Podcast suggestion

Podcast suggestion

Raskazimi

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
1,209
Reaction score
1,413
Kuna tabia yetu wengi kwenye mijadala ya kisiasa kutoa hoja zinazokosa uelewa wa historia na matokeo yake, tunakosa depth/uzito wa hoja ambao kuna wakati huko nyuma JF ilisifika kwa kuwa nao.

Wachangiaji mahiri waliolipa jukwaa hili heshima enzi za uchanga wake aidha wameondoka pengine kwa kutopendezwa na mwelekeo wa jukwaa au kwa sababu zao binafsi.

Kuna uwezekano pia kukua kwa umaarufu wa jukwaa kumekuja na wanachama pengine wasio na uelewa/kumbukumbu za nchi yetu, tulipotoka kisiasa na kiuongozi au wenye nia ovu la kuvuruga mijadala kwa lengo la kufifisha credibility ya jukwaa na hatimaye kuliondolea relevance.

Kwa mwenye nia njema ya kuwa na mchango kwenye maendeleo ya kweli ya nchi yetu, hasa kisiasa, na angependa kujua historia ya siasa zetu, rekodi za wanasiasa/viongozi kwenye ishu mbali mbali, mapito ya nchi yetu kidemokrasia, siasa za Bunge na mambo kama hayo, kwa sasa sidhani kama kuna chombo kinachofanya kazi nzuri ya ku document haya kwa mwenye nia ya kujifunza kama podcast ya Nadj Khamisi na Tundu Lissu inayokwenda kwa jina la Speaking Out with Tundu Lissu na kupatikana kwenye mtandao wa audiomack.

Kwa vipindi vinne vya kwanza toka kuanza kwake, pamoja na kuwa na wageni wapinzani na kuendeshwa na Tundu mwenyewe, hata usipokubaliana nao kiitikadi naamini kuna la kujifunza.

Ningeweka link lakini sina uhakika taratibu zinaruhusu
 
Back
Top Bottom