Polisi Dar yapiga marufuku uchomaji matairi Barabarani kuelekea sikukuu ya mwaka mpya

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa tahadhari kali kwa wananchi dhidi ya vitendo vya kuchoma matairi barabarani pamoja na kupiga baruti au fataki katika maeneo yasiyoidhinishwa, likisisitiza kuwa watakaobainika kufanya vitendo hivyo katika kipindi cha sherehe za Mwaka Mpya watachukuliwa hatua za kisheria mara moja.

Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 31, 2025, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesema Jeshi la Polisi lina jukumu la kuzuia na kudhibiti vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya Mwaka Mpya, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Amesisitiza kuwa hatua zitachukuliwa kwa haraka kwa mtu au kikundi chochote kitakachobainika kukiuka marufuku hiyo, huku Jeshi la Polisi likizingatia misingi na taratibu zote za kisheria katika utekelezaji wa majukumu yake.

Aidha, amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kushirikiana kwa karibu na wananchi pamoja na viongozi wa nyumba za ibada ili kuhakikisha shughuli zote za ibada zinafanyika katika mazingira salama kipindi cha sikukuu.

Kamanda Muliro pia amewakumbusha wananchi kuhakikisha makazi yao, ofisi na maeneo ya biashara hayabaki wazi bila uangalizi, hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na nyakati nyingine za shughuli za kijamii na kiuchumi.
 
Mimi napenda CCM. CCM OYEEEE
 
Watu wamepiga baruti kwa sana tu... Mpaka sasa wamekamatwa wangapi...

Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom