Habari
Ni Jumatatu, leo asubuhi. Nimefika kituo cha dala dala, nasubiri usafiri wa kwenda mtaani kutafuta cha kutafuta. Noah imekuja, ikapaki. Mshikaji wangu, hatujawasiliana kitambo tu. Kaniona, kasimamisha gari.
Kanipigia honi. Mwanzoni nilihisi ni ile style ya wenye magari binafsi kubeba abiria vituoni kwa kulipa buku buku ama buku 2, mtindo maarufu sana kwa waenda POSTA ama K'koo asubuhi.
Nilipokuwa naisogelea ili kuona kama Noah inaenda ninakoenda, na kama ntamudu nauli tajwa, jamaa akanitaja kwa nickname yangu ya zamani ya kichuo chuo.
Nikachanganya miguu, fasta nikadandia siti za kati kati, mbele kushoto alikaa shemeji.
Nyuma yangu kulikuwa na bidada wawili ambao na wao walikuwa na hisia kama zangu, kwamba dereva wa Noah ile anasanya, shemeji sijui kwa moyo wa huruma na kujua tabu za usafiri DSM asubuhi, akanambia waambie wapande, ama alihisi niko nao ama vp, sikuweza kujua, maduu wale wakapanda, nikakaa nao nyuma.
Laah haulah! Kumbe kuna mmoja wa wale maduu ni EX wa mshikaji, kituko ni kwamba jamaa hakushtukia mapema lile movie, kwamba katika abiria wake, kuna mmoja ni zaidi ya abiria wa kawaida.
Bahati mbaya ikaja, katika story story na kupeana ripot za mapito ya kipindi ambacho tulipotezana, kuna topic iliwagusa wale madada duu, mara wakawa wachangiaji, jamaa akashtuka kuskia sauti ya Yule mmoja. Jamaa akawa anaibia ibia kwa kuangalia pale kwenye kioo cha juu ya ndani ya gari, hakutosheka akaamua kugeuka kabisa! Mii niliiona ile movie lakini sikuwa naelewa lile chezo.
Tukiwa katika foleni jamaa akani-sms: "kuna msala humu, huko nyuma umekaa na kimeo changu, naomba usishuke mpaka mwisho, majanga kaka!" Mii sikumjibu ila nikatii Agizo Lake.
Sasa sijui ni kujifanya wa mjini ama kujifyatua akili, Yule ex, si akaanza kujifanya anamjua sana mshikaji, full kuchangia mada, sisi tumenyamaza yeye full kuroporopoka, mada ikiisha anaanzisha nyingine, gari zima kimya, yee bado yupo tu. Ghafla tukajikuta mada imekuwa ya watu wawili tu, wife na ex wa mshikaji, tulishakuwa waoga wa kuchangia! Jamaa akahamishia mada kwenye matangazo ya radio.
Tulifika mwisho wa safari salama salmini, jamaa ikabidi nimpe pole tu, nikaanza upya safari yangu ya kurudi ofisini kwangu, hamu na kiherehere cha lift kiliniisha! Thanks lord umenikutanisha na rafiki yangu wa kitambo.