1. Maghala 22 yamelipuka na kubakiwa na ghala moja namba 23.
2. Mabweni mawili ya askari wa JWTZ yaliteketea katika tukio hilo.Hali kadhalika magari 22 yaliyokuwa katika eneo hilo.
Source - Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana bungeni.
Pamoja na uharibifu wote hapo juu,, msemaji wa Jeshi la Wananchi Luteni Kanali Masoud Mgawe asisitiza kuwa hajutapoteza askari hata mmoja.
JE KUNA UKWELI HAPO?
Ina maana Jeshi lilijua kuwa kutakuwa na tukio kama hili? Tukio lilipangwa?Jeshi lilijua mabomu yatalipuka, kwa uhakika kabisa wanajeshi walisambaa katika vitongoji karibu na kambi hiyo kuwaambia wananchi namna ya kujikinga, waliambiwa watalala chini, wazime simu, umeme ulizimwa sehemu kubwa inayozunguka eneo hilo kabla ya milipuko hiyo kutokea.
Kama wananchi wangetulia wakalala chini bila kukimbia hovyo kama walivyoelekezwa basi maafa yangekuwa kidogo sana, lakini tutokana na kutokuwa na mafunzo ya kijeshi na woga wa kupoteza maisha basi hayo ndiyo yaliyowakuta, wengi walikanyagana na wengine kugongwa na magari katika process ya kukimbia kuokoa maisha yao.
Chanzo kimesema Usikivu wa maelekezo ya kijeshi ndiyo yalimsaidia kwani aliingia katika shimo la taka lililopo katika kiwanja chake, yeye na familia kwa muda wa masaa 3 wakati mabumu yanaunguruma. yupo salama.
Kwa hiyo sishangai kauli ya msemaji wa jeshi kuwa Hawakupoteza hata askari mmoja.
mkuu, haya ni maelezo mazito sana! Hebu tupe source, umesikia wapi.Jeshi lilijua mabomu yatalipuka, kwa uhakika kabisa wanajeshi walisambaa katika vitongoji karibu na kambi hiyo kuwaambia wananchi namna ya kujikinga, waliambiwa watalala chini, wazime simu, umeme ulizimwa sehemu kubwa inayozunguka eneo hilo kabla ya milipuko hiyo kutokea.
Kama wananchi wangetulia wakalala chini bila kukimbia hovyo kama walivyoelekezwa basi maafa yangekuwa kidogo sana, lakini tutokana na kutokuwa na mafunzo ya kijeshi na woga wa kupoteza maisha basi hayo ndiyo yaliyowakuta, wengi walikanyagana na wengine kugongwa na magari katika process ya kukimbia kuokoa maisha yao.
Chanzo kimesema Usikivu wa maelekezo ya kijeshi ndiyo yalimsaidia kwani aliingia katika shimo la taka lililopo katika kiwanja chake, yeye na familia kwa muda wa masaa 3 wakati mabumu yanaunguruma. yupo salama.
Kwa hiyo sishangai kauli ya msemaji wa jeshi kuwa Hawakupoteza hata askari mmoja.
mkuu, haya ni maelezo mazito sana! Hebu tupe source, umesikia wapi.
kwasababu kama hivi ndivyo, basi hii ni genocide!
Baba wa Taifa angekuwapo haya mambo yasingefikia hatua hii, watu wanajifanyia mambo bila hata kumwogopa mungu na kwamba siku ya Hukumu ipo. JK unashindwa kabisa kutatua Umeme, Maji na Huduma za afya? mbona hela zipo nyingi tu?
Kama huwezi kwa nini basi unachukua KODI zetu? hii ni dhambi kuchukua pesa za watu then mnatumia kununulia magari yenu ya kifahari - Hivi pale ikulu una magari mangapi Jumla? ya nini yote hayo? hivi tume zako zote unazounda zina umuhimu wa kuwapo? Ni kweli una uchungu wa nchi ya wananchi wake toka rohoni kwako?
Tukisema ukweli mnasema tumetumwa na vyama vya upinzani - jamani sisi ni wananchi wa nchi tu tuna uchungu tunaona nchi as if haina kiongozi tunajiendea tu.
Majeraha ya Mgawo hayajaisha, tumerudi kwenye Mabomu tena na Kamati nyingine tena - Hivi ile Kamati ya Mabomu ya Mbagala ilifikia wapi? ilipendekeza nini kwa serilali au walikula posho wakatengeneza riport ambayo nayo haikufanyiwa kazi?
Hivi kiongozi akidanganya umma anatakiwa afanywe nini? jamani mi naona nchi hii ni kwishinei - wahindi washasema- tanzania hakuna kitu bana, pesa pesa kila pahala nchi yenu kwisha kazi bana.
Kaka ni simple tu, we peleleza vitongoji vilivyo karibu ya kambi - haya yalifanyika. walijua masaa machache kabla ya milipuko kutokea ila walikuwa hawana njisi ya kuyazuia na ndiyo maana wao hawakufa kwani wanajua jinsi ya kujiokoa.
Walijaribu kuwaelimisha wananchi wachache lakini muda haukutosha na ni vigumu mtu wa kawaida kuambiwa ukisikia bomu lazima ulale chini kwani bomu likiamguka na kupasuka hushambulia kuanzia mita 2 hivi kwenda juu kwa 360 degrees kwa hiyo anayekimbia ni rahisi mno kufa kuliko aliyelala chini.
sasa kilichotokea mabomu yakiangua yanaruka na kuwashambulia ndiyo maana utaona watu wamekatika mikono, mabega n.k
Askari wa Basement store walijua "kabla" kuwa mabomu yataripuka na wakawahi kukimbia - tatizo ni kwamba hii taarifa ilikuwa "leaked" as the entire "accident" was pre-arranged!!!!
Mtajua baadaye
Statement mbovu sana hii.... kumbe askari ana uhai bora kuliko wananchi wengine. wanaoa afadhali hajafa hata askari moja.