Polepole: Mtu anasema miaka 50 hakuna kitu kilichofanyika mwambie tatizo na baba yako ambaye hakukwambia tulipotoka"

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
*NUKUU ZA NDG. POLEPOLE KWENYE KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM YA ARUSHA MJINI.*

22 Februari 2018

1. "Viongozi wote wa Chama na Serikali wanapaswa kufikika wakati wote" Ndg. Humphrey Polepole

2. "Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha shughulika na viashiria vya watu wanaoweza kutugawa, tutafanikiwa kama tutakuwa wamoja"
Ndg. Humphrey Polepole

3." Tunarudi kwenye misingi ya Chama chetu na watu wa muhimu kabisa kwenye chama chetu ni wanachama".
Ndg. Humphrey Polepole

4. "Kwenye Chama chetu muhimu sana wote kuwa na nidhamu na kuchapakazi kwa bidii".
Ndg. Humphrey Polepole

5." Kushinda uchaguzi kazi rahisi sana kama tutawajibika kuisimamia serikali yetu vizuri".
Ndg. Humphrey Polepole

6. "Viongozi wa Chama ngazi zote tengenezeni utaratibu wa kujua kero za wananchi, zipi zimetatuliwa na zipi bado".
Ndg. Humphrey Polepole

7. "WanaCCM tokeni mkaseme kwa wananchi nini serikali inafanya na
kwanini inafanya inayoyafanya".
Ndg. Humphrey Polepole


8. "Ukiona mtu anasema miaka 50 hakuna kitu kilichofanyika mwambie sina tatizo na wewe na tatizo na baba yako ambaye hakukwambia tulipotoka".
Ndg. Humphrey Polepole

9. "Ujumbe wangu mkuu leo ni Chama Kuisimamie serikali katika ngazi zote".
Ndg. Humphrey Polepole


Imetolewa na,

*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 
Kweli kazi ya Mungu haina makosa! Huyu jamaa tulikuwa tunamwona kichwa sasa amekuwa zombi kiasi hiki! Sasa hivi hata zile serikali 3 hazikumbuki tena
 
Kweli kazi ya Mungu haina makosa! Huyu jamaa tulikuwa tunamwona kichwa sasa amekuwa zombi kiasi hiki! Sasa hivi hata zile serikali 3 hazikumbuki tena
Waafrica wote wa avarage ndivyo walivyo
 
Back
Top Bottom