Police Post Keko Magurumbasi, faini za pikipiki mnazokamata zinaingia serikalini?

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,217
Habarini zenu wadau kwa ujumla.

Leo nimekuja na hili moja tu,ambalo najua huenda kuna sehemu nyengine linafanyika.

Kituo cha polisi keko magurumbazi ambacho kwa muda sasa kimekua kikifungwa na siku zingine kufunguliwa sasa hivi kimegeuka kijiwa cha sungu sungu wasioeleweka wakishirikiana na askari wa kituo hicho kuanzia saa moja jioni hukamata piki piki zinazopita barabara ya chang'ombe na kuzijaza pale,cha ajabu kabisa na kushangaza pikipiki hizo ukipita saa sita hukuti hata mmoja,

mtoa taarifa wangu amesema mradi huo unafanywa na askari shirikishi ambao mchana huwa hawaonekani lakini ikifika usiku kuanzia saa moja huja pale na kukamata pikipiki kisha kuwatoza pesa kuanzia 30000 na kuendelea kisha pesa hizo huwekwa mifukoni mwao.

wanapomaliza kazi hiyo hugawana ujira huo na kufunga kituo mpka kesho yake tena.

Naomba kumuuliza kamanda wa mkoa je unayajua haya?

ukipita hata muda utazikuta pikipiki hapo.kibaya zaidi hawana hata mashine za malipo.

je huu ndio utaifa na uzalendo kwa nchi.

SITA TAJA MAJINA HAYO.KWA SABABU MPAKA KITUO CHA KIKUBWA CHA CHANG'ombe wanajua hili.
 
Ukilipa faini sehemu yoyote ya serikali ni lazima upewe risiti ya serikal ,zinakua za rangi ya khaki kalii.. Au unapewa kile cheti cha makosa ya usalama barabarani au kile kirisit cha efd za trafik.. Vinginevyo baba umeliwaaaaaaaa...
 
usiseme nimeliwa,watu wanaiibia nchi unasema nimeliwa,nimewapa taarifa hiyo wahusika waifanyie kazi ki intelligence watabaini hayo yanayo fanyika.
 
usiseme nimeliwa,watu wanaiibia nchi unasema nimeliwa,nimewapa taarifa hiyo wahusika waifanyie kazi ki intelligence watabaini hayo yanayo fanyika.
Ndugu mwana jf ckua na maana kua ww ndo umeliwa hela.. Hio post yangu nilikua najaribu kuelezea jins gan mtu ukilipa hela kwa makosa ya pkpk/gar unavotakiwa kupewa uthibitishl wa malipo yako.
Pia nilipenda kuwajulisha wana jf wenzetu mfumo wa malipo polisi ulivyo.
Na hayo yote nimeandika kutokana na experience yangu katika matukio ya kulipa faini.

Kama nimekukwaza naomba tusameheane.. TUPO PAMOJA MKUU..
 
Back
Top Bottom