"Police loss report" isiwe jambo la lazima

wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
3,984
4,131
Salam ndugu,

Kuna huu ukasumba kila unapopoteza kitu ama nyaraka basi ni lazima ulipoti polisi na upewe barua.

Hapa nitazungumzia upande wa vitambulisho, mfano chuo, NHIF, kadi ya benki n.k

Sasa mimi kama" id holder" naripoti kwako id issuer" kuwa nimepoteza kadi yangu ya utambulisho,hunipi huduma eti hadi niende polisi.

Sasa kati ya polisi na wewe mtoa kadi nani anazotaarifa zangu?

Maana chochote kitachotokea,mwenye kitambulisho atahusika.

Binafsi naona huu ukiritimba uondoke tu maana unapoteza muda kwenye kupata huduma.

Ibakie uamuzi wa muhusika kama anaona inampendeza kuripoti polisi.
 
Kuna makampuni ya simu ukipoteza sim card ukaenda kuripoti kwao moja kwa moja wanakusaidia haraka japo watauliza loss report ya polisi, kwenda polisi kisha kwa mtoa huduma ni kupoteza fedha na muda mwingi wakati zaidi wenye sim card wanazo taarifa halisi za mteja wao
 
Fikiria kuwa umedondosha kitambulisho chako cha chuo na kikaokotwa na mtu, mtu huyo akaenda kushiriki tukio la kihalifu kubwa sana na akakidondosha pale. Unafikiri nini kitatokea kama sio wewe kukamatwa na upelelezi kuanza na wewe?
Vitu vingine tunaona vya kawaida lakini likitokea la kutokea ndiyo utaona umuhimu wake.
 
Nikikidondosha mimi eneo la tukio nikikimbia?
 
Hata hii ya online bado ni tatizo kwako mtoa mada?
Katika hili polisi wamejitahidi kupunguza mlolongo, ni vile watu hatuelewi.

Huyo issuer wa ID yako yeye atatakiwa kukupa barua ya kukutambua tu kama ni mteja na wakati mwingine itahitajika hiyo barua kuthibitisha umepoteza hicho kitu kweli.
 
Hii ya online lazima tena uende kituoni ili ithibitishwe ndipo itoke.
 
Salam ndugu,

Kuna huu ukasumba kila unapopoteza kitu ama nyaraka basi ni lazima ulipoti polisi na upewe barua.

Hapa nitazungumzia upande wa vitambulisho, mfano chuo, NHIF, kadi ya benki n.k

Sasa mimi kama" id holder" naripoti kwako id issuer" kuwa nimepoteza kadi yangu ya utambulisho,hunipi huduma eti hadi niende polisi.

Sasa kati ya polisi na wewe mtoa kadi nani anazotaarifa zangu?

Maana chochote kitachotokea,mwenye kitambulisho atahusika.

Binafsi naona huu ukiritimba uondoke tu maana unapoteza muda kwenye kupata huduma.

Ibakie uamuzi wa muhusika kama anaona inampendeza kuripoti polisi.

Inatakiwa pesa kwa jina la mapato ya serikali
 
police loss report ni jambo la msingi, tatizo police wa Tanzania siyo weledi, wanawaza rushwa sana, mfano hii ni week nafuatilia loss report, ukienda ili wahakiki malipo niweze kuprint watakuambia mhusika hayupo!
 
Nilipoteza vyeti vyangu vyote vya shule, nikaambiwa niende polisi nipewe loss report, halafu mahakamani , na mwisho wizarani nipewe vingine. Nilienda mara 4 polisi oysterbay bila mafanikio, kila nikienda mtandao hauko sawa
 
Fikiria kuwa umedondosha kitambulisho chako cha chuo na kikaokotwa na mtu, mtu huyo akaenda kushiriki tukio la kihalifu kubwa sana na akakidondosha pale. Unafikiri nini kitatokea kama sio wewe kukamatwa na upelelezi kuanza na wewe?
Vitu vingine tunaona vya kawaida lakini likitokea la kutokea ndiyo utaona umuhimu wake.

Kwahiyo hiyo report itakuokoa kwa kipi hapo wakati umelipia tu 500 online
 
Fikiria kuwa umedondosha kitambulisho chako cha chuo na kikaokotwa na mtu, mtu huyo akaenda kushiriki tukio la kihalifu kubwa sana na akakidondosha pale. Unafikiri nini kitatokea kama sio wewe kukamatwa na upelelezi kuanza na wewe?
Vitu vingine tunaona vya kawaida lakini likitokea la kutokea ndiyo utaona umuhimu wake.
Mtu alidondosha plate no ya bodaboda.
Kaenda kutoa taarifa polisi ili apate police report.
Ajabu alipofika kituoni akaambiwa arudi jumatatu.
Hiyo ni jumamosi.
 
Nilipoteza vyeti vyangu vyote vya shule, nikaambiwa niende polisi nipewe loss report, halafu mahakamani , na mwisho wizarani nipewe vingine. Nilienda mara 4 polisi oysterbay bila mafanikio, kila nikienda mtandao hauko sawa
Mkuu vyeti ulifanikiwa kupewa vingine ? Nimepoteza pia sijui pa kuanzia ! Mchakato ukoje ?
 
Nilipoteza vyeti vyangu vyote vya shule, nikaambiwa niende polisi nipewe loss report, halafu mahakamani , na mwisho wizarani nipewe vingine. Nilienda mara 4 polisi oysterbay bila mafanikio, kila nikienda mtandao hauko sawa
Hivi vyeti vya shule huwa vinapoteaga vipi? Kwamba unatembea navyo kama simu au wallet, huwa nashangaa mtu anasema amepoteza vyeti vyote vya shule
 
Vp nikifanya uhalifu kisha nikadondosha kitambulisho changu hapo halafu nikaenda kuripoti upotevu?
Vigezo vya kumuhusisha (au kutomhusisha) mtu na tukio la uhalifu viko vingi,kitambulisho kilichopatikana eneo la tukio ni mojawapo. Ila hila ya mtu kukidondosha (baada ya kufanya tukio) na kuwahi kwenda kuripoti kituoni nayo haiwezi kukugarantee kuwa wewe hujahusika.Unaweza kutwishwa mzigo wa kuthibitisha kwa ushahidi kwamba muda wa tukio hukuwepo eneo la tukio.Kifupi defence of ALIBI itakuhusu.
 
Back
Top Bottom