Labda nianze kwa kusema hivi usikubali daima nguvu ya kushindwa ikusemezeshe tena mara tu utakapomaliza kusoma post hii.
siku zote hofu ni adui wa binadamu na panapo hofu huwez hata kupata ujasiri wa kusimama mbele zawatu wengine na kuwaangalia na hata kupita mbele za watu.
uzuri wa maisha hata kama umekula leo ugali na deshi ukisimama hapo hakuna mtu atakaye jua ama hutakuwa tofauti na yule aliyekula ugali na kuku kwani wote mtakua mmeshiba. kwenye maisha uliish staili gani ya maisha ya kijijini leo hii hayana mashiko ingawa yatakufundisha tu ila hakuna anayeyaona manake hayajaandikwa usoni.
mie ninae andika hapa pengine nimekulia maisha ya dhiki kuliko hayo unayosema na leo hii natamba na kujiita gwiji la jiji kama huamini uliza wanajamvi......... nimekulia kijiji life kuskunti mwanzo mwisho tunakunywa chai kaanga na pondaponda lakin leo hii tuko utasema tulikulia masaki.
uzuri bana Mungu anajua hakuna hewa tofauti anayopumulia aliyekulia kwenye dhiki na anayopumulia aliyekuwa tajiri pia hakuna vitu ambavyo hivi vimetengenezwa kwa ajili ya matajiri tu ila bidii yako ndo itakusaidia kuvipata. sikiliza bro ukitaka kumiliki kiwanja city centre karibu na manji unaweza na ukitaka unapata wala haitaambia huyu kwakua alikuwa maskini basi asiuziwe hapana.
je toka umekuja dar ama chuon ulishawak kwenda dukan ukaambiwa hiki hatukuuzii kwasababu ulitoka kwenye familia ya dhiki? naamin hakuna basi achana na hayo mawazo. ili uondokane nayo fanya hivi
- ona kwamba maisha yako fair kwa ila mtu
- jipende sana tu na penda hali uliyo nayo and work hard
- pendelea kutoka na marafiki wa aina tofauti hata unakunywa kahawa tu inatosha ila itakupa confo.
- penda kusikilza wenzio wanapoongea na kama hukijui kitu nyamaza uwe msikilizaji tu ili kukwepa kuzodolewa.
- jijengee mazoea ya kusoma vitabu hasa novels, kuangalia tv kwenda cinema ili mradi uwe upto date basi
jua kabbisa kwamba kinachokusumbua wewe ni huko kujihisi uko nyuma hujui mambo mengi kisa ulilelewa kilage but unaweza kabisa kujiweka up to date kwa movies na news na vitabu. usije skia wenzio wakisema shwazniga ukasema ni dawa but unaweza kugoogle na kumjua hauyu shwazniga alikuwa mtu gani na anaafanya nini.
ondoa hofu jiweke up to date kila kitu kitaisha.