kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,344
- 17,584
Alikuwa anatafuta hela kwa madereva waliokuwa wanaenda Saba Saba jana kwa nguvu pale magomeni makutano ya Morogoro road na kawawa road huyu mwanadada mdogo na mwenye umbo dogo. Nilipita pale mida ya saa 6 mchana kuelekea Saba Saba, alichokuwa akifanya pale nikuongoza magari yeye badala ya taa za barabarani. Alikuwa akionyesha ishara ya kuruhusu magari kwa vipindi, dakika chache anaonyesha ishara na dakika chache anaacha ghafla kuonyesha ishara yoyote, watakopita taa nyekundu wakati yeye ameacha kuonyesha ishara yoyote atanyanyua mkono wake juu kuonyesha ishara ya kukusimamisha na kuweka gari pembeni. Mara nyingi atayasimamisha magari madogo na kuacha magari ya abiria hata kama utakuwa unafuatana na daladala au prado linalopita kwenye taa nyekundu kipindi hicho hicho. Hapo ataanza kukuomba umpe leseni kisha kukutishia kukupiga faini, ukimuuliza kwanini umeacha magari ya mbele tuliyopita nayo kwenye hiyo taa nyekundu anasema kwenye daladala wenye camera ni wengi wewe lete Saba Saba yangu la sivyo nikupige faini. Ukimuuliza kwanini hukuonyesha alama ya kusimama anakwambia kwani taa huzioni?
Tuheshimu nani zaidi kati ya polisi na taa?
Tuheshimu nani zaidi kati ya polisi na taa?