Hi imetokea kweli, nchi moja ya Kiafrica, bwn 1 alikua akiishi na dada yake (kaka alikua ana mke na watoto kadhaa) huyu dadake akaja kolewa na bwn 1 hapo hapo mjini kwao, maisha ya ndoa yakiwa yamesogeza miaka, wana ndoa hao wakawa wanagombana mara kwa mara, mke alikua akipeleka mashtaka kwa kaka yake, ilifikia binti anataka ku divorce, mara baada ya divorce mpango wake ilikua kurudi kwa kaka yake while akiwa anafanya shughuli zake za hapa na pale, siku 1 kaka yake akamwambia hivi;
Nataka shemeji yangu asikitike sana siku nitakapo kuja kukuchukua, sijashindwa kukulea dada yangu, fanya hivi, kuanzia sasa, fanya kila anachokwambia kufanya, akitaka maji ya kuoga saa fulani, hakikisha muda huo ukifika mpe, mfanyie kila kitu, ili siku nikija kukuchukua aone kwamba hakika ana ku- miss sana, binti akamsikia kaka yake na kuamua kwenda kwa mumewe
Wiki na miezi ikasogea, mume akawa mume kweli, dada akaanza kupokea vijizawadi vya hapa na pale, binti mwili ukaanza kuja, akiomba pesa za matumizi binafsi anapewa, akaona aende kwa kaka yake kumwambia kwamba, mume wangu kabadirika sana, ananipenda sana, kaka akamwambia, YES that is what i wanted, sasa nakuja kukuchukua ili asikitike sana, haya ndio yalikua maneno ya huyu dada, KAKA KWA SASA NGOJA KWANZA TUSUBIRI< sijisikii tena kuondoka kwake.
Brother akamwambia, ukiona kivuri cha kitu, ujue kuna hicho kitu somewhere, ukiita kwa sauti kubwa porini, sauti ile ile hua inakurudia (Mwangwi) so kabla hujalaumu, ni vizuri ujikague uone, ARE YOU NOT THE SOURCE OF THE PROBLEM?