Mahitaji
Maini ya kuku 1/2 kilo
Vitunguu vikubwa 2
Hoho 1
Pilipil 1
Limao 1/2
Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chai
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia
Matayarisho
Safisha maini weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu,swaum na tangawizi pamoja (hakikisha vitunguu visiwe vya brown), kisha tia maini, curry powder, pilipili, chumvi ,hoho na limao kisha changanya vizuri na ufunike. Pika mpaka maini yaive na hakikisha yanakuwa na rojo kidogo. Baada ya hapo ipua na yatakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho kama vile chapati, chips, ugali, wali. Ni matam balaa. Enjoy!
Maini ya kuku yapo super markets unaweza kununua kwa portions upendazo nadhani yanaanzia nusu kilo sababu wao huchinjisha kuku na kutenganisha kila kitu kama sehemu ya bidhaa kujiongezea faida maana ukisema uchinje mwenyewe utachinja kuku wengi kupata maini kilo moja ila supermarkets yapo tayari.
Me mara nyingi nabeba firigisi zikiwa na maini full hata sijui km kuna maini ya kuku peke ake!!! Jiko lenyewe nishamsusia dada na hivi sina mume jikoni kuingia kwa nadra sana πππππ
Me mara nyingi nabeba firigisi zikiwa na maini full hata sijui km kuna maini ya kuku peke ake!!! Jiko lenyewe nishamsusia dada na hivi sina mume jikoni kuingia kwa nadra sana