Poleni Rivers, ila hongereni pia! Mmekufa kiume kama Madunguka fc

SALOK

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
3,318
1,936
RIVERS FC, "Mwana kuli-find, mwanakuli-get". Hatimaye tumemalizana. Mlitutoa, tumewatoa, tunasonga mbele... WE ARE YOUNG AFRICAN..!! Kisasi kimeisha... Kwa hili poleni sana, ndivyo Mpira ulivyo.

RIVERS FC, Hongereni sana, leo hamkufungwa! ila mmepata suluhu ugenini.. Si jambo dogo hilo. Kwa hii YANGA ya mwaka huu! kupata suluhu ugenini si jambo dogo asilani, Shukuruni kwani, hakika mnayo bahati kubwa sana, mnastahili pongezi, wangekuwa MAKOLO wangetoa na Sadaka..

MUHIMU! Twafahamu Rivers fc wa mchongo mpo, na leo mlitamani Mabingwa wa Kihistoria tunaadhirika mfano wenu mlipoliaibisha taifa juzi, laa haula! laiti haileti, jambo limekuwa kinyume chake, WANANCHI tumenawirisha TAIFA baada ya aibu yenu. Mkaishia kupata juice safi ya Limao na ndimu.. Msilalame, mmepata mlichostahiki na kustahili, wazee wa robo fainali... wafa kiume! Hata hivyo msijali.. YOUNG AFRICAN SC. Ipo kwa ajili ya kuwapa furaha watanzania...

Ndio maana ikaitwa TIMU YA WANANCHI, Kwa hisani ya watanzania wote mkiwemo nyie Madunduka fc, Makolokolo fc, Ngada fc ama Mikia fc mnayo haki ya kufurahi pamoja nasi kama "WANANCHI". BASI FURAHINI SASA NA HATA BAADA YA KUINGIA FAINALI, KISHA KWA HISANI YA GSM TUTAWAALIKA MAKOLO WOTE KWENYE DHIFA YA KITAIFA YA KULIKABIDHI KOMBE LA CAFCC MWAKA HUU KWA WANANCHI, MAANA HAKUNA WA KUIZUWIA YANGA MSIMU HUU KUCHUKUA KOMBE HILI, MTARUHUSIWA KUPIGA NALO PICHA..!!

HITIMISHO, Rivers fc mmekufa kiume ugenini, Kama ambavyo Madunduka fc, juzi walikufa kiume kule Moroco, tuendelee kufurahia Football.....!!!
#GSMforTANZANIANfootball
 
Vpi tuwakabidhi kombe lao .....kama tuliwapa makolo FC .....kombe la kufa kiume
 
Chuki zenu ni kubwa sn sn kwa simba aisee. Furahini kwa kufuzu na si kumwongelea Simba kila saa mtapata pressure.

Simba katolewa ni dhaifu na Yanga kafuzu yupo vizuri.

Kama ni maumivu ya kufungwa goli 2 kwenye ligi,jipangeni mfuzu kwa Singida ili mkutane na Simba fainal ya FA.

Mnateseka sana
 
Simba ni kama Shamba letu tu wala hamtusumbui, zile 2 kwa mkapa ni vile tu tulijiamini kupita kiasi na kwadharau pia.... Ila si mbaya tutamalizana AZAM CUP
 
Simba ni kama Shamba letu tu wala hamtusumbui, zile 2 kwa mkapa ni vile tu tulijiamini kupita kiasi na kwadharau pia.... Ila si mbaya tutamalizana AZAM CUP
😂😂😂 eti tulijiamini kupita kiasi.......
Unaona team yako inalingana na Simba?
Lipi yaani?
Mfano Msimu huu ambao yanga anauona ni wa mafanikio kwake.
Kamzidi nini Simba mpaka sasa?
Ligi? Not yet yanga hajawa Bingwa bado.
FA? Wote mpo Semi final...
CCL ? Yanga alitolewa round ya pili, Simba alifika Robo.
CCC yanga kafika Semi, Simba hajashiriki.
 
eti tulijiamini kupita kiasi.......

CCC yanga kafika Semi, Simba hajashiriki.[/QUOTE Msimu huu]Yanga amechukua ngao ya Jamii Kwa ku mkanda Simba, Kwaiyo Hatufani.
 
Serikali ina wapenda isha wapa kombe lao makolo
7844235.jpg
 
eti tulijiamini kupita kiasi.......
Unaona team yako inalingana na Simba?
Lipi yaani?
Mfano Msimu huu ambao yanga anauona ni wa mafanikio kwake.
Kamzidi nini Simba mpaka sasa?
Ligi? Not yet yanga hajawa Bingwa bado.
FA? Wote mpo Semi final...
CCL ? Yanga alitolewa round ya pili, Simba alifika Robo.
CCC yanga kafika Semi, Simba hajashiriki.
Mapinduzi Simba mechi ya kwanza out,Yanga mechi ya pili.
 
Nyie msijifananishe na simba na pira lenu bovu..nyie semeni asante Mungu kwa kutupa kundi vibonde...
 
Chuki zenu ni kubwa sn sn kwa simba aisee. Furahini kwa kufuzu na si kumwongelea Simba kila saa mtapata pressure.

Simba katolewa ni dhaifu na Yanga kafuzu yupo vizuri.

Kama ni maumivu ya kufungwa goli 2 kwenye ligi,jipangeni mfuzu kwa Singida ili mkutane na Simba fainal ya FA.

Mnateseka sana
Baada kutufunga ikawaje?
 
Back
Top Bottom