Pigo kwa Israel: UAE yasitisha kununua mfumo wa Iron dome

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
UNITES ARAB EMIRATES YATAMKA KUACHANA NA MANUNUZI YA MFUMO WA ULINZI WA ANGA KUTOKA ISRAEL.

Urudishwaji wa mahusiano mema kati ya Saudia na Iran umeanza kuathiri Israel mara baada ya raisi wa UAE kuachana na manunuzi ya mfumo wa ulinzi wa anga kutoka Israel.

Raisi wa UAE amesema kwamba, kutokana na kurudi kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu - בנימין נתניהו UAE imasitisha kununua mfumo huo wa anga.

United Arab Emirates ilitaka kununua mfumo huo wa ulinzi wa anga kwa ajili ya kujilinda na mashambulizi kutoka kwa wapiganaji wa #Houth kutoka nchini Yemen ambapo #houth wamekuwa wakiungwa mkono na Iran.

Katika makubaliano yaliyofikiwa kati ya Iran na Saudia yanahusiana na kusitisha mashambulizi ya makombora baina na Saudis na Houth huku pia Houth wasishambulie UAE.

UAE ilikuwa bega kwa bega na Saudia vitani kupambana na wapiganaji wa Houth na kuanzia sasa hakuna mapigano na wanajeshi wa Saudis waliopo nchini Yemen wanatakiwa kuondoka muda wowote kuanzia hivi sasa.
 
Huo mfumo Uikraine aliulilia wakanyimwa.wenye mifumo wakadai hawaingilii iyo vita.

Wakubwa tukawaelewa Kwa Nini hawataki inde Uikraine maana ingekua aibu

JamiiForums-2066617636.jpg
 
UNITES ARAB EMIRATES YATAMKA KUACHANA NA MANUNUZI YA MFUMO WA ULINZI WA ANGA KUTOKA ISRAEL.

Urudishwaji wa mahusiano mema kati ya Saudia na Iran umeanza kuathiri Israel mara baada ya raisi wa UAE kuachana na manunuzi ya mfumo wa ulinzi wa anga kutoka Israel...
Yaani ametandikwa na Iran kupitia magaidi hadi akaamua
Huo mfumo Uikraine aliulilia wakanyimwa.wenye mifumo wakadai hawaingilii iyo vita.

Wakubwa tukawaelewa Kwa Nini hawataki inde Uikraine maana ingekua aibu

View attachment 2548502
Usijifanye hujui kuwa Urusi na Israel wanamkata kwenye mambo kama hayo yahusuyo vita.
 
Back
Top Bottom