Kama "hatafanikiwa na atadharaulika" kwa nini unamfuatilia ?
Kwa nini unamtisha mtu anaepaswa kudharaulika ?
Ni wazi anachofanya kina impact. Unamwogopa akiendelea kusema.
Hamjazoeza kuona balozi anaikaanga serikali kama mpinzani.
Jamani CCM, nyakati zimebadilika. Hatuko tena in the 80s and 90s.
Population ime explode, wasomi wameongezeka, teknoloji zime revolutionize dunia, watu wametembea ng'ambo, taarifa za habari za dunia tunazo kwenye simu.
Ni ngumu enzi za leo kutawala watu kama ni wale wale post independence peasants waliokuwa wana TV mbili D'Salaam, kwa Nyerere Msasani na kwa Shehe Yahaya Magomeni Mwembechai.
Mtatumia nguvu ya kuua watu weeee, mwishowe kitasanuka tu!
Na si wote mtakaowaua watakuwa nguruwe wasio na sauti. Kuna siku bila kujua mtaua mtoto wa mwanajeshi au wa mlinzi wa kiongozi, ambae hatakubali, ataamua kufa na mwanae. Binadamu sio zezeta ataekubali kuchinjwa siku zote na kuibiwa na watoto wa Rais wastaafu na wake za mawaziri, na shombe wanne wanaoshikilia uchumi waliotajwa leo na Mzee Malisa, kada wa CCM. Haiwezekani. Watawala badilikeni.
Mamilioni ya Watanzania wameona live mwenzao anamwagwa damu yake sebuleni kwake Mbeya. Kwa kosa la kudai maendeleo, kuikosoa serikali. Na Mzee anashushwa kwenye gari la abiria anachomwa na Sulphuric Acid, anayobolewa macho anatupwa kwenye majani.
Wameyabeba hayo! Msidhani mkipita wanawaita waheshimiwa basi wanamaanisha. Wana maumivu na hasira kali. Ndo maana mkifa wanaandamana kwa nyimbo barabarani. Haya, endeleeni kutawala kwa mabavu na kununua na kuuza nchi.