Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda yuko mkoani Mtwara. Amekwenda kiserikali kushughulikia mgogoro wa gesi asilia huko. Taarifa zinaonesha kuwa Waziri Mkuu Pinda amefanya mikutano mbalimbali na wadau wa kijamii na kisiasa mkoani humo.
Waziri Mkuu Pinda anafahamu vyema kilichompeleka Mtwara. Pia,anafahamu jinsi ya kuwasilisha maoni yake kwa utatuzi wa mgogoro huo. Mh Pinda anajua fika kuwa wana-Mtwara hawataki sana maneno kwasasa.Wanahitaji matendo-utekelezaji wa ahadi moja baada ya nyingine juu ya gesi asilia Mtwara.
Waziri Mkuu Pinda,anajua fika kuwa sera ya 'Gawa na Tawala' huko Mtwara haifai kwa sasa. Sasa inahitajika 'Tawala kimatendo'. Watu wa Mtwara wanahitaji kutumia ipasavyo nafasi yao hii adimu kusikilizwa na kutekelezewa ahadi zao kwa ustawi wao.
Binafsi,siamini kama wanasiasa na viongozi wa kijamii wanaofanya mikutano na Mh Pinda wanaweza kuwaambia kivingine wana-Mtwara waliowaaminisha tayari kwanza wako nao pamoja na 'Gesi kwanza,siasa baadaye'. Wakiwageuka,itakuwa hatari zaidi.
Naamini kuwa Waziri Mkuu Pinda,aliyetoa sadaka hata Mkutano wa Bunge ulioanza leo Dodoma,atafikia muafaka na wana-Mtwara juu ya sintofahamu hii. Pinda ana uwezo mkubwa wa kuanzisha safari ya kimatendo ya Serikali juu ya kadhia hii. Kweli Mh Pinda ameichagua Mtwara!