Polisi anatafutwa na Jeshi la Polisi baada ya kugundulika alijipata ajira kwa vyeti vya kugushi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Zoezi la kuhakiki watumishi hewa lililoamriwa na Rais John Magufuli limemkumba Askari Polisi aliyeajiriwa mwaka 2003 baada ya kubainika kuwa ametumia vyeti vya kugushi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amemtaja Askari huyo kuwa ni Emanuel Nikolas Nyangoli mwenye namba F5425 Pc ambaye baada ya kutuhumiwa kuwa na vyeti vya kughushi aliamua kutoroka na hajulikani aliko.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amesema Askari Emanuel Nyangol amefanya kazi ndani ya jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 13 bila kujulikana kuwa ana vyeti vya kugushi,

Vielelezo vya kuonyesha jeshi la polisi lina taarifa kuwa uajiriwa wa askari huyo ni wakutatanisha ndio ulio mfanya atoroke baada ya kujua jeshi la polisi lina taka kumfungulia mashitaka
 
Inshu ilikuwa ni watumishi hewa, hili la vyeti feki nalo ni jipu zaidi kwani wapo wengi zaidi ya watumishi hewa
 
miaka 13 ndio wanajua leo... ila sina uhakika na masijala ya polisi kama wanaweza wakawa na taarifa za mandata wote labda itoke amri kila mtu aje na vyeti halisi then kiwepo kijimashine kutoka NECTA cha kudetect kama ni orijino au fekelo hapo ikiwa hivyo hata tigo wataanza kupakia abiria (ila haiwezekani maana ujambazi utazidi)
 
Kama vipi zoezi la kuhakiki vyeti lianzishwe na lifanyike idara zote nchi nzima
 
aina maana yoyote watu wameshajua mengi kwani vyeti ni kitu gani mbona vipo vingi used tu kitaani
 
Jeshi la polisi ndilo ambalo linaongoza kwa watumishi wake kugushi vyeti .walimu wanafuatia .hivyo watumishi hewa bado wapo tena wengi tu.kuna watumishi hewa unakuta alishakufa siku nyingi,ila bado anadaka mpunga.kuna waliofukuzwa ila bado akaunt zinaingiziwa bila ya wao kujijua.kuna wastaafu bado mshahara unakuja woote.kumbuka kuwa mpaka stahiki zote alizokuwa analipwa mtumishi hewa zimelipwa.kwa hiyo wakurugenzi nk wanayajua haya yoote na wao ndoo wanakula pesa hizi.dhana ya watumishi hewa ni pana sana.
 
Maskini ya Mungu said bagaile na lameck madelu watatumbuliwaaa hawa marafiki zangu,

eeeeeeee MUNGU EPUSHIA BALI HILI BALAA LA VYETI!
 
miaka 13 ndio wanajua leo... ila sina uhakika na masijala ya polisi kama wanaweza wakawa na taarifa za mandata wote labda itoke amri kila mtu aje na vyeti halisi then kiwepo kijimashine kutoka NECTA cha kudetect kama ni orijino au fekelo hapo ikiwa hivyo hata tigo wataanza kupakia abiria (ila haiwezekani maana ujambazi utazidi)
Ujambazi wao labda wawafanyie polisi wenzao, kuna wanajeshi wanaachishwa kazi na hakuna cha hofu ya ujambazi wala nini sembuse polisi!
 
Huo ni udanganyifu kwenye taaluma, ukipiga msako mkali utaona kuna waliofoji uraia ili kuajiriwa serikalini.
 
Back
Top Bottom