Mi naona kama wanawapima imani tu...Sasa wakikutana na mtu aliyekataa rushwa ya 50ml watampa ngapi?? Naona mambo mengine ni kujifunga vitanzi tu. Mi nadhani suala kubwa hapa walitakiwa kuboresha mazingira ya kazi ya polisi kama vile mishahara, marupurupu, makazi na huduma nyinginezo. Mbona JWTZ wanawekwa vizuri tu kulinganisha na hawa Polisi wetu??! UKienda pale lugalo kwenye super market ya jeshi vitu viko bei chini ajabu kulinganisha na mtaani, acha dula lao lingine pale kambi ya Twalipo achilia mbali bia, sigara na vinywaji vingine ambavyo bei zake ziko chini sana. Sijui kwanini isiwe na polisi nao.