Leo nimekuja na ombi lingine. Hivi mwanamke (mama wa nyumbani)anastahili au hastahili kupewa pocket money ya kujinunulia vitu vyake vidogo mpaka aviorodheshe kwenye list ya vitu vya mwisho wa mwezi! Kwa kweli hili jambo linanishangaza sana kwa huyu bwana maana kupewa hio pesa ni mpaka uiombe kwa nguvu sana ikibidi na ugomvi juu yake. Sasa mume asimpompa mke pesa ategemee akapate wapi! ukiuliza kwa nini hakupi hiyo pocket money kila mwezi anakaa kimya tuu, ukimuuliza haujui kwamba anatakiwa kufanya hivyo anasema anajua. Sasa jamani mtu kama huyu aelewekeje! naombeni msaada tafadhali.
hayo matumizi madogo madogo ni yepi kwa hao kinamama?
Kwa maoni yangu, mwanamke anastahili kupewa pocket money ya matumizi yake madogo madogo, lakini wakati huo huo kwa dunia ya leo ni vizuri mama akajaribu kutafuta njia za kujiendeleza ili apate ajira au hata kufungua kabiashara kadogo ambako katamhakikishia mapato ya kukidhi matatizo yake madogo madogo ya kila siku ili kuepukana na ugomvi wa kuomba pesa kwa wanaume wakorofi ambao hawaelewi kama mwanamke anahitaji pesa za matumizi yake madogomadogo.
Sorry i use the same names. Asante sana kwa msaada wako kaka, kwa kweli ningeliweza kufanya kazi hapa nilipo ila ndo mpaka niielewe lugha ya nchi kwanza. Na licha ya hapo nilimwambia basi aninunulie drier la nyewele ili niweze kutengenezea angalao wanawake nyewele (domestic saloon.) ila napigwa kalenda za hiyo hela mpaka sasa. Nimeamua kukopa hela kwa mama mzazi nyumbani na amenihaidi baada ya mwezi mmoja.
---bubu bubu bubu.... tema mate chini mara moja!!! yaani njemba kama kibunango hujaitambua tu na post zake zote hizo kwenye 'mambo ya wakubwa'?!!Samahani Kibunango kama nimekosea, nadhani wewe ni mwanamke hivyo ungekuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutufafanunulia hayo matumizi., kama si mwanamke niwie radhi kwa makosa yangu. Matumizi hayo ni pamoja na vipodozi ikiwamo kutengeneza nywele au kusuka na pia usafi wa mwili wake hasa anapotembelewa na yule jamaa wa kila mwezi. Vinginevyo njemba inaanza kumezea mate visura wengine wakati wa kwake hampi matunzo yeyote yale ili naye apendeze.
---bubu bubu bubu.... tema mate chini mara moja!!! yaani njemba kama kibunango hujaitambua tu na post zake zote hizo kwenye 'mambo ya wakubwa'?!!
---jaribu basi kucheck vituko vyake vya Zenji upate kumwelewa kibunango!!!
---asilan umeshaomba radhi, natumaini atakusamehe........ 😉
Pole sana dada jaribu kuwa mvumilivu labda mumeo atabadilika na kuona umuhimu wa kukupa pocket money. Jitahidi uijue lugha ya hapo ulipo hii itakusaidia katika kupata ajira, pia kuna umuhimu mkubwa wa wewe kwenda shule kama utaweza kufanya hivyo.
Leo nimekuja na ombi lingine. Hivi mwanamke (mama wa nyumbani)anastahili au hastahili kupewa pocket money ya kujinunulia vitu vyake vidogo mpaka aviorodheshe kwenye list ya vitu vya mwisho wa mwezi! Kwa kweli hili jambo linanishangaza sana kwa huyu bwana maana kupewa hio pesa ni mpaka uiombe kwa nguvu sana ikibidi na ugomvi juu yake. Sasa mume asimpompa mke pesa ategemee akapate wapi! ukiuliza kwa nini hakupi hiyo pocket money kila mwezi anakaa kimya tuu, ukimuuliza haujui kwamba anatakiwa kufanya hivyo anasema anajua. Sasa jamani mtu kama huyu aelewekeje! naombeni msaada tafadhali.
Kaka naenda hiyo shule, lakini si unaelewa tena mambo ya kujisoapsoap kidogo. Ndo maana nataka angalao nijishughulishe kidogo angalao, nisijibweteshe sana lakini mwenzangu anakuwa mgumu kama kisiki na ahadi za uongo...ananikatisha tamaa, maana kama sie yeye wakunisaidia and especially huku ugenini nani mwingine! Na niongee naye vipi ili aelewe somo! Sasa kama hawezi kunisaidia mpaka nasaidiwa na wazazi wakati mimi ndo wakuwasaidia ipo maana gani ya kuwa pamoja? Hebu nisaidieni mwenzeni na mawazo.
...Teh! teh! tehhhhhh!!! usipomjali watu wanakusaidia balaa inaanzia hapo!!!Mjali mkeo
Nashukuru kwa kumtambulisha kamanda Bubu...---bubu bubu bubu.... tema mate chini mara moja!!! yaani njemba kama kibunango hujaitambua tu na post zake zote hizo kwenye 'mambo ya wakubwa'?!!
---jaribu basi kucheck vituko vyake vya Zenji upate kumwelewa kibunango!!!
---asilan umeshaomba radhi, natumaini atakusamehe........ 😉
Hongera sana kwa kuamua kwenda shule. Nakubaliana na wewe kabisa kwamba mumeo ana wajibu wa kuhakikisha unapata mahitaji yako muhimu ikiwa ni pamoja na vipodozi. Si ajabu mwanaume huyo huyo ambaye sasa hivi hakupi chochote ili kuutunza mwili wako akaanza kulkualamikia mwanamke mchafu na maneno chungu nzima ya kukukosesha raha na hata akakupa mifano mwangalie mke wa fulani siku zote anajitengeneza, kujipodoa hivyo kuonekana mzuri. Uko ugenini ni lazima ucheze karata zako vizuri ili usije kupata matatizo makubwa zaidi. Kuongea tu ndiyo suluhisho la tatito lako jaribu kutotumia lugha kali unavyomkumbusha mwenzio kuhusu mataji yako.
...Pole pole Penny, jaribu kwanza kuchukua hatua za kurekebisha mambo na huyo mumeo then uone itakuwa vipi. Unajua ukiamua kwenda kuonja nje nako ili kupata mbadala kuna tabu yake wengine ni mafundi sana utajikuta unatamani uhamie kabisa maana ukilinganisha na mumeo na hivyo anakuboa boa my friend you will end up in trouble!!!!Sio siri mpaka naingiwa sasa na hivyo vishawishi lakini namuomba Mungu sana anisaidie.
dada Penny sory to say but you sound nagging! For men to get your needs met never nag my dear, find specific times and learn to be patient. Maybe mambo naye kwake magumu na mwanaume hataadmit at first time. Mchukulie taratibu na mkumbushe akiwa stressfree, The point ya kukopa kwenu ungemtaarifu tu but for typical african men akijua unapewa hela kwenu itakuwa tabu.
Yes Men are meant kuwasupport wake lakini dunia hii si kama ya jana mdogo wangu, zamani vipato bwerere but now ni opposite. Just be calm and talk it out.
Good Luck.