Plastic Surgery zitatumaliza

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,090
Hadithi za Biblia pamoja na Quran katika uimbaji wa mwanadamu zinanipa nafasi ya kipekee sana ya kuona uimbaji huu kuwa wa kipekee sana. kwa hakika mwenyezi Mungu ni mjuzi na ni sanifu namba moja. Hadithi hii imenifanya niandae makala hii ambayo kiukweli ninabakia na swali moja tu, Je tumerogwa ama ni nini kinachotuvuruga akili zetu wanadamu? Ni wiki kadhaa zimepata tokea habari za mrembo kutoka Kenya Vera Sidika ambaye ametoa ujumbe mzito kuhusu wale wanaohangaika na kwenda kuongeza baadhi ya sehemu zao za mwili, kuchonga pua, kuweka vipini kwenye ulimi, kuotesha vidoti, kufanyiwa upasuaji wa makalio ili yawe makubwa, kufanyiwa upasuaji wa matiti yaweze kujaa vyema yapate kukaa vyema kwenye sindiria, huku wengine wakienda mbali zaidi (Nadhani mnaelewa michezo hiyo).

ATTACH]


Harakati hizi kwa wanawake uangalia upande mmoja tu, kwenye MATOKEO tu na hawana muda wa kuangalia MADHARA yake, wengine hutamani wafanyiwe upasuaji ili wapate kuona matokeo aidha wakiwa na makalio makubwa yenye uduara, midomo mipana, ama matiti makubwa, lakini hawana muda wa kutathimini MADHARA, hawana muda wa kuelewa je upasuaji ukienda vibaya itakuwaje. Hichi ndicho kinachowatokea wadada warembo, mama zetu ambao bado hawaoni kama ni wazuri wakiwa vivyo hivyo na kutamani kwenda kufanya upasuaji. Utafiti uliofanywa na Hospitali ya South Florida unadai kuwa ndani ya miaka 14 iliyopita wanawake zaidi ya 24 wamepoteza maisha mara baada ya kufanya upasuaji wa kurekebisha makalio, ndani ya taifa la Marekani.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la wadada wanaotaka kufanyiwa upasuaji wa namna hii, Brazilian Butt Lift (BBL) ama kunyanyua makalio yawe kama wadada kutoka Brazil, huku vituo vya kufanyia upasuaji vikipata wanawake wengi.

ATTACH]


Kwa mujibu wa American Association of Plastic Surgeons (ASPS), unadai kuwa kati ya mwaka 2012 mpaka 2017 tu namba ya wanawake waliojitokeza kufanyia upasuaji huu uliongezeka mpaka kufikia asilimia 135. HATARI HII.
Lakini kizuri ni kwamba chama hii cha ASPS hutoa kabsa Angalizo huku wakifafanua hatari iliyoko mbeleni, na wakidai kuwa aina hii ya upasuaji ni hatari zaidi ya upasuaji wowote mara 20 zaidi. Kwa mwaka 2017, Waamerika walitumia zaidi ya dola bilioni 6.5 kwenye kufanya upasuaji wa miili yao, kurekebisha sehemu ya miili yao. Kuanzia upasuaji wa matiti yawe makubwa, upasuaji wa viini vya macho, pamoja upasuaji wa ngozi, bila kusahau makalio.

Moja kati ya athari za upasuaji huu ni Hematoma na Seroma kwa wale wenye kufanya upasuaji wa matiti na makalio, Kujeruhi neva za fahamu na kupoteza damu kwa wenye kufanya upasuaji wa midomo, makalio na hata midomo, maambukizi katika upasuaji wa macho na midomo, kujeruhi viungo haswa kwa wale wa upasuaji wa kuondoa kitambi na makalio, makovu, pamoja na kutokuridhika na matokeo mara baada ya upasuaji (Hii ni kwa wale walifanya upasuaji wa matiti na makalio).

Wasanii na watu maarufu nao hawapo nyuma kwenye utamaduni huu wa upasuaji wa mwili, hawa ni wachache tu ambao dunia imepata kuwaona na bado hatujajifunza hata kidogo.
Kenny Rogers
“On the warm summer’s evening on the train….. I made up with the gambler…….so I handle him my bottle, and drink my last swallow…..You got to know when to hold, know when to hold, know when to walk away”

ATTACH]


Mashairi matamu sana kutoka nyota wa muziki kwenye miondoko ya Country basi huyu Kenny Rogers alitamba sana miaka ya 1970s kwa sauti yake na gitaa lake. Huku watu wengi wakimpenda sana kwa muonekano wake, wakati huo alipamba majarida mengi tu kwa umaridadi wake, sura pamoja na sharafa na ndevu, lakini alivyoona uzee umeanza kumuondoa kwenye umaarufu basi akichukua kibunda chake na kwenda kufanya upasuaji wa mwili wake.

Kwa kuwa uzee ukamfanya awe na macho yaliyo na mikunjo, yeye akaona ni vyema ngozi ifanyiwe marekebisho na kuwa imara zaidi, hakuishia hapo, Kenny Rogers akaona ni vyema na macho ya uzee pia upasuaji ufanye kazi yake, hivyo akarekebisha na kiini cha jicho la kushoto na kulia ili asionekane mzee bali kijana. Lakini mwaka 2006 Kenny Rogers akiwa kwenye mahojiano na Jarida la People magazine kuhusu upasuaji wake alidai kuwa “I’m not happy about it” kwa tafsiri ya juu juu ni kuwa “Sina Furaha kuhusu hilo”.

Joan Rivers
Mwanamama mwingine ambaye naye pia aligeuza vituo vya afya kuwa makazi yake, kwa Mujibu wa Jarida la The Buzz wanadai kuwa alifanya upasuaji wa mwili wake kwenye maeneo zaidi ya matano. Alifanya upasuaji wa shingo ili kuondoa nyama na ngozi ili shingo iwe laini na yenye muonekano mzuri.

ATTACH]


Kisha akafanya upasuaji wa uso ambapo alifanya kuondoa makunyazi na hali ya uzee na akamaliza na kufanya upasuaji wa macho ili kuyafanya yawe mazuri zaidi, huku akidai kuwa alifanya upasuaji huo mara mbili ili apate macho mazuri. Ukimuangali unaweza kutamani kucheka ila ndo matokeo ya upasuaji wake wote alioufanya.

Donatella Versace
Hakuna ambaye hamfahamu Donatella Versace labda kama unavaa mavazi na bidhaa za Versace bila kufuatili kinachoendelea. Ukikutana na Donatella Versace kitu cha kwanza ambacho kitakutambulisha ni mdomo wake, sehemu ya mdomo ya juu ni mkubwa kuliko sehemu ya mdomo ya chini, kibailojia sehemu ya mdomo ya chini huwa ni kubwa kwa asilimia 50 kuliko wa sehemu ya mdomo ya juu. Ila kwa Donatella Versace ni tofauti nadhani picha inajieleza vyema, nadhani anajutia kabsa kufanya upasuaji wa aina hii.

ATTACH]


Pia ukiangalia ngozi ya Donatella Versace utaona ni ngozi yenye utofauti sana, ni ngozi ambayo sio yake ya kuzaliwa na Donatella Versace ana ngozi yenye kungaa fulani, hii sio athari za jua bali ni matibabu ya mionzi ambayo hufanya ngozi iendelee kuwa nyororo na ya kuvutia. Ila mambo yakaenda tofauti kwake, picha inajieleza vyema sana.

Michael Jackson
“……They goin to hurt you don’t ever come here… they don’t wanna see your face, you better disappear, the fire is in their eyes, so beat it just beat it….”

ATTACH]


Mfalme wa Pop duniani naye hakuwa nyuma kwenye hili, wengi historia yake kiundani zaidi. Michael Jackson alipunguza pua yake kubwa na kuifanya iwe ndogo, kisha kuweka ngozi yake iwe na rangi tofauti, huku akifanya upasuaji wa kuweka kidevu, alifanya mpaka upasuaji wa mdogo na mengi mengi zaidi. Michael Jackson ni mfano mzuri wa kile kinachoitwa body dysmorphic disorder (BDD) ila kwa ufupi ni kuwa Michael aliona mwili wake haupo sawa hivyo alifanya kila kitu ili tu apate mwili ambao ndani ya akili yake ndo ungekuwa mzuri machoni mwa watu. Au kwa lugha ya kitaalamu ni kuwa BDD ni hali ya kukosa utimamu wa akili ambapo mtu anashindwa kujiona vile ambavyo wengine wanamuona. Ni BDD ndo hufanya watu wengi kwenda kurekebisha miili yao wakidhani kuwa wanaonekana wabaya au hawavutii machoni mwa watu, wakati hata watu hawana dhana hiyo akilini mwao.

Jocelyn Wildenstein
Wengi wanamfahamu kama "Lion Woman of New York" mwanamama ambaye aliapa kufanya kila linalowezekana ili tu apate kurudiana na mume wake ambaye alimuacha, na katika vitu alivyofanya kwa ukamilifu na moyo mmoja ni upasuaji wa mwili wake. Alifanya upasuaji wa uso wake, kisha akachoma sindano kwa ajili ya kufanya mdomo uwe mzuri zaidi, akaona bado haitoshi akafanya upasuaji wa kupandikiza kidevu pamoja na mashavu, akafanya upasuaji wa macho huku akifanya upasuaji hatari wa macho unaoitwa kitaalamu “Canthopexy” upasuaji ambao unafanya macho yawe na muonekano wa macho ya paka.

ATTACH]


Jocelyn Wildenstein akafanya yote haya na bado mwanaume hakurudi akabaki na athari zake ambazo kiukweli amekuwa na uso wa ajabu kupita maelezo.

Heidi Montag
Ni maneno yapi yanafaa kumuelezea mwanamama Heidi Montag, mwanamama ambaye alifanya upasuaji wa mwili wake mara kumi ndani ya siku moja, na sasa anaonekana sio mtu tena bali ni kama mwanasesere aina ya Barbie Doll. Ukweli ni kwamba kufanya kwake upasuaji haukumpatia faida yoyote zaidi ya kumfanya we maarufu na umaarufu huo kumfanya aendelee kufanya upasuaji zaidi.

ATTACH]


Heidi Montag alifanya upasuaji wa kiuno, kisha akaenda kurekebisha komwe, kisha akarekebisha pua, na akaona haitoshi hivyo akafanya upasuaji wa kuongeza mashavu yake, huku akifanya tena upasuaji wa kupunguza kidevu, akafanya upasuaji wa shingo, na kurudisha masikio nyuma kiasi. Heidi Montag akaona bado haitoshi hivyo akafanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti kwa mara ya pili, na kiuno, pamoja na nyonga pamoja na kuongeza ukubwa wa makalio.
Heidi Montag mwenyewe anakiri kuwa alikosea sana kufanya upasuaji wote huo, huku kwa sasa akitaabika na maumivu makubwa ya makovu pamoja na watu kumponda na kumpa jina la Barbie Doll, aliongeza kwa uchungu sana wakati akifanya mahojiano na jarida la told Life & Style Weekly.

Mickey Rourke

ATTACH]


Bwana Mkubwa huyu alifanya upasuaji wa aina tatu tofauti, kwanza alifanya upasuaji wa uso ili kuondoa makunyazi ya uzee, kisha akafanya upasuaji wa sehemu ya juu za macho yake huku akimaliza na upasuaji wa kupandikiza nywele. Kwa mujibu wa madakatari wa upasuaji wanadai kuwa upasuaji wa uso ukienda ndivyo sivyo basi unaweza kumpeleka mgonjwa kuchubuka uso wote, na hichi ndicho kilichotokea kwa Mickey Rourke ambaye uso wake umekutana na dhahama hiyo.

ATTACH]


Uwiano wa muonekano wa Mickey Rourke baina ya masikio na mashavu yake ni tofauti sana na ni ishara ya upasuaji wa uso ambao umekwenda vibaya sana na hakuna namna Mickey Rourke inambidi kuishi namna hiyo.

Carrot Top
Bwana Mkubwa Carrrot naye hakuwa nyuma na mkumbo huu maarufu duniani, huku kwa sasa akionekana kama kituko fulani hivi, sawa na mfano wa mhusika kwenye filamu za Vikaragosi (Cartoon). Huyu muigizaji alifanya upasuaji wa uso kisha akafanya matibabu ya uso wake kwa kutumia mionzi ili apate uso angavu sana. na amefanya upasuaji kwenye kila kiungo kwenye uso wake kasoro macho tu.

ATTACH]


Alifanya hivi ili aendelee kupata nafasi ya kushiriki kwenye filamu na tamthilia mbalimbali lakini kwa sasa anapata simu nyingi na nafasi za kwenda kuwa mshiriki kwenye filamu za kuchekesha watoto, na huyu hana haja ya kupakwa make-up maana muonekano wake tayari una make-up.

Priscilla Presley
Mtandao kuna swali, Je Marehemu Elvis anegpata nafasi ya kumuona Priscilla alivyo leo ingekuwaje? Kwa hakika angepatwa na mshagao mkubwa sana. Ni miaka kadhaa nyuma Priscilla alipofanya upasuaji wa uso wake pamoja na kuchoma sindano ya silicone kwenye mashavu yake. Hii inajieleza vyema kwa uso wake ulivyo sasa hivi, uso ambao umevimba haswa.

ATTACH]


Basi silicone haikutosha kumpa urmbo ambao alitamani kuwa nao, hivyo Priscilla akiongeza na matibabu ya mionzi pamoja na Botox, na hivi vikatosha kumfanya awe na ngozi angavu kweli kama mshumaa.

Jennifer Grey

ATTACH]


Jennifer Grey ni mfano bora sana wa upasuaji wa pua ambao umekwenda tofauti na matarajio yake. Jennifer alifanya upasuaji wa kurekebisha na kuondoa sehemu ya pua yake ambayo kitaalamu inaitwa dorsal hum, huku upasuaji huu ukimpatia muonekano wa tofauti zaidi, ingawa kwenye filamu mbalimbali watu walivutiwa sana na pua ya Jennifer ila yeye binafsi aliona aifanyie marekebisho. Ila kwa sasa haitaki tena.

Mwisho:
Sina nia yoyote mbaya ya kumkejeli mtu bali ni katika namna ya kuelekezana vile vitu ambavyo katika jamii yetu havina msingi wala faida. Ni wazi kuwa wanaume wengi wanavutiwa na wanawake wenye maumbo mazuri, ila pia kuna wanaume ambao na wao wanapenda wenye maumbo madogo, wanapenda mwanamke wenye matiti madogo, ama wenye kifua kidogo, na wakati huo huo wapo kina Dj Choka ambao wao ni heavyweight wanapenda vitu vizito, wanawake wenye makalio makubwa pamoja na matiti makubwa. Lakini yote hii haina maana kwamba uende kuweka hatarini maisha yako kisa tu fulani anapenda kukuona ukiwa na Makalio kama Sanchi World ama fulani. Usiende kuchoma sindano ya kuongeza matiti kisa tu fulani anapenda kukuona ukiwa na kifua kikubwa.

ATTACH]


Kumbuka kila mtu ana ladha yake na matamanio yake, kama fulani hapendi muonekano wako basi nenda kwa mtu ambaye atakupokea kwa mikono miwili na kukupenda jinsi ulivyo, hakuna haja ya kumkosoa Mungu kwenye kazi yake ya Uumbaji, acha kabsa, ridhika na namna Mungu alivyokusanifu, kama una matiti madogo kama karanga wewe ridhika nayo, kuna mtu atakupenda kwa matiti hayo hayo, na kama una matiti makubwa kama fenesi basi ridhika na kifua chako kwa sababu kuna watu kama Dj Choka wanapenda vitu hivyo.

ATTACH]


Usibadilishe chochote kwenye mwili wako kwa sababu ya watu, ili upate kupewa sifa kama uko mrembo kumbe athari zinakugonjea mlangoni tu. Ninaandika makala hii huku moyo wangu ukiwa na uchungu mkubwa sana, hivi sasa mdada ambaye hana makalio makubwa anajiona kama mlemavu tena mlemavu asiyejiamini kabsa na umbo lake, mdada kama hana kifua kipana basi hujiona kama havutii. Mhubiri mmoja aliwahi kusema “Pendezesha roho kwanza kwa matendo mazuri ndipo uanze kufikiria muonekano wa mwili wako”.
“You’re Beautiful Just The Way You’re”
Hatma ya Maisha yako iko mkononi mwako! Mungu akubariki sana!
Naomba kuwasilisha Andiko!
 

Attachments

  • images%20(27).jpg
    images%20(27).jpg
    39.2 KB · Views: 16
  • images%20(8).jpg
    images%20(8).jpg
    60.9 KB · Views: 17
Back
Top Bottom