoa akina Lissu, akina nani kule… Hivyo, nasema wanatafuta sababu ya kuendelea kutawala kupitia kuua raia,” anasema Lissu.

Anasisitiza kwamba kwa mantiki hiyo, Jeshi la Polisi limeacha kazi yao ya msingi ya kulinda raia na mali zao, na sasa limegeuka jeshi la kulinda walio madarakani ili waendelee kutawala.

“Jeshi limegeuzwa chombo cha ulinzi wa watawala. Hilo la kusema kwamba kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zao ni siasa, lakini the primary function (kazi yao ya msingi) ambayo hawaisemi ni hii ya kulinda watawala ili waendee kuwepo,” anasema Lissu.

Aidha, wachambuzi wanasema kinachotokea sasa ni kwamba watawala wanaanza kuhamanika, na wanaweza kutumia polisi kutenda mambo ambayo hatima yake itakuwa mbaya kwao, kama ilivyokuwa kwa watawala wa mataifa mengine waliofikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu, The Hague, Uholanzi.

Taratibu, kwa sababu ya matumizi mabaya ya Jeshi la Polisi, hata sifa ya Tanzania katika jamii ya kimataifa inaanza kuchafuka.

300466_3125930406832_1338529998_n.jpg


Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi baada ya kupigwa bomu

Mungu wabariki waTanzania, Mungu endelea kuwatia upofu watawala maana siku zao sasa zimebaki chache….!!

SOURCE TZ DAIMA


Waandishi wa Habari na Wanakijiji wakiwa wamebeba Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi kuelekea Makabirini




Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akiweka Shada la Mauwa kwenye Kaburi la Mume wake kwa machungu

Mke wa Daudi Mwangosi alishindwa kujizuia hapa akiwa amelala kwenye Kaburi la Mumewe akiwa analia kwa uchungu mwingi inasikitisha sana


Ni ngumu sana Kuamini kwa mke wa Marehemu lakini hali ndivyo ilivyo kuwa akiwa na huzuni kubwa

Watoto wa Marehemu wakiwa wanaweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Baba yao hawatamuona tena



Mbunge wa Jimbo la Rungwe na Waziri asiye na Wizara Maalum Mh. Prof. Mark Mwandosya akiweka Taji la maua pamoja na mkewe


Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Willboard Slaa akiweka Shada la Mauwa kwenye Kaburi la Marehemu



MHESHIMIWA RAIS ANGALIA PICHA HIZI MBILI, JE HUU SIO UDIKTETA HUU??

12.jpg

Septemba 2, 2012: Pichani JUU: CCM inafanya mkutano wahadhara huko Bububu, Zanzibar licha ya Serikali "kusitisha shughuli zote za kisiasa ili kupisha sensa ya watu na makazi."

Septemba 2, 2012 Pichani CHINI,mwandishi wa habari wa kituo cha TV cha Channel Ten,Daudi Mwangosi akipata kipigo kutokakwa FFU kwa "kosa" la kufanya coverage ya KIKAO CHA NDANI cha Chadema huko Nyololo,Iringa,ambacho Polisi sio tu walikizuwia kwa SABABU ZILEZILE ZILIZORUHUSU MKUTANO WA HADHARA JIMBONI BUBUBU bali walipiga,kujeruhi wananchi wasio na hatia na HATIMAYE KUMUUA mwandishi Daudi Mwangosi ."

966099517.JPG


Mheshimiwa Rais, damu za wananchi wasio na hatia wanaouawa na polisi kwa "kosa la kutumia haki zao za kikatiba za freedom of association" hazitapotea bure. Polisi waliua Arusha,lakini hiyo haikuzuwia wanachama na wapenzi wa Chadema kukusanyika Morogoro ambapo polisi waliua tena.Hata hivyo,kifo hicho hakikuwatisha wana-Chadema kukusanyika tawini kwao huko Nyololo ambapo baada ya unyanyasaji wa hali ya juu,polisiwaliua tena.



Hivi Mheshimiwa Rais hujifunzi kitu kutoka kwenye JEURI hii? Labda umesahau kuwa hata tawala dhalimu kabisa za kikomunisti huko Ulaya Mashariki zilijidanganya kuwa ukatili na unyama wavyombo vya dola utazidumisha (tawala hizo) milele,lakini wakati ulipofika zilisambaratika.Na huko Afrika ya Kusini,makaburu walitawala kwa mtutu wa bunduki lakini hawakuweza kuzuwia kuanguka kwa mfumo wa kibaguzi.



Mwanafalsafa Karl Marx aliwahi kuusia kuwa "mnyonge hana cha kupoteza zaidi ya minyororo." Wakati mafisadi wanaishi kwa hofu ya kunyang'anywa walichotupora, wanyonge wasio na uhakika na mloujao wanaishi kwa matumaini tu.Lakini kuishi huko kwa matumaini kunaweza kuwa silaha yenye nguvu kuliko vipigo,risasi na unyama wa FFU.



Watu wameichoka CCM na ni wazi kuwa vitisho na mauaji ya raia yasiyo na hatia hayawezi kushusha chuki hiyo.Sana sana inawaongezea tu sababu ya kukichukia chama hicho. 2015 si mbali.CCM inaweza kung'olewa madarakani.Ni vema,Mheshimiwa Rais,ukaanza kutafakari hatmayako pindi hao wanyonge wanaonyanyaswa sasa wakishika madaraka.



Watanzania wana kila sababu ya kuichukia CCM lakini inaonekana kana kwamba chama hicho kinasaka sababu nzito zaidi.Sijui ni kuishiwa na uwezo wa kuongoza au ndio kimezeeka na kinasaka namna ya kujipeleka kaburini,lakini kilicho wazi ni kuwa kila tone la damu linalomwagika kutokana na unyama wa polisi wetu ni sawa na lita nyingi za petroli kuchochea moto wa mabadiliko.




Source Mitandao:

Sincerely, DM


 
Back
Top Bottom