Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,411
Ajali hii imetokea asubuhi leo External jijini Dar.
Chanzo inadaiwa kuwa ni uzembe wa Polisi wa usalama barabarani. Askari amemsimamisha Dereva wa Lori mita 10 kutoka taa za barabarani..huku mwenye boda akiwa nyuma ya Lori ...
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa mwenye Bodaboda alipojaribu kukwepa Lori hilo akagongwa na Lori lingine nakufia hapo hapo...fuvu la kichwa likapasukia ndani ya Helmet yake.
Baada ya tukio wananchi wakagoma kutoa ushirikiano kwa Askari umati mkubwa uliokuwa eneo hilo wakigomea magari binafsi kubeba mwili wa marehemu....
Hata gari la polisi ilipofika eneo la tukio kwa ajili ya kubeba mwili bado wananchi wakagoma kubeba mwili kwa madai kuwa ni uzembe wao. Mbaya zaidi Askari aliyesababisha ajali hiyo akikimbilia kituoni kwa aibu na woga wa kupigwa na wananchi.