Polisi: Hakuna kuandaa disko vumbi sikukuu Mwanza

Polisi: Hakuna kuandaa disko vumbi sikukuu Mwanza

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
505
Reaction score
887
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewataka wananchi kuchukua tahadhari za kiusalama katika kipindi hiki cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya huku likiwataka kuondoa hofu kutokana na Jeshi hilo kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya Jiji la Mwanza.

Yamesemwa hayo leo Disemba 24, 2025 na Jeshi hilo katika ofisi za kituo kikuu cha polisi kilichopo Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza ambapo limewataka wakazi wa Mwanza kusherehekea sikukuu hizo kwa amani na usalama ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani

Akizungumza, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wamiliki wa kumbi za starehe kuchukua tahadhari za kiusalama kwa mujibu wa kanuni na taratibu zinazowaongoza ikiwa ni pamoja na kutoendesha miziki ya watoto (disko vumbi)

"Nipende kuwakumbusha wamiliki wa kumbi za starehe kuhakikisha kuwa wanachukua tahadhari zote za kiusalama kwa majibu wa leseni zao za kibiashara na hakuna kuandaa au kuendesha mambo ya miziki ya watoto maarufu disko vumbi" amesema Wilbrod Mutafungwa
 
Back
Top Bottom