PostGE2025 Polisi: Gwajima, Golugwa, Brenda Rupia, Lema, Mahinyila na Mnyika wajisalimishe katika vituo vya Polisi

PostGE2025 Polisi: Gwajima, Golugwa, Brenda Rupia, Lema, Mahinyila na Mnyika wajisalimishe katika vituo vya Polisi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Wakuu,

Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa kuhusu operesheni inayoendelea ya kuwasaka watu waliopanga na kutekeleza vitendo vya uhalifu, uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali za umma kufuatia matukio yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025 katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya waliopanga matukio hayo tayari wamekamatwa na kufikishwa mahakamani, huku msako mkali ukiendelea kwa wengine. Polisi imetaja majina ya watu wanaotafutwa kuwa ni:
  1. Josephat Gwajima
  2. Brenda Jonas Rupia
  3. John Mnyika
  4. Godbless Jonathan Lema
  5. Machumu Maximillian Kadutu
  6. Deogratius Cosmas Mahinyila
  7. Boniface Jacob
  8. Hilda Newton
  9. Award Kalonga
  10. Amaan Golugwa
Jeshi la Polisi limewataka wote wanaotajwa kujisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyo karibu, na limeonya kuwa mtu au kikundi chochote kitakachopanga au kutekeleza uhalifu hakitasita kuchukuliwa hatua za kisheria.

photo_2025-11-08_00-47-50.jpg

photo_2025-11-08_00-47-53.jpg
photo_2025-11-08_00-47-55.jpg
 
Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa kwa Umma wa Watanzania kuwa, kufuatia matukio ya vurugu, uporaji wa mali na uvunjifu wa amani yaliyotokea tarehe 29/10/2025 katika Majiji ya Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya, pia katika Mikoa ya Shinyanga, Geita, Songwe, Ruvuma, Mara,Dodoma, Kilimanjaro na Iringa na kusababisha madhara kwa binadanu, kuharibu mali nyingi za umma na za watu binafsi kulileta athari kubwa.
20251108_004743.jpg

20251108_004744.jpg
 
View attachment 3498833

View attachment 3498834
Wachawi wanatafuta mchawi nje ya club ya wachawi.
 
Godbless Lema alivyokua muoga itakua kashafika Namanga anavuka border kwa njia za panya , ila mitandaoni mikwara kibao na kudanganya Nyumbu zitoke kuandamana huku yeye hatokei hata mara moja barabarani maana anapenda kuishi kuliko kufa
 
GenZ ngoja waitishe maadamano ya kudai wenzao walioshikiliwa na kupewa kesi za Uhaini uone kama serikali aijatema ndoano wakiandaa maandamano ya Kushinikiza Wenzao kuachiwa serikali itakua imejitafutia matatizo bure
 
Back
Top Bottom