makilo
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 2,679
- 5,387
STORY FUPI INAYOFUNZA SANA Miaka 10 ya ndoa yetu siku
moja niliingia
nyumbani nikamkuta mke
wangu akiniandalia
chakula cha usiku. Nilimshika
mkono na kumwambia: “Nina jambo
ninalotaka
kukueleza.” Alikaa na
kunisikiliza kwa makini.
Dalili za wasiwasi nilikuwa
nikizishuhudia machoni mwake. Ghafla nilijikuta
katika hali ya kushindwa
kukifungua kinywa changu.
Lakini ilikuwa ni
lazima ajue ninachokifikiria,
hivyo nilipiga moyo konde, nikamwambia kwa
upole: “Ninataka
tuachane.” Hakuonekana
kuudhika kwa hoja
niliyokuwa nimeiwasilisha
mbele yake, bali aliniuliza kwa sauti ya upole kabisa:
“Kwa nini?” Nilijaribu
kulikwepa hilo swali, hivyo
alighadhibika sana na
kuniambia kwa sauti ya
juu: “Wewe si mwanaume!” Usiku ule
hatukusemeshana, na muda
wote alikuwa
akilia. Nilitambua kuwa
alitaka kujua kitu gani
kimetokea katika ndoa yetu. Lakini sikuweza kumpa jibu
lenye kuridhisha; kwa sababu
sikuwa na mapenzi naye
tena, moyo wangu
ulikuwa umetekwa na binti
mwingine aitwaye Jane. Nilimsikitikia sana!
Huku nikiwa na hisia za hatia
moyoni mwangu,
niliandika pendekezo la
talaka ambalo lilieleza
kuwa atachukua nyumba yetu, gari na shea ya
asilimia 30 ya kampuni
yangu. Mke wangu
aliitazama karatasi hiyo kisha
akaichana na
kuitupa kwenye ndoo ya takataka. Huyu ni mwanamke
aliyekuwa ameishi nami kwa
muda
wa miaka kumi alikuwa
amegeuka kuwa kama
mgeni kwangu. Nilisikitika sana na kumuomba
radhi kwa kumpotezea muda,
rasilimali na
nguvu zake lakini sikuweza
kutengua kauli
yangu kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana Jane na
nilikuwa nimezama kweli
kweli ndani ya
huba lake na kuwa teja wa
penzi lake. Hatimaye
alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo
nilikuwa nikitarajia kuliona.
Kilio chake kwangu
kilikuwa kama faraja. Wazo
la talaka
lililonitawala kwa wiki kadhaa lilikuwa likizidi
kupata nguvu na sasa
lilionekana kuwa wazi
kabisa. Siku iliyofuata nilirudi
nyumbani nikiwa
nimechelewa na kumkuta akiandika kiandika
kitu mezani. Sikutaka kula
chochote zaidi ya
kuelekea moja kwa moja
kitandani kwa sababu
nilikuwa nimechoka sana kutokana na
mishemishe za siku hiyo
nikiwa na Jane. Niliposhtuka,
bado alikuwa hajatoka
mezani.
Sikujali hata kidogo, nikageuka na kuendelea
kuuchapa usingizi. Asubuhi
alinipatia masharti ya talaka:
hakutaka
mali yoyote kutoka kwangu,
bali alitaka kuwe na muhula wa mwezi mmoja
kabla ya talaka.
Alitaka kwamba katika
kipindi hicho tujaribu
kuishi kama kawaida kwa
kadiri iwezekanavyo. Hoja yake ilikuwa wazi:
mtoto wetu alitarajia kufanya
mitihani ya shule ndani ya
mwezi huo
na hakutaka tumchanganye
kwa tukio la talaka. Hili nililikubali. Lakini alikuwa na
nyongeza:
alinitaka nikumbuke siku ya
ndoa yetu
nilipomnyanyua kumpeleka
chumbani kwetu. Alitaka kwamba katika
kipindi hicho cha mwezi
mzima niwe nambeba kila
siku asubuhi kumtoa
chumbani mpaka mbele ya
mlango wa nje ya nyumba. Nilihisi kuwa alikuwa
ameshikwa na
wendawazimu. Nilikubali
ombi lake kwa sababu
niliona kuwa mwezi mmoja
sio kitu, kwani nilitaka tuachane.
Nilimsimulia Jane kuhusu
masharti ya talaka
yaliyotolewa na mke wangu.
Alicheka sana na
kuona kuwa ni upuuzi. “Hata akitumia hila gani
lazima apewe talaka,”
alisema Jane kwa
masihara. Tangu nilipoelezea
nia yangu ya
kutaka kuachana naye, hatukuwa na uhusiano wa
kimwili na mke wangu. Hivyo
nilipombeba
siku ya kwanza, sote
tulionekana kutokuwa na
uchangamfu. Mtoto wetu alifurahi na kupiga
makofi: “Baba amembeba
mama”. Kauli yake
ilinipa maumivu moyoni.
Kutoka chumbani
mpaka barazani, kisha mlangoni, nilitembea mita
kumi nikiwa nimembeba
mikononi
mwangu. Aliyafumba macho
yake na kuniambia
kwa upole na ulaini: “Usimwambie mtoto wetu
kama tunaachana.” Nilikubali
kwa kutikisha kichwa huku
nikiwa
nimefadhaika. Nilipofika nje
nilimshusha akaenda kituoni kusubiri basi,
nami nikachukua
gari langu na kwenda ofisini
nikiwa peke yangu. Siku ya
pili tulijaribu kutoonesha hali
yoyote ya mifarakano. Aliegemea
kifuani kwangu nikahisi
manukato mazuri ya blauzi
yake. Nilibaini kuwa
sikuwa nimemtazama vizuri
mke wangu kwa muda mrefu. Uso wake
ulikuwa umeanza kuwa
na mikunjo na nywele zake
zilikuwa zimeanza
kubadilika. Ndoa yetu ilikuwa
imemfanya achoke. Kwa dakika kadhaa
niliduwaa na
kuwaza kile nilichokuwa
nimemfanyia. Siku ya nne
nilipombeba nilihisi aina ya
ukaribu na mvuto ikirejea. Huyu ni
mwanamke
aliyekuwa amenipa miaka
kumi ya uhai na
maisha yake. Siku ya tano na
ya sita, kwa mara nyingine, niliona hali ya ukaribu na
mvuto fulani ikirejea
kati yetu. Sikumsimulia Jane
kuhusu hali hii.
Kadiri siku zilivyosonga mbele
ndivyo nilivyozidi wepesi wa kumbeba.
Yumkini ilisababishwa na
ile hali ya kumbeba kila siku
kiasi cha kumuona kuwa ni
mwepesi. Asubuhi moja
alikuwa akichagua nguo ya kuvaa. Alijaribu nguo kadhaa
lakini hakupata
inayomfaa. Alishusha pumzi
na kusema: “Nguo
zangu zote hazinienei,
zimekuwa kubwa”. Nilibaini kuwa alikuwa
amekonda na ndiyo
maana niliweza kumbeba
kwa urahisi. Nilisikitika kwa
sababu nilihisi kuwa alikuwa
amebeba mambo mengi moyoni mwake. Hivyo
nilimsogelea na kukipapasa
kichwa chake. Ni wakati huo
ambapo mtoto wetu aliingia
na
kusema: “Baba sasa ni muda wa kumbeba
mama”. Tukio la kumuona
baba yake akiwa
amembeba mama yake
lilimuathiri na kuwa
sehemu muhimu sana ya maisha yake. Mke
wangu alimuita na
kumkumbatia kwa upendo.
Niligeuza uso wangu
pembeni, sikutaka
kuangalia tukio hilo nisinje nikabadilisha
uamuzi wangu wa talaka.
Nilimnyanyua na
kumbeba mke wangu,
nikatembea kutoka
chumbani, sebuleni mpaka nje. Aliizungusha
mikono yake mizuri shingoni
kwangu, nami nikamshikilia
vizuri; ilikuwa kana kwamba
ni
siku ile ya harusi yetu. Lakini wepesi wa mwili
wake ulinifanya niwe
mwenye huzuni. Siku ya
mwisho nilipombeba
niliingiwa na uzito
wa kupiga hatua. Wakati huo mtoto wetu tayari
alikuwa shule. Nilimshikilia
vizuri na kusema:
“Sikuwa nimejua kuwa
maisha yetu yamekosa
mvuto”. Niliwasha gari kuelekea ofisini,
niliamua kupita kwa Jane.
Nilipofika nilitoka haraka bila
hata kuubana mlango wa
gari.
Nilikuwa na wasiwasi nisije nikaghairi nia
yangu… nikapandisha ngazi.
Jane alipofungua
mlango nilimwambia:
“Samahani Jane, sitaki
kuachana na mke wangu”. Alinitazama kwa mshtuko na
kunigusa kwenye
paji la uso. “Una homa?”
alisema. Niliutoa
mkono wake na
kumwambia: “Samahani Jane, sitaki kumuacha mke wangu.
Yawezekana
maisha yangu na mke wangu
yalikosa
uchangamfu kwa sababu
hatukuwa karibu, sio kwa sababu hatukupendana. Sasa
nimebaini
kwamba kwa kuwa
nilimbeba siku ya ndoa yetu,
ninapaswa kuendelea
kufanya hivyo mpaka kifo kitutengenishe.” Jane
alionekana kushtuka
sana. Alinizaba kibao,
akaubamiza mlango na
kuanza kulia. Nilimuacha
nikapanda gari na kuondoka. Njiani
nilipita kwenye duka la maua
nikaagiza shada la
maua kwa ajili ya mke
wangu. Muuzaji
akaniuliza ujumbe unaotakiwa kuandikwa juu
ya kadi nikatabasamu na
kumwambia aandike:
“Kila siku asubuhi nitakubeba
mpaka kifo kitakapotutenga
nisha”. Jioni nilifika nyumbani nikiwa na maua
mkononi, tabasamu usoni,
nikapandisha ngazi
mpaka ndani. Nilipofika
chumbani mke wangu
alikuwa amelala akiwa amefariki dunia. Kumbe
alikuwa akipambana na
KANSA kwa miezi
kadhaa lakini sikujua kwa
sababu nilikuwa nimetekwa
na Jane. Bila mimi kufahamu, kumbe marehemu mke
wangu alijua kwamba
muda si mrefu atafariki dunia
na alitaka
kuniokoa dhidi ya fikra
yoyote mbaya kutoka kwa mtoto wetu kama
tungeachana muda mfpi
kabla ya kifo chake. Angalau
machoni mwa mwanangu
naonekana kuwa mume
mwenye upendo… WAPENDANAO NATAKA
MJIFUNZE 1) Wengi wanatengana si
kwa sababu
hawapendani, bali hawapeani
muda wa
kusikilizana. 2)Wengi wanaamini
ukiachana na mpendwa
wako ni lazima muwe
maadui. 3)Busara ndani ya pendo ni
zaidi ya mali na
pesa......
moja niliingia
nyumbani nikamkuta mke
wangu akiniandalia
chakula cha usiku. Nilimshika
mkono na kumwambia: “Nina jambo
ninalotaka
kukueleza.” Alikaa na
kunisikiliza kwa makini.
Dalili za wasiwasi nilikuwa
nikizishuhudia machoni mwake. Ghafla nilijikuta
katika hali ya kushindwa
kukifungua kinywa changu.
Lakini ilikuwa ni
lazima ajue ninachokifikiria,
hivyo nilipiga moyo konde, nikamwambia kwa
upole: “Ninataka
tuachane.” Hakuonekana
kuudhika kwa hoja
niliyokuwa nimeiwasilisha
mbele yake, bali aliniuliza kwa sauti ya upole kabisa:
“Kwa nini?” Nilijaribu
kulikwepa hilo swali, hivyo
alighadhibika sana na
kuniambia kwa sauti ya
juu: “Wewe si mwanaume!” Usiku ule
hatukusemeshana, na muda
wote alikuwa
akilia. Nilitambua kuwa
alitaka kujua kitu gani
kimetokea katika ndoa yetu. Lakini sikuweza kumpa jibu
lenye kuridhisha; kwa sababu
sikuwa na mapenzi naye
tena, moyo wangu
ulikuwa umetekwa na binti
mwingine aitwaye Jane. Nilimsikitikia sana!
Huku nikiwa na hisia za hatia
moyoni mwangu,
niliandika pendekezo la
talaka ambalo lilieleza
kuwa atachukua nyumba yetu, gari na shea ya
asilimia 30 ya kampuni
yangu. Mke wangu
aliitazama karatasi hiyo kisha
akaichana na
kuitupa kwenye ndoo ya takataka. Huyu ni mwanamke
aliyekuwa ameishi nami kwa
muda
wa miaka kumi alikuwa
amegeuka kuwa kama
mgeni kwangu. Nilisikitika sana na kumuomba
radhi kwa kumpotezea muda,
rasilimali na
nguvu zake lakini sikuweza
kutengua kauli
yangu kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana Jane na
nilikuwa nimezama kweli
kweli ndani ya
huba lake na kuwa teja wa
penzi lake. Hatimaye
alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo
nilikuwa nikitarajia kuliona.
Kilio chake kwangu
kilikuwa kama faraja. Wazo
la talaka
lililonitawala kwa wiki kadhaa lilikuwa likizidi
kupata nguvu na sasa
lilionekana kuwa wazi
kabisa. Siku iliyofuata nilirudi
nyumbani nikiwa
nimechelewa na kumkuta akiandika kiandika
kitu mezani. Sikutaka kula
chochote zaidi ya
kuelekea moja kwa moja
kitandani kwa sababu
nilikuwa nimechoka sana kutokana na
mishemishe za siku hiyo
nikiwa na Jane. Niliposhtuka,
bado alikuwa hajatoka
mezani.
Sikujali hata kidogo, nikageuka na kuendelea
kuuchapa usingizi. Asubuhi
alinipatia masharti ya talaka:
hakutaka
mali yoyote kutoka kwangu,
bali alitaka kuwe na muhula wa mwezi mmoja
kabla ya talaka.
Alitaka kwamba katika
kipindi hicho tujaribu
kuishi kama kawaida kwa
kadiri iwezekanavyo. Hoja yake ilikuwa wazi:
mtoto wetu alitarajia kufanya
mitihani ya shule ndani ya
mwezi huo
na hakutaka tumchanganye
kwa tukio la talaka. Hili nililikubali. Lakini alikuwa na
nyongeza:
alinitaka nikumbuke siku ya
ndoa yetu
nilipomnyanyua kumpeleka
chumbani kwetu. Alitaka kwamba katika
kipindi hicho cha mwezi
mzima niwe nambeba kila
siku asubuhi kumtoa
chumbani mpaka mbele ya
mlango wa nje ya nyumba. Nilihisi kuwa alikuwa
ameshikwa na
wendawazimu. Nilikubali
ombi lake kwa sababu
niliona kuwa mwezi mmoja
sio kitu, kwani nilitaka tuachane.
Nilimsimulia Jane kuhusu
masharti ya talaka
yaliyotolewa na mke wangu.
Alicheka sana na
kuona kuwa ni upuuzi. “Hata akitumia hila gani
lazima apewe talaka,”
alisema Jane kwa
masihara. Tangu nilipoelezea
nia yangu ya
kutaka kuachana naye, hatukuwa na uhusiano wa
kimwili na mke wangu. Hivyo
nilipombeba
siku ya kwanza, sote
tulionekana kutokuwa na
uchangamfu. Mtoto wetu alifurahi na kupiga
makofi: “Baba amembeba
mama”. Kauli yake
ilinipa maumivu moyoni.
Kutoka chumbani
mpaka barazani, kisha mlangoni, nilitembea mita
kumi nikiwa nimembeba
mikononi
mwangu. Aliyafumba macho
yake na kuniambia
kwa upole na ulaini: “Usimwambie mtoto wetu
kama tunaachana.” Nilikubali
kwa kutikisha kichwa huku
nikiwa
nimefadhaika. Nilipofika nje
nilimshusha akaenda kituoni kusubiri basi,
nami nikachukua
gari langu na kwenda ofisini
nikiwa peke yangu. Siku ya
pili tulijaribu kutoonesha hali
yoyote ya mifarakano. Aliegemea
kifuani kwangu nikahisi
manukato mazuri ya blauzi
yake. Nilibaini kuwa
sikuwa nimemtazama vizuri
mke wangu kwa muda mrefu. Uso wake
ulikuwa umeanza kuwa
na mikunjo na nywele zake
zilikuwa zimeanza
kubadilika. Ndoa yetu ilikuwa
imemfanya achoke. Kwa dakika kadhaa
niliduwaa na
kuwaza kile nilichokuwa
nimemfanyia. Siku ya nne
nilipombeba nilihisi aina ya
ukaribu na mvuto ikirejea. Huyu ni
mwanamke
aliyekuwa amenipa miaka
kumi ya uhai na
maisha yake. Siku ya tano na
ya sita, kwa mara nyingine, niliona hali ya ukaribu na
mvuto fulani ikirejea
kati yetu. Sikumsimulia Jane
kuhusu hali hii.
Kadiri siku zilivyosonga mbele
ndivyo nilivyozidi wepesi wa kumbeba.
Yumkini ilisababishwa na
ile hali ya kumbeba kila siku
kiasi cha kumuona kuwa ni
mwepesi. Asubuhi moja
alikuwa akichagua nguo ya kuvaa. Alijaribu nguo kadhaa
lakini hakupata
inayomfaa. Alishusha pumzi
na kusema: “Nguo
zangu zote hazinienei,
zimekuwa kubwa”. Nilibaini kuwa alikuwa
amekonda na ndiyo
maana niliweza kumbeba
kwa urahisi. Nilisikitika kwa
sababu nilihisi kuwa alikuwa
amebeba mambo mengi moyoni mwake. Hivyo
nilimsogelea na kukipapasa
kichwa chake. Ni wakati huo
ambapo mtoto wetu aliingia
na
kusema: “Baba sasa ni muda wa kumbeba
mama”. Tukio la kumuona
baba yake akiwa
amembeba mama yake
lilimuathiri na kuwa
sehemu muhimu sana ya maisha yake. Mke
wangu alimuita na
kumkumbatia kwa upendo.
Niligeuza uso wangu
pembeni, sikutaka
kuangalia tukio hilo nisinje nikabadilisha
uamuzi wangu wa talaka.
Nilimnyanyua na
kumbeba mke wangu,
nikatembea kutoka
chumbani, sebuleni mpaka nje. Aliizungusha
mikono yake mizuri shingoni
kwangu, nami nikamshikilia
vizuri; ilikuwa kana kwamba
ni
siku ile ya harusi yetu. Lakini wepesi wa mwili
wake ulinifanya niwe
mwenye huzuni. Siku ya
mwisho nilipombeba
niliingiwa na uzito
wa kupiga hatua. Wakati huo mtoto wetu tayari
alikuwa shule. Nilimshikilia
vizuri na kusema:
“Sikuwa nimejua kuwa
maisha yetu yamekosa
mvuto”. Niliwasha gari kuelekea ofisini,
niliamua kupita kwa Jane.
Nilipofika nilitoka haraka bila
hata kuubana mlango wa
gari.
Nilikuwa na wasiwasi nisije nikaghairi nia
yangu… nikapandisha ngazi.
Jane alipofungua
mlango nilimwambia:
“Samahani Jane, sitaki
kuachana na mke wangu”. Alinitazama kwa mshtuko na
kunigusa kwenye
paji la uso. “Una homa?”
alisema. Niliutoa
mkono wake na
kumwambia: “Samahani Jane, sitaki kumuacha mke wangu.
Yawezekana
maisha yangu na mke wangu
yalikosa
uchangamfu kwa sababu
hatukuwa karibu, sio kwa sababu hatukupendana. Sasa
nimebaini
kwamba kwa kuwa
nilimbeba siku ya ndoa yetu,
ninapaswa kuendelea
kufanya hivyo mpaka kifo kitutengenishe.” Jane
alionekana kushtuka
sana. Alinizaba kibao,
akaubamiza mlango na
kuanza kulia. Nilimuacha
nikapanda gari na kuondoka. Njiani
nilipita kwenye duka la maua
nikaagiza shada la
maua kwa ajili ya mke
wangu. Muuzaji
akaniuliza ujumbe unaotakiwa kuandikwa juu
ya kadi nikatabasamu na
kumwambia aandike:
“Kila siku asubuhi nitakubeba
mpaka kifo kitakapotutenga
nisha”. Jioni nilifika nyumbani nikiwa na maua
mkononi, tabasamu usoni,
nikapandisha ngazi
mpaka ndani. Nilipofika
chumbani mke wangu
alikuwa amelala akiwa amefariki dunia. Kumbe
alikuwa akipambana na
KANSA kwa miezi
kadhaa lakini sikujua kwa
sababu nilikuwa nimetekwa
na Jane. Bila mimi kufahamu, kumbe marehemu mke
wangu alijua kwamba
muda si mrefu atafariki dunia
na alitaka
kuniokoa dhidi ya fikra
yoyote mbaya kutoka kwa mtoto wetu kama
tungeachana muda mfpi
kabla ya kifo chake. Angalau
machoni mwa mwanangu
naonekana kuwa mume
mwenye upendo… WAPENDANAO NATAKA
MJIFUNZE 1) Wengi wanatengana si
kwa sababu
hawapendani, bali hawapeani
muda wa
kusikilizana. 2)Wengi wanaamini
ukiachana na mpendwa
wako ni lazima muwe
maadui. 3)Busara ndani ya pendo ni
zaidi ya mali na
pesa......