Pilau la Kibunge Magetoni

Koffi Annan

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2018
Posts
2,259
Reaction score
6,697
Leo nimeamka asubuhi nikaona nitoe kitu geto kama Mwachiluwi
Nilienda dukani kununua mahitaji na mengine yalikuwepo ndani

Nikachemsha nyama wakati inaiva nikaandaa viungo kama vinavyoonekana hapo chini

Nyama haikua nzuri sana sababu sio fresh ila pilau lazima linoge,
Msela geto la jirani aliandaa breakfast ya ugali na mayai tukagonga wakati naanza kupika, ilikua saa tano asubuhi


Nikaanza kupika kwa kukaanga viungo kwenye mafuta hadi kuiva, baada ya kuiva nilitwanga viungo vya pilau kwenye glass kwa kutwanga na mwiko(geto hamna kinu)(Saumu, pilau masala na tangawizi) kisha nikaviongeza kwenye mchanganyiko

Kitu kikabadilika rangi kuwa brown nikaongeza njegere hicho kifuko kinauzwa buku tu, kisha nikaongeza supu na maji kipimo cha mchele kilo moja

Nyama na viazi nilikaanga pembeni nikaweka baada ya maji kuchemka ili viazi visitengeze uzito kwenye maji ya mchele, baada ya kuviweka kwa maji nikaweka na mchele kitu kikafunikwa vizuri



Ndani ya dk ishirini geto pakaanza kunukia nikafungua madirisha na mlango kumuumiza roho demu mpangaji mwenzangu aliyenikataa kisa nakunywa pombe


Wakati naandaa viungo nilikata pia viungo vya salad nikatia kwa fridge vipate baridi hapa nimetoa naongeza limao pilipili manga na mayonise, leo tunakula pilau na french salad


Chini kuna ice cubes, smirnof ice, glass zina passion, sprite, limao na juice ya rosela kwa ajili cocktail ya kushushia pilau letu la kibunge,
Glass zipo tatu nilimpigia simu mwana aje kula pamoja na msela tuliyekula nae ugali asubuhi alikua mpiga picha wangu hivyo tupo watatu


Niambie umependa part gani kwenye comments uje kula pilau
 
Kama wewe sii mchoyo taja member watano uliowakaribisha kwenye mlo ilio andaa na kuturusha roho humu jukwaani.
 
Dah hongera masta, jikoni unajitahidi sana jamaa yangu Mwachiluwi anainsapaya wengi ,,, ! Mkuu mnatoka/unatoka kanda ya ziwa ? Ugali asbh then pilau mchana ? Mm ningekula huo ugali asbh mchana ni mwendo wa kupiga desh_
Tulikula kiasi kidogo, alipika geto kwake akaleta, haikua plan πŸ˜†
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…