sasa kuwahamisha Wakurugenzi wa Halmashauri
*Ni siku chache baada ya kuwahamisha wakuu wa wilaya
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameendelea kukunjua makucha aliyoyaficha kwa muda mrefu na kuonyesha rangi yake halisi, baada ya kutangaza mpango wa kuwahamisha wakurugenzi waliokaa kituoni kwa muda mrefu na kujigeuza miungu watu.
Katika hatua yake hiyo Pinda amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza aandae orodha ya watumishi wa mkoa huo ambao wamekaa kwenye nafasi za ajira kwa zaidi ya miaka 10 na kumpelekea ili awahamishie vituo vingine.
Pinda ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na baadaye kuwa Waziri Kamili katika Wizara hiyo, alikuwa mwiba mkali kwa watendaji wa halmashauri hatua iliyomfanya kuongoza kwa mafanikio wizara hiyo.
Hiyo ndiyo iliyolifanya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulipuka kwa shangwe, vifijo na vigelegele wakati Rais Jakaya Kikwete alipowasilisha jina lake kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta wakati huo kumtangaza Pinda kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pinda leo ametoa agizo hilo wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Iringa waliofika kusikiliza majumuisho ya ziara ya siku sita ya Waziri Mkuu kwenye mkoa huo. Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ulioko Mafinga, wilayani Mufindi.
Tafuta wote waliokaa zaidi ya miaka 10. Ni lazima tuwabadilishe... niletee orodha mapema iwezekanavyo, alisema Waziri Mkuu.
Alisema nia ya zoezi hilo ni kuongeza ufanisi kwani watumishi wakikaa sehemu moja kwa muda mrefu wanakuwa butu kwa kukosa ubunifu kwenye kazi zao, wanaota mizizi na kugeuka kuwa chanzo cha matatizo katika baadhi ya sehemu.
Alimtaka pia Mkuu huyo wa Mkoa pamoja na timu yake wasimamie vizuri ukusanyaji wa mapato ili kuongeza kiwango cha mapato cha mkoa huo. Na siyo hilo tu, simamieni vizuri matumizi ya fedha zilizopangwa kwenye miradi mbalimbali ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi mnaowaongoza, alisisitiza.