Pinda kuutema Uwaziri Mkuu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda kuutema Uwaziri Mkuu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiguu na njia, Nov 13, 2011.

 1. K

  Kiguu na njia Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wadau!!!
  Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio yanayoonesha wazi kuwa serikali imekosa control juu ya utawala wa nchi. Matukio ya mapambano ya polisi na wamachinga mkoani Mbeya, machafuko ya Arusha na Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Aidha mchakato wa katiba mpya umeielemea serikali na haioni ni wapi pa kutokea. Kauli ya Mbunge wa Monduli na M/kiti wa kamati ya bunge ya ulinzi na Mambo ya nje na PM mstaafu Mhe. Edward Lowassa kutahadharisha kuwa wakati wowote bomu la machafuko laweza kulipuka ni mwiba mwingine kwa serikali. Seriali sasa hivi inasononeshwa na kauli mbiu ya CHADEMA ya peoples power kiasi cha kuifanya kutojua ni nini kitatokea kesho. Suala la Jairo lilimfanya Mhe. Pinda kunyong'onyea na hata kujinyanyapaa mwenyewe mbele ya bunge na hata raia wa kawaida.

  Kwa siku za karibuni PM Pinda ameonesha wazi kuwa ni kama kiongozi asiyekuwa na mamlaka yoyote ktk utendaji kazi na kila jambo lazima lifanywe na Rais au maagizo toka kwa Rais pekee. Kwa ujumla amekuwa ni kama ceremonial Prime Minister!! Kwa hali inaonesha wazi amekata tamaa na anaona bora liende ili mradi anapata mshahara na marupu yake. Kwa jinsi mambo yanavyozidi kuharibika ni wazi Rais Kikwete anaweza kufanya mabadiliko makubwa ili kuepuka seriali nzima kuondoshwa madarakani kwa maandamano au kura ya kutokuwa na Imani na serikali bungeni!! Watch out and see!!


  Wakati haya yanatokea Mhe.
   
 2. mtalae72

  mtalae72 Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuwepo na viongozi wenye uwezo mdogo wa kutatua matatizo kama anavyoonekana Mh Pinda ndiyo uthibitisho tosha kwamba katiba yetu ina mapungufu makubwa na imepitwa na wakati. Raisi anateua waziri mkuu anapitishwa bungeni, Raisi anateua wakuu wa mikoa kama hao akina Kandoro na yule wa Arusha, wanaenda kuwaagiza polisi watumie risasi za moto kuzima maandamano ili kujipendekeza kwa mkubwa wao wa kazi aliyewateua. Inabidi tufike mahali wakuu wa mikoa waeleze sera zao kwa wananchi wapigiwe kura ili waweze kuwajibika kwa wananchi wao na siyo kwa raisi anayesafiri kwenda nje ya nchi kila kukicha. Anachoenda kutafuta huko ni kuomba misaada. Kuna nchi gani iliwahi kuendelea kwa handouts?? Hakuna taifa hata moja llimewahi kuondokana na umasikini katika historia ya dunia hii kwa kutegemea misaada. Inakuwaje sisi tuendekeze huu ulemavu wa kutaka tu kuomba misaada?
   
 3. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Mh. Pinda si uwezo mdogo kama mnavyodhani, huyu mzee Pinda si mwanasiasa
  na anatumia sana diplomasia hata kwenye mambo yanayohitaji kufanya maamuzi magumu...
   
 4. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nataka pinda afukuzwe si kujiuzuru
   
 5. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Mh kwani kosa lake ni lipi, ndugu yangu?
   
 6. C

  Capitalist Senior Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 165
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ha! ha! ha! ha! ha!
   
 7. Mbassa

  Mbassa JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 247
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  hata mpumbavu akikaa kimya akatulia atahesabiwa mwenye hekima, utamtambua tu atakapoanza kuzungumza...! Nimeongea kiswahili cha juu.
   
 8. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Magamba wameoza
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  wa kumfukuza nani? yule jamaa kwanza hakuamini na wala hakutarajia kuwa waziri mkuu..so kwake ni zali vile...
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hakuna hoja ya msingi na ya maana hapa juu,mmeandika kwa chuki na ushabiki.....fanyeni kazi acheni kuandika vitu vya kufikirika na kusadikika apa jamvini sio mtu unaamka unakuja na ndoto zako apa kwa great thinkers,utaumbuka.............
   
 11. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mimi Mh. Pinda aliniacha hoi pale aliposhindwa kujua ni nani hasa anaetakiwa kumuwajibisha katibu mkuu, kwangu hapa alionesha udhaifu mkubwa sana hasa pale Luhanjo alivyotokea kwenye vyombo vya habari na kusema si rais bali ni yeye (Katibu Mkuu Kiongozi) anastahili kuwawajibisha makatibu wakuu wote.
   
 12. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Inauma eeeeehh...!!!
   
 13. r

  rachel kusia Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hakika inasikitisha kuona nchi au bunge linaongozwa kwa mtindo wa aina y ake toke huyu ndugu awe waziri mkuu. Hana uwezo wa kutoa hoja au kupinga hoja inayohusu maslahi ya taifa hasa akiwa kiongozi wa shughuli za serikali. Hana uwezo stahili na hili liwaume watu wengi ili waone sababu ya kupinga mswada huo unaosomwa leo kwa mara ya pili, ili washawishike kuingia barabarani kudai haki. Haki ni lazima idwaiwe. Hivyo naungana na watoa hoja kuwa afukuzwe nasio kuachia ngazi mwenyewe.
   
 14. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,110
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Anatafuta urais huyo hawezi kufanya maamuzi
   
 15. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuzingatia maneno yako (yenye rangi nyekundu) Nadhani katiba huijui vizuri, nchi haiwezi kuwa na viongozi watendaji wawili, lazima mmoja awe juu, kwa Tz katiba yetu iko silent kuhusu kazi ya waziri mkuu wakati rais ndiye kiongozi wa serikali na mkuu wa nchi. kwa maneno mengine ni kwamba pm ni ceremonial tu, ni kama cheo cha maalim seif Zanzibar.
   
 16. N

  Natasha Ismail JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Mbasa,
  Nimekipenda hicho kiswahili cha juu uko right.
   
 17. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2011
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  pinda hana pupa kesha mjua mkuu wa kaya akitoa tamko anaweza kugeuka juju kwa juu unaona ,
   
 18. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Jamani wewe mleta mada huyu Lowassa SI waziri mkuu mstaafu unataka kuleta mambo ya Tbc1 hapa?
   
 19. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 80
  Another illogical and baseless writing!!!
   
 20. il dire

  il dire Member

  #20
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  huu usemi nimeupenda sna congrats. Mzee pinda anatakiwa aamue anafuata policy mtoto wa mkulima au nae anakula bati na kushea pamoja na Mafisadi akiresign itakua poa sna.
   
Loading...