Pixel: Mfalme wa Chromebook

Pixel: Mfalme wa Chromebook

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
Ubora
+ Ina Skrini yenye kuongoza duniani kwa ppi
+ Mnunuzi anapata 1TB ya Google Drive kwa miaka 3
+ Ina boot kwa wastani wa sekunde 8

Udhaifu
- Chrome OS bado ni ngeni kwa wengi
- Inatumika kwenye Mawingu (Cloud) tu hivyo lazima uwe na intanet
- Bei ni ghali mno kwa kompyuta ya aina hii

Chrome book ni kompyuta ambazo kwa maoni yetu zimetangulia kiwango cha teknolijia cha nchi nyingi duniani, sababu ni kwamba Chromebook ni kompyuta ambazo asilimia kubwa ya programu na data wakati wa matumizi huhifadhiwa kwenye mawingu (cloud) badala ya kompyuta yenyewe, hivyo ni kawaida kabisa kuona kompyuta za chromebook zina diski ya ndani yenye ukubwa wa 16GB. Iwapo huna intanet basi kompyuta hii ni vigumu kuitumia, vile vile ni kompyuta ambayo haina mambo mengi ambayo unaweza kuyafanya kutokana na ukosefu wa apps/program za hali ya juu, ingawa kwa matumizi ya kawaida tunaweza kusema laptop hii karibu inatimia.

Hata hivyo Google Chromebook Pixel ni miongoni mwa laptop ambazo zinajaribu kusukuma mauzo ya kompyuta zinazotumia OS ya Chrome na ina sifa nyingi za kompyuta ya hali ya juu. Awali imebuniwa kwa umbile lenye kuvutia mno, tangu Apple kuanza kutumia skrini za retina katika MacBook, Chromebook Pixel ni kompyuta ya kwanza kutoka ikiwa na rezolushani bora kuliko za MacBook zenye kioo cha retina, Chromebook Pixel ina 239 ppi ambapo MacBook Pro Retina 15” ina 220 ppi na 13” ina 227 ppi. Kioo cha Chromebook Pixel kina ukubwa wa 13”.

Ubora wa maumbile na kioo kinachoonyesha picha yenye maelezo na muonekano wa hali ya juu sio uzuri pekee wa Chromebook Pixel, kompyuta hii pia ina kioo aina ya Gorilla, vioo ambavyo vina sifa ya umadhubuti na pia ni kioo cha kugusa (touch screen). Chromebook vile vile ni laptop ya kwanza yenye teknolojia ya 4G LTE.

Mbali na hayo Chrombook pixel ina disk aina ya SSD (Solid State Drive) ambazo zina kasi zaidi ya HDD za kawaida, disk hiyo ina nafasi ya 32GB. Inatumia prosesa aina ya Intel Core i5 yenye kasi ya 1.8 GHz na core mbili huku ikiambatanishwa na kadi ya graphics aina ya Intel HD 4000. Kwa vile hii ni kompyuta ya kutumia kwa mawingu (cloud) Google inatoa 1TB Google Drive kwa kila mnunuzi wa kompyuta hii kwa muda wa miaka mitatu.

Laptop hii pia ina RAM kiasi cha 4GB na Kamera yenye uwezo wa HD 720p. Betri yake inakisiwa kudumu masaa matano kwa mtumiaji wa kawaida. Mauzo ya Chromebook yamekuwa wakiripotiwa kuwa ni madogo pamoja na kuwa na bei nafuu mno, je Google Chromebook Pixel itaweza kunyanyua mauzo ya kompyuta za aina hii? Pamoja na uzuri wa kiasi kompyuta hii huenda bei ikwa ndio kikwazo kikubwa kwa vile inauzwa kwa jumla ya £1,049 ambazo ni sawa na TSh 2,571,265.43, ukizingatia kwamba unaweza kufanya matumizi ya Chromebook kwa kutumia browser ya Google Chrome na kudownload apps zake, hatuelewi Google wanatarajia ni vipi watu watanunua kompyuta hii!

Chanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia

Bongo bado sana kunubua kutu kama hii, Network zetu bado ni ghali na ni slow kama kinyonga mlemavu, hata ukipewa 5GB za Google Drive huwezi zijaza.
 
Bongo bado sana kunubua kutu kama hii, Network zetu bado ni ghali na ni slow kama kinyonga mlemavu, hata ukipewa 5GB za Google Drive huwezi zijaza.

lol sio bongo dunia nzima ni ghali labda mtu uwe mpuuzi huwezi toa milion 2 kununua browser
 
Hapa nakubaliana na nyinyi kuwa kompyuta hii ina matatizo mawili yaani bei na jinsi ya kuitumia (internet), Hata ukiwa unaishi kwenye nchi zenye speed nzuri ya internet bado unaweza ukawa sehemu ambayo huna internet labda ufanye teathering au uweke sim card ambapo ni gharama nyingine tena. Na kama umezoea 30 - 50 mb speed teathering inaboa mno mpaka uwe na 4G ambapo mpaka sasa ni ghali mno.

Nadhani Google wenyewe wanalenga kuzitangulia kampuni nyingine kwenye mafanikio ya cloud kwa miaka ya baadae, ndio maana wanaendelea kuzi-push computer hizi. Huenda teknolojia hii ikipevupa na kukubalika basi wao tayari watakuwa wameshazitangulia kampuni nyingi na OS zote kwa mafanikio ya kompyuta za mtindo huu. 4G LTE na teathering cost itakaposhuka huenda watu wakaanza kuzikubali ingawa sio kwa bei hii. hata hivyo zipo chromebook za bei rahisi mno. (£200)

Kwa sasa baadhi ya kampuni kubwa katika nchi zilizoendelea zimeanza kutumia cloud computing kwa kiwango kikubwa kwa sababu ya data safety na universal data access (yaani huhitaji kuwa kwenye computer fulani ili kuzipata data fulani) Google inazizidi kampuni nyingi za tech kwa future forecast.

Tusubiri ni wakati tu ndio utakatujulisha kama Google wataweza kuuteka ulimwengu wa laptop kama walivyofanya kwenye simu mpaka sasa.
 
mkuu zipo hadi za dola 199 very cheap. Mi nafkiri google anatakiwa azieke kimedia zaidi ziwe kama tablet. Sababu chrome sio nzito kama android so specs ndogo inarun vizuri unaeka storage kubwa mtu anaingia net na kucheki media zake. Akifanya hivyo ataniteka na mi ntakua mteja wake
 
Back
Top Bottom