Polisi Chang'ombe wameanza kuuza "hisa"? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Chang'ombe wameanza kuuza "hisa"?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by malimwengu, Mar 28, 2012.

 1. m

  malimwengu Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika hali ya kushangaza polisi kituo cha Chang'ombe wameanza kuuza hisa kwa wahalifu ili nao wawe sehemu ya jeshi hilo.

  Hii iko hivi, kuna watu wanatengeneza document feki za kuibia mizigo bandarini na kwenye ma godown mbalimbali. Wakifanya dili hii polisi huabarishwa lakini polisi humuachia mwenye mali. Akishtuka polisi hufanya nae kazi na kuwakamata wahalifu, huchukua pesa kutoka kwa mwenye mali na huchukua pesa kutoka kwa wahalifu na kuwaachia, wote waliowahi kukamatwa na kutoa pesa wameachiwa. Hivi karibuni kuna watu wamekodi gari na kubandika namba bandia kwenda kuiba mzigo, mwenye mali akashtuliwa, akawashtua polisi, jamaa wamekatwa na gari limekamatwa cha kushangaza mwenye gari hajakamatwa bali yupo uraiani ameambiwa atafute milioni tano waweze kumrudishia gari lake na pia akitaka kufanya shughuli zake hizo awaarifu kwanza polisi. Hii dili inapigwa na mtu ambaye namba za gari lake zilitumika anayejulikana kwa jina la Massawe anayeishi Arusha pamoja na OCS CID Chang'ombe.

  Jamaa sasa anatafuta hizo milioni tano na ameshaanza kuchangisha ndugu zake ili kununua hisa za kushirikiana na polisi katika uhalifu.

  Kumbe kazi ya jeshi la polisi sasa imebadilika kutoka kuwa usalama wa raia na mali zao mpaka kuwa uhakika wa majambazi na kazi zao. Mungu libariki sana jeshi la polisi
   
 2. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mh! Hivi kuna ukweli hapa? Kama ni kweli basi jeshi letu la polisi limeingiwa na kansa ya ajabu sana. Usalama wa taifa fanyeni kazi yenu kwa makini katika hili. Kweli taifa linawahitaji sana kuliko ccm inavyowahitaji.
   
 3. P

  Peter Nyanje Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa askariw a Chang'ombe kufanya hivi mimi wala hainishangazi, pale wapo kibiashara zaidi
   
 4. c

  collezione JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Haha, hiyo ndo Tanzania zaidi unavyoijua.

  Ila mimi nasema kila siku, na nitarudia kusema. Kuandika Jamii forum hapa haitoshi.

  Tunatakiwa tuwe na chombo cha habari kisicho_chakachua habari... Mambo kama haya yawekwe hadharani (iTV na TBC hawawezi leta hii habari)...

  Kuna siku hawa watawala wetu wataona hii Tanzania ni chungu...tumechoka manyanyaso wakati uko kwenu. Let's wait time will tell
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Kwani si ndio kituo hiki ambacho mjane alikwenda kuripoti kesi na tajiri ya marehemu mumewe afisa mmoja wa kike akaungana na mshatakiwa kufuta message kwenye simu ya mlalamikaji!
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  i am speechless.........
   
 7. Matango

  Matango JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sasa tunataka kuona polisi anamkamata polisi !!
   
 8. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ushauri tuanzishe kituo chetu cha Redio
  JF REDIO
  kazi yake kubwa itakuwa ni kutoa habari kama hizi pasi kutiwa chumvi
   
 9. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  exactly
   
 10. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Hapa Mwanza kuna polisi hatari, wanavaa kiraia na kutumia gari lenye namba za kawaida, zamani wakifahamika kama TZR, ukikamatwa na hiyo mibaunsa usalama wako ni usiwe na pesa kama una japo mil.1 tu umekwisha.
  Sasa hivi wanatumia defender ya rangi ya kitani yenye namba T 516 BJU. Hao jamaa nao ni sehemu ya ujambazi.
  Tanzania hatuna polisi kabisa.
   
Loading...