Polepole: Tatizo la CCM ni Unafiki uliopitiliza!

Polepole: Tatizo la CCM ni Unafiki uliopitiliza!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,600
Je, katika hili Komredi Polepole yuko sahihi au amebwabwaja tu?

Mlale unono 🙏
 
Hilo tatizo sio la ccm tu bali karibu vyama na wanasiasa wote, Polepole yupo tofauti sana na wanaisa maslahi ambao wapo kwenye vyama vyote likija jambo linalohusu maslahi yao wapo pamoja.
 
Unataka tulale unono wakati nyie ccm hamlali mnaikula nchi usiku mzima?

Mnaipiga nchi mbele na nyuma bila haya
 
Polepole ni mnafiki tu, hana lolote, ana chuki binafsi na Mh. Rais wetu Mama Samia
 
Tatizo la unafiki liko kila sekta na kila nyanja. Ni hulka ya watanzania wote.

Hata Polepole ni mnafiki pia;-
1. Lisu alipigwa risasi wakati huo Polepole akiwa kwenye viete kama mwenezi. Ulimsikia akisema?
2. Polepole aliendesha kampeni ya iuwanunua wabunge wa upinzani, maarufu kama kuunga juhudi. Mhuni Polepole aliona sawa tu
3. Magufuli alijaza nduguze na watoto wa dadake kwenye nafasi nyeti. Ulimsikia akilalama?
4. Watu walikuwa na kuokotwa kwenye viroba ktk fukwe za bahari, ulimsikia Polepole akisema??
5. Watumishi walinyimwa nyongeza ya mishahara kwa miaka 5, ajira zilisitishwa kwa miaka 5, ulimsikia kaongea?

Mnafiki tu huyu.
 
Akiwemo na yeye maana ile katiba ya warioba aliinadi ila alipoteuliwa ndani ya ccm akaikana
 
Hilo tatizo sio la ccm tu bali karibu vyama na wanasiasa wote, Polepole yupo tofauti sana na wanaisa maslahi ambao wapo kwenye vyama vyote likija jambo linalohusu maslahi yao wapo pamoja.
Unafiki ni tatizo la Watanzani wote.
 
Back
Top Bottom