Pinda lazima Ashitakiwe!!!!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,948
Reaction score
29,506
Mh Pinder kavunja Katiba ya Nchi kwa kuamuru watu WAPIGWE TU! Amekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 100 kifungu kidogo cha pili (2). Lakini kabla ya kuwaonyesha ni jinsi gani Pinder alivyovunja katiba, ngoja niweke ibara yote ya 100 ili tuende sawa:
………………………………………………………………………………………………………
100 (1). Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali pengine nje ya Bunge.

(2). Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.
……………………………………………………………………………………………………....

UFAFANUZI WA KISHERIA:-
Mtaona kwamba kifungu cha kwanza (1) kinampa mbunge uhuru wa kuongea chochote bungeni bila kushtakiwa. Lakini kifungu cha pili (2) kimemuwekea mipaka, KWAMBA anaweza asishtakiwe pale tu jambo atakalokuwa amelitenda au kusema ndani ya bunge halitaathiri katiba au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika.
******************************************************************************
Je, pinder kaathiri (kavunja) Katiba hii au hajaiathiri? Ndio ameiathiri. Kivipi? Tazama vifungu vifuatavyo kwenye sheria mama (Katiba):

KIFUNGU CHA KATIBA KILICHOATHIRIWA NA PINDER:-
Mh Pinder kavunja (kaathiri) Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 13 kifungu cha sita (6), kifungu kidogo (e) ambacho kinasomeka kama ifuatavyo:-

13 (6) (e). Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.
………………………………………………………………………………………………………
HITIMISHO:-
Pinder anashitakika na hakika hapa hachomoki hata kidogo. Wale mnaotetea kwamba analindwa na Katiba mmeona jinsi ambavyo katiba hiyo hiyo inatoa mwanya kwake kushtakiwa? Mkisoma Katiba msiwe mnasoma nusu nusu, someni kwa ukamuilifu wake na bila jazba. Haya tuonyesheni basi ni kifungu gani cha sheria kinachompa uhuru usio na mipaka kutamka au kutenda jambo lolote bungeni halafu asishtakiwe. Haya ni mambo rahisi kutambuliwa na mtu yeyote anayejua kusoma na kuandika. Sio lazima uwe na shahada ya sheria ili ufahamu jinsi Pinder alivyosigina Katiba ya Nchi. Tafakari, chukua hatua!
 
Safi sana Mkuu si unajua elimu yetu Wabongo ni ya kuunga unga kama ya wale Ma Dr wengi ambao Kanerugaba aliwaandikia kitabu na hakuana walikompeleka. Kama zaidi ya asilimia 60% ya watoto wetu wa form Four wanakula Mzinga tutaijua katiba kweli? Ujue pia kwamba hata watawala wapo kiubishibishi na uzoefu tu. Na Pinda mwenyewe alisema wamechoka hawana njia nyingine hapo tutapona kweli?
 

Ndugu yangu, watu wanajua kubisha tu kiubishi kabla ya kusoma sheria kwanza. Hapa Pinder hachomoki--asubiri tu kutolewa jela kwa msamaha wa rais au kama atakingiwa kifua na DPP--kama ilivyo kawaida yake ya 'kufunika kombe mwanakharamu apite'
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi
kwa kweli kauli ya Mh. Pinda inasikitisha na inahudhinisha ukizikatia wanaopigwa na hata kupoteza uhai ni watoto na wakina mama
Hakika Mungu atatenda
 
Noma sana wa tz tubadilike wamezidi kutukandamiza bana inatubd tufanye changes
 
Tangu lini akili ya upeo wa juu ikahindwa na akili ya kiwango cha chini.
heleni anadhani pinda ni msela kama alivyo kijo bisimba la hasha.
saizi ya kijo ni akina geku,rose kamili make hawa wametelekezwa kama kijo.
 

Dar/Dodoma. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemfungulia mashtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokana na kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kwamba wanaokaidi maagizo ya dola wapigwe.

Hatua hiyo ya LHRC imepingwa vikali na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Dk Elieza Feleshi akisema hakuna uhalali wa mashtaka yoyote dhidi ya kiongozi huyo sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.

Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo Bisimba alifungua mashtaka hayo katika Mahakama Kuu jana akisema kuwa wanamshtaki Waziri Mkuu kwa maelezo kuwa amekiuka kifungu cha Katiba Ibara 13 (1). Pinda ametajwa kuwa ni mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 24.

Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia alisema jana kwamba, mwingine aliyeunganishwa katika kesi hiyo ya kikatiba iliyofunguliwa na LHRC na Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

Alisema katika kesi hiyo, kuna jopo la mawakili wasiopungua 20 na kwamba wamepata saini za wananchi 2,029 wanaopinga kauli hiyo ya Pinda na kuunga mkono kufunguliwa kwa kesi hiyo.

Mjumbe wa Bodi ya LHRC, Wakili Dk Ringo Tenga alisema katika kesi hiyo wameangalia zaidi sheria na hasa haki za msingi za binadamu na kwamba kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda inahatarisha haki hizo.

Kauli yenyewe

Wakati wa Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu bungeni, Juni 19, mwaka huu, Waziri Mkuu akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyeuliza: “Serikali ipo tayari kiasi gani kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”

Waziri Mkuu alijibu: “Ni lilelile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.

“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka.” Kesi hiyo itakayosikilizwa na majaji watatu, haina uhusiano na kesi nyingine ambazo wajibu maombi hupewa siku 90 kujibu hoja zilizowasilishwa. Kesi hiyo imefunguliwa kwa mujibu wa Katiba Sura ya Tatu.


Akizungumza juzi kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma baada ya kufungwa kwa Warsha ya Wapelelezi na Waendesha Mashtaka wa Serikali ngazi ya mikoa, Dk Feleshi alisema hakuna uhalali wa mashtaka hayo kwa sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.

“Hii haikuwa kuchochea apige watu, alichosema ni kupiga wale wasiotaka kutekeleza amri halali na zaidi alisema piga lakini si kupiga na kuua,” alisema.

Mkutano huo uliendeshwa chini ya ulinzi mkali huku kukiwa na udhibiti wa kuvuja siri kwa kiwango cha juu. Pamoja na mambo mengine, ulikuwa ukijadili mbinu za kisasa katika kuendesha kesi pamoja na kujiuliza sababu za Serikali kushindwa katika kesi nyingi.

“Kwa sababu lile neno kupiga ni lazima lipewe maana pana huwezi kumpiga tu mtu hivihivi ambaye hakuvunja sheria lakini nilivyoelewa, ilikuwa ni hivyo, ni sawa na mtu ambaye anamshambulia askari,” alisema Dk Feleshi.

Alisema kuna sheria ya kutumia nguvu pale ambako kuna mkusanyiko usiokuwa wa halali pindi raia wanapokaidi kutawanyika kwa hiari hivyo hakuna shaka kauli ya Waziri Mkuu ililenga hivyo.

Hata hivyo, alisema hajapata taarifa za LHRC kumshtaki Waziri Mkuu kimaandishi na kwamba akizipata atatoa ufafanuzi baada ya kuona lengo la mashtaka.



Msimamo

Akizungumza baada ya kufungua mashtaka hayo, Dk Bisimba alisema Waziri Mkuu anaweza kushtakiwa kwa kuwa alizungumza kwa nafasi yake ya Waziri Mkuu na si mbunge na kusisitiza kwamba hakuna aliye juu ya sheria na kudai kwamba kauli hiyo ni kinyume cha Katiba.

Alisema kuwa kila anayevunja Katiba lazima ashughulikiwe kisheria na kwamba mahali pake ni mahakamani tu. Alisema kwa mujibu wa hati hiyo ya madai, kauli na amri kama hizo zinapotolewa na kiongozi mwenye hadhi kama ya mdaiwa wa kwanza (Waziri Mkuu) huchukuliwa kama sheria inayopaswa kutekelezwa na wakala wa utekelezaji wa sheria kama vile polisi. Wadai hao wanadai kuwa kwa ufahamu wao polisi wanaweza kuchukulia kauli hiyo kama amri halali kutoka kwa mkubwa wao na hivyo kuwapiga na kuwatesa watu wasio na hatia, kinyume cha Katiba.

Pia wanadai wanatambua kuwa Ibara ya 100 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa kinga kwa wabunge na uhuru wa maoni bungeni. Hata hivyo, wanatambua kuwa Ibara ya 100 (2) ya Katiba hiyo inawawajibisha wabunge wote chini ya masharti ya Katiba na kwamba kauli aliyoitoa Waziri Mkuu Pinda inakiuka Ibara ya 12(12).

Hivyo wanaiomba Mahakama hiyo itamke kuwa kauli na amri hiyo aliyoitoa Pinda inavunja Katiba.




Mkurugenzi wa taasisi inayofuatilia Mwenendo wa Bunge (Watch), Marcos Albania alidai kwamba wamegundua kuwa kauli hiyo ya Pinda ni moja kati ya matamko makubwa yanayovunja Katiba.

Alisema mbali na shtaka hilo, kuna la pili dhidi ya Waziri Mkuu Pinda, ambalo hawajalifikisha mahakamani ambalo pia linatokana na kauli hiyo aliyoitoa bungeni kwamba: “Sasa wamechoka
 
Noma sana wa tz tubadilike wamezidi kutukandamiza bana inatubd tufanye changes
Kweli mmenyanyaswa sana tangu 2003 hadi leo mbowe amekatalia kwenye uenyekiti poleni ni vema mkabaki tu hapo bavicha.
 
Kijo kachemsha hizo njaa zake za kutumiwa na wanasiasa hata pata kitu,huyu mama akipewa elfu kumi tu anaenda kutoa tamko kweli njaa mbaya,serikali wangemtafutia mtu ili atulie make anahangaika na ukizingatia hajitambui kuwa kachuja atagota tu,
mwanamke kakomaa mpaka uso kwa ajili ya njaa wamsaidie kumpa nafasi hata pale bawacha au pale makao mkuu ya chadema awe hata mpishi tu,make kumtumia na kumwacha hivi wanazidi kumzeesha.
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi
kwa kweli kauli ya Mh. Pinda inasikitisha na inahudhinisha ukizikatia wanaopigwa na hata kupoteza uhai ni watoto na wakina mama
Hakika Mungu atatenda
Mkuu mungu siyo mchaga wala siyo mrundi kama kijo,walimtumia sana ulimboka wakaua wagonjwa wetu hawakutosheka sasa anahangaika na pm,kuna shairi moja linasema usisumbukie kichaa,nikumwacha kijo apayuke mpaka achoke halafu ni bibi ambaye hana kazi ya kufanya acheni ahangaike apate chakula make kama mume hana yani kakosa vyote,
Ukisikia fungu la kukosa ndo yupo huyu mama dini hana,haiba ya kike hana,upeo mdogo,anatumika kama tambala la deki tu,hajitambui halafu kazeeka tumrudishe kwao burudi akiwa angalao anahiyo pumzi make amekatalia tz utadhani wa huku tz.
 

Kama ni lazima kujibu kila post basi ni bora ujielekeze kwenye hoja ndugu.Hoja hapa ni kuhusu jinsi ambavyo waziri mkuu Pinda amevunja katiba kwa kauli yake.Sasa kama unapingana na hoja iliyotolewa ni lazima uonyeshe ubatili wake kupanua mjadala.Unachokifanya ni kumshambulia mtu/watu binafsi badala ya walilolifanya au kusababisha lifanyike,pamoja na ubatili wake.

Ni tabia ya ajabu sana kufanywa na mtu ambaye amejipa mamlaka ya kuitetea serikali.Ni lazima uitetee serikali yako unayoipenda sana kwa hoja.Achana na personal vendatta.

Vinginevyo watu makini wataona unaidhalilisha serikali kwa kuonyesha kuwa imekosa watu makini wa kuitetea.Jiulize kama hauna hoja kwa nini basi uitetee serikali?Ni lazima?Ulazima huo unaletwa na uchumia tumbo au mapenzi kwa serikali?
Kwa jinsi unavyotukana watu na kupuuzia hoja inaonyesha hauna hayo mapenzi na serikali.Inaonyesha dhahiri kuwa wewe ni mchumia tumbo.

Invisible,watu wa namna hii wanaoacha hoja na kushambulia watu binafsi kwa namna isiyo ya kistaarabu karibia kwenye kila topic, itaendelea kuachwa mpaka lini?Hawa wanashusha sana hadhi ya jf tafadhali wadhibitiwe
 
Last edited by a moderator:
LHRC na TLC wamshtaki Waziri mkuu Mizengo Pinda source ITV TANZANIA youtube
 
Last edited by a moderator:
mm sijui jf inamoderator wa aina gani unakuta mtu anatukana watu badala ya kujibu hoja na wao wanaona sawa tu ..hii ni kejeli na kubasilisha mada pia kama tabia itaendelea hii forum inaenda kupoteza maana
 
Kweli mmenyanyaswa sana tangu 2003 hadi leo mbowe amekatalia kwenye uenyekiti poleni ni vema mkabaki tu hapo bavicha.

Usitutoe kwenye mada maana yake akili zako zimehamia kwenye ma------,,na Lipumba kakaa miaka mingapi? au ndo nawewe wa Lumumba wale wa bukt7?
 



Mkuu bila shaka ulichoandika ni sawasawa na akili zako kabisa, pia jifunze vizuri Kiswahili.
 
Porojo tu ''''' ccccm haishitakiwi majaji wako mifukoni
 
Wewe si mzima, sasa suala la kukomaa kwa mtu na kufungua kesi vina uhusiano gani? Na unapomhusisha na Bawacha una maanisha nini? Ina maana bawacha ndio wamemtuma kufungua kesi au ni bawacha waliomtuma Pinder kuropoka bungeni aliporuhusu watu 'wapigwe tu'? Kama haufikiri kwa kutumia tumbo, bila shaka utakuwa unatumia MA------!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…