Kwa kauli aliyotoa Pinda jana bungeni, inatosha kabisa pasi na shaka kukosa vigezo vya kugombea nafasi ya juu kabisa ya kuongoza nchi hii.
Nasema hivyo kwa sababu ameonekana wazi wazi kutoka kuzima jambo hili kwa maslahi binafsi ama yeye mwenyewe au kulinda kundi la watu waalifu na wezi.
Kwa nchi yenye watu makini swali ni moja tu, kama kwa nafasi yake kwa waziri mkuu na matarajio yake ya urais ameweza kudiriki kufanya vile je akipewa nafasi hiyo kubwa ataficha maovu mangapi na wakati huo atakuwa na rungu la kufanya hivyo?
Pinda umeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati kweli? Natamani ungejua sisi wananchi tunakuonaje huku kitaa.
Hakika umekosa sifa, umekosa upako, umekosa weledi na zaidi umekosa wofu ya Mungu!
Pinda umejitoa mwenyewe katika kinyang'angiro cha urais.
Pinda sasa hata ubunge si halali yako kwani ukifika bungeni unaweza kukosa nafasi ya uwaziri na si hekima kwa mtu aliyekuwa waziri mkuu!
Pinda jana ilikuwa tarehe 20/11/2014 hutasahau tarehe hii!
Nimuda sasa watanzania na ulimwengu mzima ukijiuliza nani anayehusika na hali hii ya sitofahamu ya IPTL na wengi wetu tukiwa na hamu kubwa ya kutaka kujua nani wa kufungwa kengere kwa hili.ila wasi wasi wa watanzania tuliowengi ni kwamba tusije pigiwa ngoma tusiyoijua mapingo yake kisha tukaaza kufunga vibwebwe na kucheza.hapa nikiwa naama kuwa swala hili tusije changanyiwa na harakati za uraisi 2015.kwani hili limejitokeza baada ya kuona jinsi gani mh mizengo pinda anavyotupiwa makombora na wanasisa wenzake ndani na nje ya chama je wanasiasa wetu wanajua wanachofanya kuwa hakina mashiko ndani na nje ya chama coz watanzania wa sasa nitofauti sana na wale wa miaka 5 iliyopita.kwani tonao uwezo wa kuhoji na kufafanua jambo hivyo nivyema wanasiasa wetu wakalijua hili na kuacha moja kwa moja tabia ya kitoto kama wanayofanya sasa.kwani hili naamini haliwezi kumjumbisha mh pinda na chama chake kwa ujumla kwani naamini wamejipanga vizuri kwa hili .na wale wanayumba kimawazo kama mh kagasheki ni watu wanaopaswa kuombewa na kwenye chama kuchukukiwa hatua kali za kisheria.kwani watanzania wanajua yote yanayoendelea ndani ya nchi yao hivyo kama wanasisa au mtanzania yoyote ambaye hana la kusema nibora wakae silent nasio kulipotosha taifa.kwa mimi naona sasa kinachomfanya pinda kunyooshewa mikono sio kuhusika na iptl bali ni kutokana kuwa kaa la moto katka harakati za kugombea uraisi ila mimi naamini kuwa uongozi hutolewa na mungu hivyo hata tumpinge vita kwakila njia kama mungu amemuandikia awe katka nafasi yoyote atakuwa tu.na nivyema watanzania tukajitambua na kutambua mambo kabla ya hawa wanasisa wetu wa maji taka hawajaaza kutupotosha .namalizia kwakusema naipenda nchi yangu na naipenda serikali yangu ya jamhuri ya muungano wa tanzania.na pia mungu ambariki waziri wetu mkuuu na viongozi wandamizi wa serikali yetu ya muungano wa watanzania.
Kwa kauli aliyotoa Pinda jana bungeni, inatosha kabisa pasi na shaka kukosa vigezo vya kugombea nafasi ya juu kabisa ya kuongoza nchi hii.
Nasema hivyo kwa sababu ameonekana wazi wazi kutoka kuzima jambo hili kwa maslahi binafsi ama yeye mwenyewe au kulinda kundi la watu waalifu na wezi.
Kwa nchi yenye watu makini swali ni moja tu, kama kwa nafasi yake kwa waziri mkuu na matarajio yake ya urais ameweza kudiriki kufanya vile je akipewa nafasi hiyo kubwa ataficha maovu mangapi na wakati huo atakuwa na rungu la kufanya hivyo?
Pinda umeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati kweli? Natamani ungejua sisi wananchi tunakuonaje huku kitaa.
Hakika umekosa sifa, umekosa upako, umekosa weledi na zaidi umekosa wofu ya Mungu!
Pinda umejitoa mwenyewe katika kinyang'angiro cha urais.
Pinda sasa hata ubunge si halali yako kwani ukifika bungeni unaweza kukosa nafasi ya uwaziri na si hekima kwa mtu aliyekuwa waziri mkuu!
Pinda jana ilikuwa tarehe 20/11/2014 hutasahau tarehe hii!
Kwa kipi hasa?ebu tuambie ni kwa namna gani mtoto wa mkulima anahusika katika hiyo issue ya Escrow account?
Ebu toeni maelezo kwa namna gani PINDA anahusika katika ufisadi huo?