Nilikuwa safarini Sumbawanga na Mpanda,nilipofika Mpanda nikahamua kwenda CRDB kuchukua vijisenti kabla ya kuendelea na safari Tabora.CRDB Tawi la Mpanda ni kati ya Majengo mapya ya kisasa kabisa,nilishangaa kukuta Kibanda cha walinzi hapo gaitini kikiwa kimeungua moto,ni kibanda kipya kabisa kilichojengwa kisasa lakini tayari kimeungua moto,nilipouliza wadau wakaniambia kuwa polisi mmoja mvuta bhangi alidondosha kipisi kwenye godoro kisha yeye na mwenzake wakatoka nje ya lindo kwenda kutafuta wanawake kurudi walikuta Kibanda kinateketea,kwa kweli inasikitisha sana,inabidi polisi wachukue hatua za maksudi kuthibiti ongezeko la polisi wapya ambao asilimia kubwa ni wavuta bhangi,inatia aibu unapokutana na polisi in uniform amekaa kijiweni anapuliza ya Arusha,ikibidi katika vipimo kabla ya kwenda CCP wongeze kipimo cha damu kama mtu ni mtumiaji wa banghi au drugs,vinginevyo tunakoelekea ni kubaya sana.Naomba kuwasilisha wakuu