Pinda aitaka IUCEA kutoa elimu bora

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125








Pinda4%2830%29.jpg

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amelitaka Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) kuhakikisha kwamba vyuo hivyo vinatoa elimu bora ya juu inayokidhi mahitaji ya jamii kwa sasa.
Katika hotuba yake iliyosomwa jana mjini hapa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, Waziri Mkuu Pinda alilitaka baraza hilo kuhakikisha elimu inayotolewa na vyuo inakuwa bora.
“Hebu tuvifanye vyuo vyetu vikuu viwe maeneo mahususi na yenye mazingira mazuri yatakayoimarisha na kutoa viwango bora vya elimu,” alisema.
Aliwataka washiriki wa mkutano huo wa tisa wa mwaka wa IUCEA ambao ni makamu wakuu na wawakilishi wa vyuo, kuwapokea wanafunzi kwa kuzingatia uwezo wa chuo husika katika miundombinu, maabara, vifaa vya utafiti na idadi ya wahadhiri.
Alisema baadhi ya vyuo sasa hivi vimekuwa vikishindana kupokea idadi kubwa ya wanafunzi licha ya vyuo hivyo kutokwa na miundombinu na mazingira mazuri ya kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.
Hata hivyo, Pinda lilipongeza baraza hilo kupitisha azimio kuruhusu uhamaji wa wanafunzi kutoka chuo kimoja hadi kingine kwa kuzingatia kwamba elimu inayotolewa katika vyuo hivyo ina viwango bora vinavyofanana.


Akitoa neno la shukrani baada ya hotuba ya Waziri Mkuu, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mashahidi wa Uganda, Profesa Charles Olweny, alisema ni azma ya baraza hilo kuhakikisha kwamba vyuo vyao vinatoa elimu bora.

Alizishukuru serikali za Afrika Mashariki kwa kutenga fedha za kuendeshea vyuo na akataka vyuo vijiimarisha katika kufundisha na kufanya utafiti.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom