Polisi acheni kubambika watu kesi

R Mbuna

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
2,295
Reaction score
5,458
Habari za wakati huu wana jukwaa.

Hii habari imenisikitisha sana na imenikera sana kwa jinsi polisi wanavyolazimisha kuwapa watu makosa ili hali ni raia mwema tu.

Niende kwenye mkasa ambao umepelekea kuleta hili bandiko humu jukwaani, kuna kijana anauza duka huko maeneo ya Mbagala sasa juzi siku ya Jumapili mida ya saa mbili usiku alikuwa ameenda kupunguza nywele baada ya kuona zimekuwa ndefu kichwani kwake.

Kabla hajafika eneo la saluni alikutana na polisi njiani wakamwambia kwa nini anazurura usiku, yeye akajieleza kuwa anaenda kupunguza nywele na hakai mbali na pale walipomkuta polisi. Hivyo polisi wale ambao walikuwa na gari yao ya doria wakamwambia leo utaenda kulala ndani kesho utaenda mahakamani kwa sababu ya uzururaji.

Bahati nzuri kuna watu walimuona wakati anakamatwa na kila mtu alishangaa jinsi ya ukamataji ule kwa sababu ni kijana ambaye ni mtaratibu sana na wala hana kawaida ya kukaa vijiweni yeye kutwa anashinda kwenye duka lake tu.

Kijana mwenyewe masikini ya Mungu ni mlokole hata hiyo sigara katika maisha yake hajawahi kuvuta analia mpaka anatia huruma. Ameniambia kaka kama wamenifungulia hiyo kesi waambie wakanipime mkojo ili wajiridhishe kama katika maisha yangu nimeshawahi kutumia kilevi cha aina yoyote.

Wanalazimisha wapewe hongo hawa jamaa sio watu wazuri ndio maana wananchi hawatoi ushirikiano kwa hii taasisi ya serikali kwa sababu wakati mwingine huwa wananyanyasa raia bila sababu za msingi.

Tunaomba waziri mwenye dhamana aangalie sana hii idara yake ya polisi hii sio poa kabisa.
 
Wana njaa sana siku hizi

Zaidi ya 24hrs mtu yupo mahabusu hawajampeleka mahakamani wanasubiri mlungula tu na kijana amesema yeye hatoi kitu kama vipi wampeleke tu mahakamani.

Leo nimeacha kuna jirani zetu wanamfuatilia waone kama kuna jinsi ya kumsaidia ili atoke.
 
Polisi hii tabia sijui wataacha lini.

Ndio maana raia wanawachukia sana hawa jamaa.
 
Inasikitisha sana hao mara nyingi huwa ni waonezi huwa wanajifanya wanapiga doria kumbe wanatafuta hela ya pombe hata wakikuta unajirudia kwako umechelewa mida ya usiku watakutikisa hadi uwatoe chochote.

-Ndumilakuwili-
 
hao ndiyo polisi wa Tanzania mkuu. awaambie wampeleke mahakamani Kule ataenda Toka kirahisi tu
 
Punguza hasira, ulokole wa jirani yako ni ww unayeutambua!!! Si kila askari atatambua huyu ni mlokole.
Yawezekana eneo lenu ni sumbufu kwa vibaka,wezi na wavuta bhangi na mmoja wa wananchi wa eneo hilo katoa taarifa na huyo mlokole akitajwa kuwa ni mmoja wa wakola ktk eneo hilo.
Polisi imetekeleza kwa kukamata na kuhoji mpaka hapo itakapojiridhisha. Mtoa taarifa anafurahi taarifa yake kufanyiwa kazi na mlengwa wake (mlokole) kuwa ndani jirani analalamika na kusema polisi waonevu na wala rushwa na hata mlokole atakapotoka mtoa taarifa atasema polisi rushwa tu tunawapa taarifa hawazifanyii kazi wanakamata na kuchukua rushwa tu.
Ndo maana nawachukia siwapi taarifa.jamani hao ndo polisi hawawezi kupendwa ni ADUIRAFIKI akikusaidia rafiki akikuminya adui maisha yanasonga.
Tukumbuke Polisi wanangazi zao ukiwa kituoni muone in charge wao palipo na dosari zozote husizozikubali lengo tuikwepe KIBITI.
 
Waacheni police wapige kazi yao bhana, kumkamata mtu mdhurulaji.. Eti kisa mpole ndy iwe sababu ya police waache kufanya kz yao.!! Hata hyo rushwa umesema ww, police wa sasa wanafanya kz kiweledi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…