Polepole: Cheche zangu hizi hapa

Polepole: Cheche zangu hizi hapa

Pole Pole anadhalilisha tunu na ufahamu aliopewa Binadamu na Mungu ili kuwatofautisha na viumbe/wanyama wengine hususani Kuku.
 
Ukweli unatakiwa ulewe sana ndio uweze kusimama mbele ya kamera kuyazungumzia haya masuala ya madini na rushwa hasa ukiwa wewe ni mwanaccm! Mnaanzaje kumwaminisha mwananchi kuwa yale mliyoyafanya miaka ya nyuma siyo haya mnayoyapaka rangi kwa nje? Mliingia mikataba ya hovyo, juzi mnaahidiwa hiyo good faith tena kwa upfront na mtu yuleyule mliyemwita mwizi miezi mitatu nyuma mkamshangilia na kumbadilishia jina na kumwita a real friend! Hata yule mzungu aliwashangaa sana mjue!
Siamini na sitokaa niamini kuwa maendeleo ya nchi hii yataletwa na kusimamiwa na ccm! Yaani badala ya kufanyakazi kama chama tawala mnafanya ya kina Zitto et al.
 
USAHIHI NA UHALALI WA SERA NA MSIMAMO WA CCM

Mnamo mwezi wa April 2017, Kabla ya Majadiliano na Barrick walisema kwa kuzuia makinikia tutashtakiwa na kushinikiza tuachane na jambo hilo.

Ilipofika kwenye mwezi wa Julai 2017, tukaendelea kusimama imara na kuwapuuza, Mtendaji wa Barrick akaja na kukiri makosa na kukubali lazima Tanzania ipate haki yake katika uchimbaji madini. Wapinzani wakasema sio kweli na hatukuelewa kiingereza cha Bwana Thornton. Tuliwapuuza na tukaanza majadiliano kwa umakini mkubwa, kwasababu hawakujua mazungumzo yalikuwaje, wakazusha kwamba ngoma nzito, na eti majadiliano yamekwama.

Leo Mwezi wa Oktoba 2017, Majadiliano yameisha na Mtendaji wa Barrick amesema haya ni makubaliano bora zaidi kuingiwa huenda Duniani. Tanzania inapata gawio la umiliki migodi asilimia 16 na itapata gawio la faida baada ya kodi zote kukatwa la asilimia 50 na Barrick asilimia 50.

Maana yake ni 16% + 50% ya faida + Kodi zote kwa mujibu wa sheria + Bilioni 700 za awali na Mazagazaga mengine kibao kwa watanzania.

Wapinzani mufilisi wanasema eti tukatae twende Mahakamani.

Tumewashtukia, tumewang'amua mnataka kutuchezesha ngoma ya kitoto ilhali sie watu wazima.

Kwa Serikali ya CCM, Endeleeni kuchapa kazi maana 2020 tutatoa hesabu kwa ushahidi, hawa jamaa wa kuzungusha ngumi na vidole uma hawana cha kupoteza

Rais Magufuli ameshaelekeza kufumua pia maeneo mengine ya madini katika Almasi na Tanzanite ili kuhakikisha kila haki ya watanzania inapatikana. Najua katika mchakato na vita hii tutakanyaga vidole vya baadhi ya watu tunafanya kwa nia njema na maslahi mapana ya watanzania.

Waendelee kuzungusha ngumi wakati sisi tukizungusha gurudumu la Maendeleo ya Taifa, wakati wao wakinyoosha vidole sisi tupambane kunyoosha nidhamu ya Nchi na hasa kwa watumishi na Viongozi wetu.

Ukombozi wa Kiuchumi ni Sera ya CCM Awamu ya V na ni hakika

Ndg. John Pombe Joseph Magufuli watanzania wamekuamini simamia haki zao, unaacha alama kubwa katika maisha ya wananchi wa kawaida, utabarikiwa hapa duniani na mbinguni, komaa baba, sisi watu wa kawaida tuko nawe na tunaona matunda ya kazi zako.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Huwez kuwa timamu ukaandika upuuzi huu, unatuaminisha ccm ni chama chakuendelea kupewa nafasi leo tena toka 1977 kwa hali hii? Sheeenzi kabisa utakuwa mchawi wewe uzeeni
 
Magufuli ni level nyingine muda utaongea, kama issue ya madini ameiweza basi hatashindwa na kitu chochote tumpe ushirikiano tu Tanzania itafika mbali.

Ni ushirikiano upi wakati wewe mwananchi tu! au kumuombea na kama tunasikilizwa si tujiombee wenyewe kwanza, mambo ya kushadadia watu wanatimiza wajibu wao na tena wanalipwa ndio ulofa.
 
Mbona mkalimani alikuwa nyuma ya Thornton akitafsiri lakini kwa macho yako ya kibavicha hukumuona?
Ndio mlivyoaminishana kuwa bodyguard alivyomwambia atoke akakae nyuma ya Thornton, kwani kipaza kilikuwa nyuma ya Thornton? We kweli umelewa
 
Polepole alikuwa yuleee, sio huyu hapa, masikini! Mpaka huruma
 
Waipeleke Bungeni sasa hayo makubaliano wabunge wakayajadili kama ni kweli wanakiona walichokifanya ni sahihi.
 
Back
Top Bottom