Polisi Arusha waingia lawamani part 3

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
180
POLISI ARUSHA WAINGIA LAWAMANI PART 3

Mwandishi wetu,

Mpendwa mwana jukwaa kama kawaida juzi nilihaidi kuwaletea kwa mfululizo lile sakata la jeshi la polisi mkoani Arusha kukataa kutii amri halali iliyotolewa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (DPP) mkoani Arusha iliyoagiza wakili wa mfanyabiashara MATHEW MOLLEL na mkurugenzi wa kampuni ya utalii,RAIMBOW TOURS & SHUTTLE aitwaye DUNCAN OOLA akachukue hatimiliki ya mteja wake mbele ya polisi baada ya kuona hakuna sababu ya wao kuendelea kuishikilia hatimiliki hiyo.

Polisi hadi sasa wamegoma kutoa hatimiliki hiyo wanampiga danadana bwana MOLLEL kwa kuwa inasemekana kuna kigogo ndani ya ofisi yua RCO ARUSHA anahitaji kiasi cha sh,milioni 2 ili amkabidhi na mfanyabiashara huyo amegoma kutoa pesa hizo kwa kuwa haoni sababu na hatimiliki ni haki yake .

Lakini mtakumbuka katika part 2 nilihaidi kuwajuza taarifa za mtu aitwaye MOSES KING”ORI ambaye anatajwa kulimezea mate eneo la bwana MOLLEL.

HUYU MOSES KING”ORI JE NI NANI?

Huyu anafanya kazi katika kampuni ya RIVERSIDE SHUTTLE iliyopo eneo la METROPOLE jijini ARUSHA.ameajiriwa na mama ZAINAB KARAMA ambaye anaishi naye haieleweki kama wameoana au la lakini ni mama mfanyabiahsara mkubwa tu na mmiliki wa KARAMA LODGES ARUSHA kama mtakumbuka aliwahi kuwa mpambe wa karibu wa DK BATILDA BURIANI wakati akigombea ubunge wa jimbo la ARUSHA MJINI.

Chanzo cha ugomvi baina ya MOLLEL na KING”ORI ni kwamba miaka ya nyuma bwana MOLLEL kabla hajafungua kampuni yake alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya RIVERSIDE kwa zaidi ya miaka 9 na ushee na alipotaka kuondoka ndipo dalili za chuki binafsi zikaanza ghafla.

MOSES alianza visa na mikasa na pamoja na MOLLEL kuiingizia faida kampuni hiyo lakini alijikuta akiondoka kwa ugomvi na ndipo walipomdhulumu basi 5 aina ya coaster lakini aliamua kuwaachia ili akatafute maisha yake mengine kwa kufungua kampuni yake binafsi ambayo kwa sasa inafanya vizuri sana katika soko la utalii ARUSHA .

Chuki ya MOSES iliendelea kubaki hadi leo na ndipo aliposikia tukio la MAKANGA mara alipokuja ARUSHA mwaka 2014 ndipo akamtangazia dau kwamba atampatia milioni 200 endapo akiuziwa kiwanja hicho lakini inasemekana dau hilo lilitolewa na MAMA ZAINAB KARAMA baada ya kumshawishi kwa kuwa MOSES hana uwezo wa kupata kiasi hicho cha fedha na inadaiwa amewekwa na MAMA huyo hapo RIVERSIDE .

Taarifa zilizopo nyuma ya pazia ni kwamba MOSES ndiye aliyekuwa akifadhili gharama za kesi ya jinai iliyofunguliwa MAHAKAMA YA WILAYA YA SEKEI na kesi nyingine iliyofunguliwa BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA MKOANI ARUSHA ambazo zote bwana MOLLEL mwisho wa siku alishinda.

K wa sasa tunavyoongea kuna taarifa kwamba inasemekana kampuni ya RIVERSIDE SHUTTLE inayumba kibiashara kutokana na usimamizi mabovu na matumizi mabaya ya fedha lakini pia kuna taarifa kwamba aliyekuwa akitoa fedha kufadhili kesi ni MAMA ZAINAB KARAMA na kwa sasa amegoma kuendelea kutoa fedha maana amebaini anadanganywa na bwana yake na anaona kiwanja cha bwana MOLLEL kimekwama kwani inasemekana amekuwa akitoa pesa nyingi tangu mwaka 2014 bila faida yoyote .

USIKOSE EPISODE 4

Katika episode ya 4 tutamwangazia mtu mmoja aitwaye KIJJA SHIJA huyu ni mtu wa karibu na DAHNI MAKANGA ndiye mpambe wake hapa jijini ARUSHA na amekuwa akimwakilisha mahakamani mara kwa mara je na hata wakati MAKANGA akienda kusaka hati nyumbani na ofisini kwa bwana MOLLEL alikuwa bega kwa bega,SHIJJA inadaiwa kwamba ndiye amekuwa akitumia pesa na MOSES KING”ORI za MAMA ZAINAB KARAMA kwa kumdanganya je ni nani huyu?je ana maslahi gani katika sakata hili usikose mtu wangu wa nguvu.

(PICHANI CHINI NDIYO ILE BARUA YA DPP ARUSHA KWENDA POLISI)

BARUA YA DPP.jpg
 
Ningefurahi kuona maelezo yanayotoa "facts" lakini bahati mbaya maelezo mengi yanatoa "feelings" inakuwa ni vigumu kuhukumu mtu kwa "hisia" na story imeandikwa upande mmoja tu je umeshaonana na wahusika ukawauliza kwa mfano polisi kwamba kwanini wanaendelea kushikilia hati hiyo? mbali na barua ya mahakama pengine kuna maelekezo toka ngazi za juu.Polisi hufanya kazi kwa utaratibu na si vinginevyo.Hutendi haki pale ambapo hujauliza upande wa pili kuthibitisha kilichosemwa ni kweli au la.Nadhani usiegemee kwa maelezo ya Mollel pekee nenda kwa wahusika waulize na kama hukuweza kuwahoji usitumie maneno ya Mollel kujaza nafasi ya mazungumzo yao na ndio maana nasema yaliyoandikwa ni hisia nyingi dhidi ya watu wengine, hisia hizo mwisho wa siku hazitajenga mahusiano mema.Mfano umemwandika king'ori vibaya mahusiano yake na mapenzi au mke hapa yanahushu nini ?

-Barua ya mwanashaeria inaonyesha apewe hati lakini bado imeonyesha kuna haja ya kufunguliwa kesi ya madai maana yake kuna tatizo hapo.na hii haimainishi asipewe hati.Lakini kuna uwalakini hapo.sasa vilevile muulize wakili wa serikali kwanini Makanga anshauriwa afungue kesi ya madai ? wao wanasheria wameona nini mpaka kutoa ushauri huo?Hali kadhalika nenda kwa polisi waulize kwa nini wanaendelea kushikilia hati hiyo? wakati ambapo kesi imekwisha? (Maelezo toka pande mbili hizi yatasaidia kupata upanana uelewa wa mabo jinsi yalivyo).

-Vilevile muhtasari unaodaiwa kughushiwa uwekwe hapa hadharani kama ilivyoweka barua ya mwanasheria ili tuweze kuona na kutoa maoni.Vilevile kama kuna orodha ya watu kwenye muhtasari basi nao wahojiwe wathibitishe wanautambua muhtasari na majina na sahihi ni za kwao na si vinginevyo.Ukifanya hayo haki itandeka na sisi wasomaji tutapata picha kamili.
 
Back
Top Bottom