Polepole: Mmoja Mkubwa Upinzani kurudi CCM wiki ijayo

Polepole: Mmoja Mkubwa Upinzani kurudi CCM wiki ijayo

Ukiwa unafikiri kuwa hatua za maendeleo zinazoonekana ni jitihada za ccm na ukasahau upinzani utakuwa una AKILI ZA PLASTIKI.
Pole pole alisema hawataruhusu kuwapokea wote wanaoomba kurudi Ccm, wako pia wabunge ili kulinda demokrasia yetu, kulingana na tafsir ya demokrasia tuliyo kubali
 
Hivi hizi anazofanya pole2 sio siasa? Mbina wengine wakijaribu hata kukusanyikia vyumbani meao wanafurushwa na marungu? Au kijani tuu ndo kinasurusiwa?
 
Pole pole ananifurahisha sana yaani hapo namuona kabisa anavyoweka ile mikono yake ya uongo lakini leo ana washabiki wake Tanzania.
Hongera sana kwa kupigania tumbo lake mungu hambariki.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Mbona mahafali na vikao vya ndani CDM vinazuiliwa?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Wakati wengine waliwekwa ndani masaa 24 yeye anaendelea siasa nchi nzima katoka Mwanza juzi

Post sent using JamiiForums mobile app
Inakuonesha Chaguzi zina matokeo, elections have consequences,
Nawaza Ukawa ingeshinda 2015, where will Ccm have Been today,
 
Mbona mahafali na vikao vya ndani CDM vinazuiliwa?

Post sent using JamiiForums mobile app
Anaetegemea meza ya mwingine hula makombo,
Who depends on athers tables, eats last, ndo inayotafuna ukawa
 
Majizi chadema kwisha habari yao

Post sent using JamiiForums mobile app
View attachment 543066
tapatalk_1500141993160.jpeg


Post sent using JamiiForums mobile app
 
Asifikiri wote waliopo CCM wanapendezwa na CCM ya Magufuli wapo wanaochukizwa nayo na wanajiunga na upinzani na hawajionyeshi kuwa wamejiunga na upinzani,limbukeni na wataka sifa wapokea posho kutoka CCM ndio wanaojitangaza kuwa wanarudi CCM lakini wenye akili na busara zao wanajiunga kimyakimya na wapinzani.siku mbuyu utakapokuja kuanguka ndipo watakapokuja kushangaa kwa kuwa mbuyu ulikuwa unaliwa na mdudu ndani kwa ndani pasipo kuonekana.
 
ccM chao ni chao chawenzao ni chao, ghilba, madhila na choyo ndiyo hulka yao!
 
Katibu Mwenezi, ndo. Humphrey Polepole ametaja hilo akiwa Bagamoyo kwenye sherehe za mahafali ya wanafunzi kutoka shirikisho la vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Pwani, ameeleza haya,
1. Ccm haina haja ya kuhonga wa wenzetu wa upande wa pili, ila wanarudi kwani sasa wanaona Ccm Mpya inayojenga Tanzania mpya,
2. Wanarudi na mwanzo uamuzi ulikuwa warudi katika matawi husika, wapatiwe elimu ya itikadi na malengo ya chama Tawala
3. Namba sasa haitasomwa tena, maake kwa spidi iliyopo ni vigumu hata kusoma namba, 2020 ushindi mweupe,
4. Chaguzi ndogo baada ya 2015, Ccm imeshinda karibu 95%, ni mabadiliko makubwa kutoka 58% ndani ya kipindi kifupi,
5. Sheria za rasilimali zetu ni bora zaidi kuliko nyingine zozote zilizo wahi kuwapo, hapa amewapa changamoto watanzania wenzetu wasio na uzalendo wanao kaa kushambulia jambo jema hili, wanatamani wananchi watanzania washindwe,
6. Ameonesha namna ambavyo Jembe letu, chuma cha Pua, Mzalendo JPM amepambana na anaendelea kupambana, hongera kwake Mh. Rais,
7. Ametoa pole kwa wananchi wa Pwani kwa matatizo wanayopata, shukran sana,
8. Amehimiza uadilifu na kuonya wanaopanga safu za viongozi Chamani,
9. Ccm ndio chama pekee Tanzania kinachopigania haki, na umoja kwa watanzania,
Katika mahafali hayo watu kadhaa walipata nafasi ya kuongea machache, Mh. Ridhiwani, Mh. Kawambwa, Mwakilishi wa wakuu wa Vyuo Mkoa wa Pwani DR. Masanja, ndugu Mabuga mwenyekiti Seneti pwani, katibu Ccm Mkoa wa Pwani,
Wakati huo huo katibu mkuu a chadema na viongozi wenzie wamekamatwa na polisi wakidaiwa kufanya siasa!

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Mpuuzi sana huyo kijana.
Anajitamba vipi kuwa mshindi na kimbilio la watu ilhali wamezuia vyama vingine kufanya siasa ?

Wao kila kukicha wanafanya mikutano ya nje na ndani,lakini wengine marufuku,wakilkusanyika tu wanakamatwa na kubambikiwa shitaka la unlawful assembly.

Polepole "skulumeti" wangu nlikuheshimu sana lakini sasa umekuwa mnafiki kupindukia,ni dhahiri hata aliyekuwa Headmaster wetu Mzee Kwayu(Azania sec) anajihuzunika mno kwa namna ulivyokengeuka
 
Back
Top Bottom