Please jamani inabidi tubadilike

Please jamani inabidi tubadilike

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,379
Sio ajabu sikuhizi ukipita kila kona utakuta watu wengi wakipoteza muda wao mwingi wakijihusisha na matendo machafu ya ngono ikiwa aidha kupenda ngono, kutongoza ovyo ovyo, kuangalia ma porno, ushoga, usagaji, na wengine punyeto hivi majuzi tu nmepita ofisi flani wafanyakazi flani bize wapo kwenye kompyuta wanachek x tena mkono ukivinjari sehemu nyeti akiwa hivyo tunakoelekea ni wapi wandugu?
 
Ndio maisha waliyoamua kuyaishi kwa majira haya
 
Dunia ya sasahivi ilipofikia ni kwa Neema tu tutaweza kukombolewa, manake lusifa kamwaga roho chafu zinafanyakazi tena overtime, bila kujikabidhi kwa Mungu tegemea anguko kubwa no
 
wewe mwenyewe huwa hutongozi, hutii, huangalii picha za x? Majibu unayo mwenyewe.
 
We are living in a society where losing a phone is more important than losing a virginity!!
 
Mtakatifu na azidi kuwa mtakatifu, na mchafu na azidi kuwa mchafu, kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.
 
Dunia imebadilika kiasi kwamba mambo hayo yanakuwa wazi zaidi siku hizi.
 
Mtakatifu na azidi kuwa mtakatifu, na mchafu na azidi kuwa mchafu, kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.

Kama imefikia hapa basi dunia imekwisha.. Huwa nikitafakari hilo neno......
 
Nadhani kila kitu kina mahala pake, mbaya ni pale unapofanya kitu sehemu isiyotakiwa.

Mfano; Kuangalia porn ofisini, lakini kuangalia ukiwa kwako sio mbaya.
 
Hujamalizia, huwa ukitafakari unafanyaje?

Najiuliza sana, hivi Haya maovu nifanyayo sipati kusamehewa au hili neno bado halijafikia mda wake, na kama bado, lini utimilifu wake.
 
Najiuliza sana, hivi Haya maovu nifanyayo sipati kusamehewa au hili neno bado halijafikia mda wake, na kama bado, lini utimilifu wake.

Mungu anasamehe kila kitu ila anachukia sana pale tunaporudia rudia dhambi,hili neno muda wake ndio sasa ndo maana akatuambia tuchague kuwa moto au baridi,ama uzima au mauti ,anachukia mtu wa vuguvugu na hapendezwi na mtu wa nia mbili.
 
Subiri, nieleze tena...
Aliye mtakatifu Na azidi kuwa mtakatifu..wapo watakatifu duniani saivi?
tuanze na hili..
 
Mungu alisema hataiangamiza dunia kwa moto tena! kama kipindi cha Sodoma na Gomora..wala.kwa maji kama kipindi cha Nuhu..wala kwa.magonjwa ya wamisri kipindi cha farao..maovu yamezidi sasa huwa natafakari dunia itajaangamizwa kwa style gani jamani sipati jibu..maana kama ni maasi na maobu ualiyotabiriwa yapo tunayaona..zinaa mauaji usaliti...tamaa..uongo n.k
kila mmoja ajiweke tayari maana hatujui siku wala saa..tutubu turejee huku tukimngoja
 
Back
Top Bottom