Pitia hapa ujifunze kulinda biashara yako

Mzigdash

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
440
375
Habari!

Je biashara yako ni ya aina gani?

Je ni biashara ambayo huwezi kuifanya katika muda wote wa mwaka? ikiwa jibu ni NDIYO, basi biashara yako ni ya MSIMU.

Je msimu wa biashara unapokwisha (kipindi mauzo yanapokuwa madogo) unafanya nini?

Haya ni mambo muhimu ya kupitia na kujifunza.
naomba kuwasilisha, karibuni pia kwa kuchangia na kuongeza mengine

1. Dhibiti mtiririko wako wa pesa vizuri(cash flow management)

2. Jitahidi kuweka akiba hasa kipindi biashara inapokuwa nzuri (boom stage). Akiba hii unaweza kuitumia kuinvest kitu kingine kipindi msimu wa biashara unapokwisha.

3.Usiajiri wafanyakazi wapya mwisho wa msimu.

4. Kuwa na mikataba ya muda mfupi na wafanyakazi wako, ukilenga mwisho wa mkataba uwe ni kipindi msimu unapomalizikia. Ishi na wafanyakazi hao vizuri, ili uweze kuwaajiri tena msimu unapoanza ili kuepuka gharama kuajiri "watu wapya" kabisa ambapo utahitaji gharama kubwa kuwa-train.

5. Hakikisha unadumisha mawasiliano na wateja wako katika kipindi kisicho cha msimu ili msimu unaporudi usianze moja kutafuta wateja.

6.Punguza matumizi (expenditures)

7. Wakati unapoona msimu unakaribia kwisha , anzisha biashara ndogo ndogo ambayo ina uhusiano na biashara yako kuu au isiyo na uhusiano.

8. Ukiwa ndio unaanza biashara, na biashara yako ni ya msimu, Fanya forecasting kwa kuangalia data za mauzo kutoka kwa marafiki au watu wafanyao biashara kama hiyo. hii itasaidia kujua ununue mzigo wa kiasi gani ambao utauuza hadi mwisho wa msimu bila kubakia na kuingia hasara.

9. Fanya store management, hakikisha unajuwa kilichopo store: kiasi gani kipo, expire date. Hii itasaidia kuepukana na hasara.
 
Noted!
 
Na kama mkuu biashara yako aina msimu kwamfano biashara ya chakula mama ntilie
 
Back
Top Bottom