WISE 2012
JF-Expert Member
- Mar 13, 2012
- 634
- 460
Kuna siku nilichelewa kurudi nyumbani!dingi akanikata stick nyingi sana akaniambia hakuna kula mchana!mtembezi hula miguu yake,afu mama ndio alikua anaepua maharage jikono na kitu cha wali kilikua tayari chini kinanukia hatari!!haya bna nikaenda kulala kwa huzuni kubwaaa sana huku tumbo likinguruma kwa njaa!!watu wakala wakamaliza mk nikajipitisha ili hata mzee anionee huruma nile lakini wap!!Nikashangaa mama ananiita kwa Hasira,We kuja hapa Pumbavu wewe Chukua hyo ndoo hapo uende ukachote maji!!nikazidi kuumia kuona mama nae ananipa kazi na njaa yote ile!!basi nikasepa kinyonge nikiwa njiani nikahisi kwenye ndoo kuna kitu kufungua hivi nakutana na bakuli kubwa limejaa Waliiiiii kwanza nililia kidogo kwa furaha then nikaula fasta HAPPY WOMEN'S DAY