Kiranja Mkuu
JF-Expert Member
- Feb 18, 2010
- 4,059
- 4,055
Pikipiki zaua 181 kwa miezi minne
JUMLA ya watu 181 wamefariki dunia kwa ajali za pikipiki katika ajali 1,414 zilizotokea kote nchini katika kipindi cha miezi minne kuanzia Januari, huku zikiacha majeruhi 1,206, imeelezwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana wakati akitangaza mabadiliko ya tarehe za kuadhimisha Wiki ya Usalama Barabarani, Mwenyekiti wa baraza linalosimamia masuala hayo, Abbas Kandoro alisema ajali nyingi zilitokana na mwendo wa kasi.
"Ajali nyingi zinatokana na abiria kushabikia mwendo wa kasi na wengi kutovaa kofia za kujikinga kichwa," alisema Kandoro, ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Alisema ndio maana kaulimbiu ya mwaka huu ni "ajali inaua, inajeruhi; usishabikie mwendo wa kasi; mpanda pikipiki vaa kofia ngumu" ambayo aslisema inalenga kuwaelimisha wapandaji wa usafiri huo kuwa makini.
Ongezeko hilo la ajali linaonekana kwenda sambamba na ongezeko la vyombo hivyo vya usafiri, ambavyo katika mwaka mmoja uliopita pikipiki zimekuwa moja ya vyombo vinavyotegemewa sana kwa usafiri wa abiria.
Ongezeko la idadi ya pikipiki linaonekana kuchochewa na unafuu wa bei tangu vyombo hivyo vianze kuingizwa kutoka China na nchi nyingine za Asia. Lakini mara kadhaa polisi wamekuwa wakilalamika kuwa waendeshaji wa vyombo hivyo hawana leseni wala ujuzi wa kutosha na hivyo kufanya operesheni za mara kwa mara kuwakamata.
Akielezea mabadiliko ya tarehe za kuadhimisha siku hiyo, Kandoro alisema katika mwaka huu ambao ni wa kueleke uchaguzi mkuu, siku ya usalama barabarani imebadilishwa na kufanyika mwezi Julai na kwamba kitaifa itanyika mkoani Tanga.
Kandoro alisema wamebadilisha siku hiyo kutoka mwezi Septemba kwa ajili ya kupisha shughuli za uchaguzi mkuu na kwamba wiki ya usalama itafanyika kuanzia Julai 19 hadi 24 ambapo itakwenda sambamba na zoezi la ukaguzi wa magari.
Alisema polisi wa usalama barabarani wataanza ukaguzi wa magari katika wiki hiyo na kuwataka wamiliki wa magari kuhakikisha wanayapeleka ili yakaguliwe na kubandika stika.
Kwa jiji la Dar es salaam ukaguzi utafanyika katika vituo vya Polisi trafiki ,Ikiwa ni Trafili Ilala, Temeke,Oysterbay na mikoani watapeleka vituo vya polisi wa usalama barabarani, alisema Kandoro.