Defn na maelezo yako yana kaukweli lakini ni tofauti na hali halisi. Kwa maelezo yako, alipojiuzulu Lowasa ilitakiwa system nzima iodoke, mbona haikuwa hivyo?Now basi watanzania tuache kushikiwa akiri zetu na watu wengine wakazichezea na kuzifanya wanavyo taka wenyewe na sisi tukafuata kama wanavyo taka basi........pufikie wakati tujue maana ya system basi kwa msaada zaid "system as a collection of interrelated components that work together toward a collective goal" so leo ukiniambia Pinda anataka kuutema PM unakuwa uongo na uzandiki mkubwa katika anga hii because Pinda is one among the component in a system, so hamna fact ya kumkosha moja na kumchafua mwine. Hatutofika hivyo... na tutoweza kujenga Tanzania mpya kwa taarabu kama hizi zisizo na mashiko kwa Taifa na wananchi
Wadau!!!
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio yanayoonesha wazi kuwa serikali imekosa control juu ya utawala wa nchi. Matukio ya mapambano ya polisi na wamachinga mkoani Mbeya, machafuko ya Arusha na Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Aidha mchakato wa katiba mpya umeielemea serikali na haioni ni wapi pa kutokea. Kauli ya Mbunge wa Monduli na M/kiti wa kamati ya bunge ya ulinzi na Mambo ya nje na PM mstaafu Mhe. Edward Lowassa kutahadharisha kuwa wakati wowote bomu la machafuko laweza kulipuka ni mwiba mwingine kwa serikali. Hivi sasa serikali inasononeshwa na kauli mbiu ya CHADEMA ya peoples power kiasi cha kuifanya kutojua ni nini kitatokea kesho. Suala la Jairo lilimfanya Mhe. Pinda kunyong'onyea na hata kujinyanyapaa mwenyewe mbele ya bunge na hata raia wa kawaida.
Kwa siku za karibuni PM Pinda ameonesha wazi kuwa ni kama kiongozi asiyekuwa na mamlaka yoyote ktk utendaji kazi na kila jambo lazima lifanywe na Rais au maagizo toka kwa Rais pekee. Kwa ujumla amekuwa ni kama ceremonial Prime Minister!! Kwa hali inaonesha wazi amekata tamaa na anaona bora liende ili mradi anapata mshahara na marupu yake. Kwa jinsi mambo yanavyozidi kuharibika ni wazi Rais Kikwete anaweza kufanya mabadiliko makubwa ili kuepuka serikali nzima kuondoshwa madarakani kwa maandamano au kura ya kutokuwa na Imani na serikali bungeni!! Watch out and see!!
Unaota, unauliza au unawakilisha?
Mimi nadhani ni waziri mkuu dhaifu kujiri kuliko wote tuliowahi kuwa nao. Ngoja tuone itakuwaje?
Unategemea waziri mkuu anayetokana na uteuzi wa rais dhaifu aweje? Kwa vyovyote lazima awe dhaifu kama boss wake.Mimi nadhani ni waziri mkuu dhaifu kujiri kuliko wote tuliowahi kuwa nao. Ngoja tuone itakuwaje?
vipi kuhusu sakata lake na magufuli hadi kupelekea magufuli aandike barua ya kujiuzulu? Vipi kuhusu kauli yk juu ya mauaji ya Arusha?hamtambui lolote , pinda ndy waziri mkuu bora kuliko wote waliyomtangulia kwa nn,,maamuzi mengi amekuwa akitoa baada ya kufanya uchunguzi kwa kina mdo maana ktk kauri zake zimekuwa zikitoka kwa umakini mkubwa bila kuingilia mamlaka zilizo juu yake ama chini yake.