Polepole kuitisha mifumo ya uchaguzi na NIDA kuhusiana na CCM kukaguliwa, ili kujiridhisha ina maana gani kiufundi?

Polepole kuitisha mifumo ya uchaguzi na NIDA kuhusiana na CCM kukaguliwa, ili kujiridhisha ina maana gani kiufundi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
"Nimefanya ka research kidogo, kuongea na manguli kadhaa wa kadhaa pia kuchukua wasaa kujiridhisha."

Yafuatayo ni Yatokanayo:

Ashukuriwe mwana halisi wa nchi hii Humphrey bin Polepole aliyeutambua u Tanzania wake kama thawabu kubwa zaidi mno, dhidi ya uchawa na uchama.

Kasema Polepole mifumo ihusikanayo na uchaguzi imekuwa inachezeka vilivyo kutokea CCM. Jambo hili si dogo, "a very serious issue!" Kwamba wako na "unauthorized, full access," wahuni wasiyopaswa kuwa nayo.

Hii ina maana kutokea CCM kuna milango ya kuingilia kwa wakati wao na kufanya mabadiliko yoyote: ikiwamo kufuta, kuhariri, kurekebisha, kuongeza, kupunguza, nk, lolote; kama inavyoweza kuwapendeza wao kwa wakati wowote. Kwamba kwa mfano, CCM wanazo funguo zote za spare za vyungu vyote muhimu, ikiwamo vya tume ya uchaguzi!

Anachoitisha Polepole ni kitu muhimu sana. Kuwa inatakiwa kufanyika "total forensic audit" ya hiyo mifumo yote iliyotajwa, na hasa ya vyungu (servers) vya pale tume ya uchaguzi.

IMG_20240428_070927.jpg

Ikumbukwe kwa Kenya waliokuwa wanashikilia funguo za vyungu vya IEBC wakati Ruto akifanza vitu vyake, leo wote ni marehemu. Humo wamo yule ambaye ni wazi kuwa aliuwawa na bwana Wafula Chebukati mkurugenzi mkuu IEBC, aliyekufa chigafla akiwa na miaka 61, "mysteriously" kama Magufuli tu.

Forensic audit yataka ubobezi. Zieleweke taarifa zote za ma vyungu yaliyopo, database gani, apps gani, na makorokoro kadha wa kadha wezeshi husika yanayo ikamilisha mifumo husika.

"Zionekane log files zote zenye kutunza kumbukumbu zote za utendaji wa vyungu vyenyewe. Kwamba nani alingia, alingia lini, kutokea wapi, akawepo muda kwa gani, akafanya nini, nk."

Uzuri mifumo hii mamboleo, huwezi kuzitoroka wala kuzifanyia karabati log files, nje ya kuzifuta tu. Kama zimefutwa hiyo nayo ni taarifa muhimu ya ukaguzi zaidi. Tangu lini mhalifu akaweza kuondosha alama zake zote kwenye eneo la tukio? Hapo pia bado cross examination za viwango vya kina Chibatala au TAL. Kwamba ni lini ziliwahi mwacha m'bambika kesi gani, wapi salama?

Kwamba taarifa zote, za nani kaingia, tarehe ngapi, saa ngapi, kutokea wapi, kafanya nini nk, nk, zipo? Hapa si ni kama chui tu aliyeng'ng'aniwa na fisi kwa mkia?

Kwani kunatakikana nini basi wandugu hata tukafike huko kwenye kufukua makaburi? Kaorodhesha Polepole pale mambo yote ya kufanywa, tena kwa unyenyekevu mkubwa. Kulikoni yafike mbali hadi wakaanze kupatikana kina Balali? Kwamba hata hao nao kumbe wangali hai?

Tusifike mbali hadi tukafikishana kukimbizana na ma interpoli right, left and center, wakati sote ni ndugu. Yote ya nini? Polepole anaomba: "kupisha shari, si kumwagwe oil tu?"

Si ashauriwe mama sawa sawa, tena kwa unyenyekevu mkubwa amwage oil, wakati ungalipo!

Pia soma : GE2025 - Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba
 
Binafsi Pole Pole nimemuelewa vizuri kabisa.

Kuna siku walikuja watu wa CCM wakitaka kuniandikisha ili wanipe Kadi, Sasa kilicho nishangaza walikuwa wanataka na Namba ya NIDA.

Nilipowauliza Namba ya NIDA na Kadi ya CCM vinahusianaje wakashindwa kunijibu.

Nikawaambia sihitaji na Kadi yao.

Tangu wakati huo nimekuwa nikihisi kwamba Kuna Namba Vitambulisho vya NIDA vinatumiwa na CCM kuiba kura.

Hili la Pole Pole ni uthibitisho tosha.

Oktoba NRNE
 
Hapa sasa ni kuunganisha nguvu na kina Gwajima. Hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.

Wana access kwenye vyungu kwenye tume ya uchaguzi vipi bank kuu, kwenye banks zingine?

Vipi migodini au hata bandarini huko?
 
CCM mbinu zao zote zitaanikwa tu safari hii

Hapa tuunganishe nguvu na wote tunaosikilizana tupigane na agenda za leo. Tulikuwa na nafasi ya Tanzania njema sana.

Agenda za yeyote kuturudisha nyuma tusimvumilie mtu. Akielewa Act, CHAUMMA, Mbowe au awaye ,yote karibu. Asipoelewa akafie mbele!
 
Binafsi Pole Pole nimemuelewa vizuri kabisa.

Kuna siku walikuja watu wa CCM wakitaka kuniandikisha ili wanipe Kadi, Sasa kilicho nishangaza walikuwa wanataka na Namba ya NIDA.

Nilipowauliza Namba ya NIDA na Kadi ya CCM vinahusianaje wakashindwa kunijibu.

Nikawaambia sihitaji na Kadi yao.

Tangu wakati huo nimekuwa nikihisi kwamba Kuna Namba Vitambulisho vya NIDA vinatumiwa na CCM kuiba kura.

Hili la Pole Pole ni uthibitisho tosha.

Oktoba NRNE
Mimi walifika usiku saa 2 wakadi nida nikawauliza mumetokea nida mara hii kwa sababu nawajua shughuli zao. Wote watatu waligeuka nyuma na kuondoka.
 
Mimi walifika usiku saa 2 wakadi nida nikawauliza mumetokea nida mara hii kwa sababu nawajua shughuli zao. Wote watatu waligeuka nyuma na kuondoka.

Futungo + wahuni wa Polepole wana uchunwa madaraka uliopitiliza.

Uchu kuliko mzee fisi!
 
Anachoitisha Polepole ni kitu muhimu sana. Kuwa inatakiwa "total forensic audit" ya hiyo mifumo yote iliyotajwa, na hasa vyungu (servers) vya pale tume ya uchaguzi.
"Zionekane log files zote zenye kutunza kumbukumbu zote za utendaji wa vyungu vyenyewe. Kwamba nani kaingia, kaingia lini, kutokea wapi, kawepo muda gani, kafanya nini nk."
Dah,
Inasikitisha sana.

Kwa sasa unahitajika muujiza wa haraka wa kukwamua nchi kutoka mikononi mwa wahuni na magenge ya wahalifu
 
Kaorodhesha Polepole pale mambo yote ya kufanywa tena kwa unyenyekevu mkubwa. Polepole anaomba kupisha shari, si kumwagwe oil tu?

Si ashauriwe mama sawa sawa, tena kwa unyenyekevu mkubwa amwage oil, wakati ungalipo!
Asante sana kwa uzi wako mzuri.
 
Dah,
Inasikitisha sana.

Kwa sasa unahitajika muujiza wa haraka wa kukwamua nchi kutoka mikononi mwa wahuni na magenge ya wahalifu

NRNE, TAL na Polepole, ni mpango wa Mungu. Impendeze Mungu tuwawajibishe wahuni wote sawa sawa na uhuni wao.

Kwa hakika alipiga Polepole zaidi mno ya mle kulimo tarajiwa:

NRNE na mazagazaga yake ni mpango wa Mungu. Nani ajuaye kuwa Polepole leo, hatutajua walipo wenzetu waliopotea na yote ya uvunguni?

Tlaat laah, Shtuxnet, Hoihoi2, ChoiceVariables, Manyau Nyau, shiembe, sandrano, joni, Lukasi na wale wengine:

Au nasema Uongo?
 
Kwa hakika alipiga Polepole zaidi mno ya mle kulimo tarajiwa:
👇
 
Roho yangu inapata ganzi napowaza hii Hali !
TISS imefikia hapa?..Uzalendo kwa nchi umefikia hapa?
..au Kuna mwingiliano( usio na afya) na Intelijensia( tukufu) ya JWTZ?
...haya , je Wastaafu tena wabobezi nao wanajidanganya. kuwa anayewalipa viinua mgongo yuko timamu?
Bora nianze upya kusoma somo la Uzalendo...maana huku mtaani kumechafuka..
 
🙌🙌kuna watu wamepewa Kadi ya Chama na hawakuomba
 
Back
Top Bottom